Uchaguzi ni sayansi: Lissu anaenda kugaragazwa vibaya sana na Mbowe

Mapumbavu ya ccm ndio yanajadili uchaguzi wa lissu mbowe.
 
Duh mpaka sinza pazuri kaja na uzi jukwaa la siasa basi shuguli syo ndogo itakuwa
Ngoja tusubirie mtanange

Ova
 


Afrika haitakaa daima iwe na Demokrasia ya maana.

Mbowe ndiye atakayeiua Chadema . Na mwaka huu na mwaka kesho ndio mwisho wa chadema kuwa Chama kikuu cha Upinzani endapo Mbowe atakosa maarifa ya kujua kuwa ni wakati wa kukabidhi kijiti.

Ni kweli Mbowe atashinda kama atagombea lakini ni wazi kuwa anashinda kwa sababu ya ukabila . Tanzania ina makabila 127 lakini wajumbe karibu 60% ni wa kabila la mbowe au watu wa Kaskazini . Kwa hiyo huu ushindi wa Mbowe utajenga chuki kubwa sana kwa makabila mengine na Kanda nyingine . Hili halina ubishi.

Vyama vyote vya upinzani vimekufa kwa sababu ya wenyeviti kukaa muda mrefu madarakani .

Vijana wa Kanda ya Kaskazini acheni upumbavu Chadema hakufikishwa hapo na Mbowe peke yake . Mnashangilia pesa zake sio kingine. Kabla ya chadema Wapinzani wakubwa walikua ni NCCR Mageuzi. Chadema haina wanachama wake wa asili wengi bali wengi ni Kutoka NCCR Mageuzi . Vijana waliojiunga na chadema hivi karibuni hasa wale wa Makabila mengine hawajajiunga kwa sababu ya Mbowe bali kwa sababu ya wanaharakati mahiri na wabobevu wa sheria kama Lisu ,Heche, mwabukusi ,Madereka , Kibatara na Vijana machachari kama Pambalu.

Ni waambie wazi makanisa 126 kwa sasa wanawachukua wachaga kuongoza taasisi yoyote. Na hata ndani ya CCM na serikali kwa ujumla kwa sababu ya kupenda kushikilia kila kitu peke yao na kutothamini watanzania wengine. Kama Chadema imekua na unataka sasa kushika dola 'ni bora Mbowe aepuke mtego ulioko Mbele yake wa kung'ang'ania uenyekiti wa chama kama alivyofanya Lipumba , Mrema, cheyo na wengine ambao vyama vyao vilikuwa na nguvu kubwa vikafa baada ya wenyeviti wao kung'ang'ania madaraka.

Miaka 20 mbowe anataka kufanya nini zaidi na ili iweje?
Kwa nini asibaki kuwa mdau wa CHADEMA na agombee ubunge awaachie wengine ili kukilinda chama na mfumo mzima wa Demokrasia ?

Kiroho safi kabisa Mbowe asigombee ,aache chama kiingie kwenye level ya juu zaidi kidemokrasia kuliko huu ujinga wa kuwajaza wapumbavu kuwa eti kila anayegombea anataka kuua chama ,ujinga mtupu.

Yaani waafrika ni rahisi kudanganywa kwa pesa . Mbowe anajua wazi kuwa hakubaliki kitaifa na kimataifa kama Lisu ndio maana hagombei Urais . Anajua kura za makabila yote Tanzania hazipati na hakubaliki hata kule Hai nyumbani kwao.


Uchaguzi wa mwaka 1995 Mbowe aligombea Jimbo la Hai akiwa kijana mdogo aliyetuhumiwa kufanya biashara ya madawa ya kulevya. Alipigwa kipigo cha mbwa koko na Mgombea wa NCCR mageuzi .
Chadema ikapata nguvu sio kwa sababu ya Mbowe wala Mtei bali kwa sababu ya kufa kwa NCCR Mageuzi.

Kwa hiyo ni lazima Mbowe aepuke wapambe wanaompamba bali ajiulize hivi anaweza kugombea kwa kura za wananchi akashinda kwa kura kutoka makabila yote au anategemea wajumbe Mabepari aliwaweka yeye. ? Lisu anaungwa mkono na watangayika wengi sana toka makabila yote kwa hiyo kama watashinda kwa mizengwe chama kitasambaratika kabisa na Mbowe atapoteza wanachama wengi hasa wa makabila mengine. Watu wa kaskazini kwa sasa hawaaminiki maana hawapigi kura kabisa kwa sababu ya figisu za uchaguzi hivyo hata Urais ujao Chadema itakufa kabisa ..
.

Ni wazi kuwa Mbowe kamwe hawezi kuhamasisha watu hasa wananchi wanyonge ambao ndio wanaoweza kulala barabarani na kufunga njia . Mbowe amezungukwa na Mabepari wachache amabo hawawezi kuandamana ndio maana siku zote amekuwa akitumia watu maarufu kama Dr. Slaa , Sumaye , Lowasa na Lisu mara baada ya kupigwa risasi aligeuka kuwa mtaji wa mbowe .

Chama kina mika zaidi ya 32 Mbowe peke yake ameshika miaka 20 halafu bado anasema hakuna mtu wa kukivusha chama.
Hivi amekivusha wapi wakati mkoa kama Kilimanjaro hana hata Diwani . Eti anategemea maridhiano na CCM. Tangu lini vyama tawala duniani vikawa na maridhiano na watu waoga?

