View attachment 3175794
Tundu Lissu ni baba aambiliki nilimuonya hapa majuzi aache mission yake ya kukiua chama hajataka kusikia.
Sasa anaenda kufundishwa adabu na bingwa wa sayansi ya siasa za upinzani Aikael Mbowe.
Kelele ni nyingi mtandaoni lakini hazitomsaidia Lissu na kichapo cha mbwa mwizi toka kwa Mbowe.
Lissu ana wapiga kelele haswa wa mtandaoni, Mbowe ana wapiga kura. Mpaka hapo nani anaenda kushinda?
Uchaguzi wa Chadema una wajumbe wa mkutano mkuu wanakaribia 1300 ambao wana vigezo vya kupiga kura.
Mpaka hapo nafikiri mnaelewa kwa nini Lissu alikuwa anatoa milio mingi kwenye chaguzi zilizokuwa zinaendelea kwa sababu anajua Mbowe alikuwa anapanga safu yake ya kumpigia kura. Yani Mbowe mpaka sasa ana wapiga kura wa kutosha.
Kilichobaki ni Lissu kunyolewa bila maji then akimbie chama kwa hasira yeye na wapiga kelele wenzake.
Baada ya hapo Mbowe ataisuka upya Chadema yake na kurecruit damu mpya nyingi za vijana watiifu wafanya siasa sio harakati.
Lissu anasema uchawa kwenye chama haufai wakati yeye ndio alikuwa chawa namba moja wa Mbowe. Zitto na Kitila wanafukuzwa Lissu ndio kijumbe yupo pembeni ya Mbowe anatoa ushauri wa kisheria.
Dr Slaa anakimbia Chadema, Lissu yupo pale anamnyoosha Dr Slaa.
Yeye ndio alikuwa mastermind wa kuondoa ukomo wa uongozi kwa kuwa alikuwa ananufaika leo anawadanganya chama hakikuwa na watu.
Nasemaje Lissu anatakiwa apigwe vizuri mpaka hata hicho chama anachotaka kuanzisha aghairishe arudi kula pensheni ubeligiji.
Sababu ni moja ni TRAITOR.
Alimsaliti JPM mkamshangilia.
Amefanya kwa Mbowe kipenzi chenu.
Amesaliti watu wengi sana ili yeye ajenge jina lake kwamba anaipenda Tanzania kuliko kiumbe yoyote.
Mimi sio shabiki wa Mbowe ila watu kama Lissu wenye kelele nyingi na hekma sifuri hawatakiwi kuongoza taasisi yoyote. Chadema ipo hapo ilipo kwa vingi ikiwemo hekma za Mbowe. Mbowe ni Nigga ila ni kiongozi mara 200 kumzidi Lissu.
Afrika haitakaa daima iwe na Demokrasia ya maana.
Mbowe ndiye atakayeiua Chadema . Na mwaka huu na mwaka kesho ndio mwisho wa chadema kuwa Chama kikuu cha Upinzani endapo Mbowe atakosa maarifa ya kujua kuwa ni wakati wa kukabidhi kijiti.
Ni kweli Mbowe atashinda kama atagombea lakini ni wazi kuwa anashinda kwa sababu ya ukabila . Tanzania ina makabila 127 lakini wajumbe karibu 60% ni wa kabila la mbowe au watu wa Kaskazini . Kwa hiyo huu ushindi wa Mbowe utajenga chuki kubwa sana kwa makabila mengine na Kanda nyingine . Hili halina ubishi.
Vyama vyote vya upinzani vimekufa kwa sababu ya wenyeviti kukaa muda mrefu madarakani .
Vijana wa Kanda ya Kaskazini acheni upumbavu Chadema hakufikishwa hapo na Mbowe peke yake . Mnashangilia pesa zake sio kingine. Kabla ya chadema Wapinzani wakubwa walikua ni NCCR Mageuzi. Chadema haina wanachama wake wa asili wengi bali wengi ni Kutoka NCCR Mageuzi . Vijana waliojiunga na chadema hivi karibuni hasa wale wa Makabila mengine hawajajiunga kwa sababu ya Mbowe bali kwa sababu ya wanaharakati mahiri na wabobevu wa sheria kama Lisu ,Heche, mwabukusi ,Madereka , Kibatara na Vijana machachari kama Pambalu.
Ni waambie wazi makanisa 126 kwa sasa wanawachukua wachaga kuongoza taasisi yoyote. Na hata ndani ya CCM na serikali kwa ujumla kwa sababu ya kupenda kushikilia kila kitu peke yao na kutothamini watanzania wengine. Kama Chadema imekua na unataka sasa kushika dola 'ni bora Mbowe aepuke mtego ulioko Mbele yake wa kung'ang'ania uenyekiti wa chama kama alivyofanya Lipumba , Mrema, cheyo na wengine ambao vyama vyao vilikuwa na nguvu kubwa vikafa baada ya wenyeviti wao kung'ang'ania madaraka.
Miaka 20 mbowe anataka kufanya nini zaidi na ili iweje?
Kwa nini asibaki kuwa mdau wa CHADEMA na agombee ubunge awaachie wengine ili kukilinda chama na mfumo mzima wa Demokrasia ?
Kiroho safi kabisa Mbowe asigombee ,aache chama kiingie kwenye level ya juu zaidi kidemokrasia kuliko huu ujinga wa kuwajaza wapumbavu kuwa eti kila anayegombea anataka kuua chama ,ujinga mtupu.
Yaani waafrika ni rahisi kudanganywa kwa pesa . Mbowe anajua wazi kuwa hakubaliki kitaifa na kimataifa kama Lisu ndio maana hagombei Urais . Anajua kura za makabila yote Tanzania hazipati na hakubaliki hata kule Hai nyumbani kwao.
Uchaguzi wa mwaka 1995 Mbowe aligombea Jimbo la Hai akiwa kijana mdogo aliyetuhumiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya. Alipigwa kipigo cha mbwa koko na Mgombea wa NCCR mageuzi .
Chadema ikapata nguvu sio kwa sababu ya Mbowe wala Mtei bali kwa sababu ya kufa kwa NCCR Mageuzi.
Kwa hiyo ni lazima Mbowe aepuke wapambe wanaompamba bali ajiulize hivi anaweza kugombea kwa kura za wananchi akashinda kwa kura kutoka makabila yote au anategemea wajumbe Mabepari aliwaweka yeye. ? Lisu anaungwa mkono na watangayika wengi sana toka makabila yote kwa hiyo kama watashinda kwa mizengwe chama kitasambaratika kabisa na Mbowe atapoteza wanachama wengi hasa wa makabila mengine. Watu wa kaskazini kwa sasa hawaaminiki maana hawapigi kura kabisa kwa sababu ya figisu za uchaguzi hivyo hata Urais ujao Chadema itakufa kabisa ..
.
Ni wazi kuwa Mbowe kamwe hawezi kuhamasisha watu hasa wananchi wanyonge ambao ndio wanaoweza kulala barabarani na kufunga njia . Mbowe amezungukwa na Mabepari wachache amabo hawawezi kuandamana ndio maana siku zote amekuwa akitumia watu maarufu kama Dr. Slaa , Sumaye , Lowasa na Lisu mara baada ya kupigwa risasi aligeuka kuwa mtaji wa mbowe .
Chama kina mika zaidi ya 32 Mbowe peke yake ameshika miaka 20 halafu bado anasema hakuna mtu wa kukivusha chama.
Hivi amekivusha wapi wakati mkoa kama Kilimanjaro hana hata Diwani . Eti anategemea maridhiano na CCM. Tangu lini vyama tawala duniani vikawa na maridhiano na watu waoga?
Hivi hajui kuwa CUF ndiyo iliyosababisha pakawa naaridhiano yaliyosababisha vyama vya upinzani vikawa vinapata wabunge na madiwani angalau kwa uchache?
Utawala Afrika ni utajiri ndio maana hakuna mwenye habari na maridhiano bila nguvu kubwa ya kusababisha hata waliokalia ofisi waone kuwa hawapo salama katika viti vya dhulma.
Naamini kuwa Chadema bila Mbowe inawezekana lakini chadema bila wanachama wa makabila yote haifiki popote.
CUF wakati inakufa Chadema walidhani kuwa watapata wanachama lakini cha ajabu haikupata hata mwanachama mmoja . Je, kwa nini hawakupata wanachama toka CUF? Jibu rahisi ni moja watu wenye malengo ya kisasa wanaona wazi kuwa Chadema ni chama cha mtu binafsi na cha kilabila . Waliotoka CUF walijua wazi kuwa Chadema hakuna Demokrasia halisi zaidi ya Mtu mmoja kuhidhi chama . CUF wakakimbilia ACT na sasa ACT ipo ndani ya serikali Zanzibar na Walifanikiwa kuwachukua wanachama wa makabila mengine 126 waliopo Chadema basi ACT litakua chama kikuu cha Upinzani na Mbowe ataendelea kukivusha chama mitandaoni.
Mbowe hatumchukii ila tunasema hali halisi ,hakuna mtu anayeweza kukaa madarakani miaka zaidi ya 20 halafu aendelee kupendwa tuu huku pakikosekana mtu mwingine wa kuongoza . Kama hakuna mtu mwingine ndani ya chama basi chama kimefeli sana .
Hivi kwa mfano Chadema ikishika madaraka itakuaje ,wakati huo mbowe ana teuzi mkononi zaidi ya 2000 zenye ulaji . Je, Ataachia madaraka ? Ni Wapumbavu tu wanaodhani kuwa Eti Mbowe akifanikiwa kuingia madarakani basi ataachia chama. Yaani asikiachie wakati kukiwa hakina dola na maslahi makubwa ake kukiachia kikiwa kimeshika Hazina na Wizara zote na mihimili yote?
Busara itakayowashtua CCM ni Mbowe kumwachia Tundu Lisu Chama . CCM wanamuogopa sana Lisu maana uwezo wake kitaifa na hata kimataifa ni mkubwa sana huku alizijua sana siasa za Dunia.
Mbowe Kama alivyokijenga chama ndivyo atakavyokibomoa kwa kung'ang'ania uenyekiti huku chama kikiitwa cha kidemokrasia.ç