Hivi hajui kuwa CUF ndiyo iliyosababisha pakawa naaridhiano yaliyosababisha vyama vya upinzani vikawa vinapata wabunge na madiwani angalau kwa uchache?
Utawala Afrika ni utajiri ndio maana hakuna mwenye habari na maridhiano bila nguvu kubwa ya kusababisha hata waliokalia ofisi waone kuwa hawapo salama katika viti vya dhulma.

Naamini kuwa Chadema bila Mbowe inawezekana lakini chadema bila wanachama wa makabila yote haifiki popote.

CUF wakati inakufa Chadema walidhani kuwa watapata wanachama lakini cha ajabu haikupata hata mwanachama mmoja . Je, kwa nini hawakupata wanachama toka CUF? Jibu rahisi ni moja watu wenye malengo ya kisasa wanaona wazi kuwa Chadema ni chama cha mtu binafsi na cha kilabila . Waliotoka CUF walijua wazi kuwa Chadema hakuna Demokrasia halisi zaidi ya Mtu mmoja kuhidhi chama . CUF wakakimbilia ACT na sasa ACT ipo ndani ya serikali Zanzibar na Walifanikiwa kuwachukua wanachama wa makabila mengine 126 waliopo Chadema basi ACT litakua chama kikuu cha Upinzani na Mbowe ataendelea kukivusha chama mitandaoni.


Mbowe hatumchukii ila tunasema hali halisi ,hakuna mtu anayeweza kukaa madarakani miaka zaidi ya 20 halafu aendelee kupendwa tuu huku pakikosekana mtu mwingine wa kuongoza . Kama hakuna mtu mwingine ndani ya chama basi chama kimefeli sana .

Hivi kwa mfano Chadema ikishika madaraka itakuaje ,wakati huo mbowe ana teuzi mkononi zaidi ya 2000 zenye ulaji . Je, Ataachia madaraka ? Ni Wapumbavu tu wanaodhani kuwa Eti Mbowe akifanikiwa kuingia madarakani basi ataachia chama. Yaani asikiachie wakati kukiwa hakina dola na maslahi makubwa ake kukiachia kikiwa kimeshika Hazina na Wizara zote na mihimili yote?

Busara itakayowashtua CCM ni Mbowe kumwachia Tundu Lisu Chama . CCM wanamuogopa sana Lisu maana uwezo wake kitaifa na hata kimataifa ni mkubwa sana huku alizijua sana siasa za Dunia.

Mbowe Kama alivyokijenga chama ndivyo atakavyokibomoa kwa kung'ang'ania uenyekiti huku chama kikiitwa cha kidemokrasia.ç
 
Mtoto wa Mjini !!
Bila Mbowe saa Hizi Lissu angekuwa shimo la Tewa !! Hiyo asisahau na awe na adabu kwa mwamba !
 
Point yangu hapo tu uliposema "Alipomsaliti Magufuri na sasa anamsaliti Mbowe" akili yako na rangi yako ishajulikana. Alafu mbona nyinyi wa upande huo ndio mnaumia sana baada ya Lissu kutangaza nia ya kugombea nafasi ya uwenyekiti CHADEMA?
 
4. Mbowe yupo kibiashara zaidi hivyo ni lazima atumie pesa zake zote kuakisha anaendelea kulindi biashara zake
 
Ngoja wamfariji na makelele ya mitandaoni ataona moto
 
Daah ww umekurupuka
 

So what? Unataka kusema nini? Kwani hajui kuna kushinda na kushindwa? Atapoteza nini? Na atakuwa wa kwanza duniani? Uvccm mmechanganyikwa tangu jana mna pumba tupu! Eti umemuonya? Hahaha we nani? Unatoka kamasi wapi hapo? Unajipa umuhimu kwa wanaume!🤣🤣🤣
 
Kwa kweli wana hubiri demokrasia na jina lao lina sema chama che demokrasia na maendeleo alafu wanasema mbowe anatosha daah. Lissu ni shujaa na ana maono. Mbowe kawa mwenyekiti zaidi ya 20yrs je anataka kufia kwenye umwenyekiti. ..? Demokrasia izingatiwe
 
Kitendo Cha mkt kuja amelewa kwenye ufunguzi wa mikutano ya hadhara pale furahisha na kusema CCM oyeeee,

Kiliniudhi sana.
 
Pamoja na yote hata kama siyo Lissu au Mbowe nadhani wanahitaji damu mpya kama akina Heche. Mbowe imetosha.
Chama kiwe na sura ya kitaifa vinginevyo ni kipigo cha mbwa mwizi kwenye masanduku ya kura.
2020 ni mfano ambao hautafutika kwa mkoa wa Dar
Waliopita kugombea ubunge hawakuleta picha ya kitaifa.

2015 wananchi mkoa wa Dar wakihamasishana kumchagua Lowasa.
Cha ajabu watu wengine tena kwenye mabaa wakipanga himaya ya watu fulani tu.
Ina maana mtumike tu kuwachagua kama zana za kilimo?
Kama siasa ndio hiyo hatupigi kura tunabaki majumbani.
 
Mbowe kamkaribisha kwenye mpambano, watoane damu asije sema alizuiwa kugombea.

Lakini Lissu anajua fika anaenda kushindwa. Lengo lake nini? Kuua chama.
Lissu ameshanusa kuwa 2025 CHADEMA hawata muweka kama mgombea Urais.
Kwahiyo lengo lake ni kukihama chama na tobo pekee aliloliona ni hiki alichofanya.
 

View: https://www.instagram.com/reel/DDhooTEijc7/?igsh=bml4ZHYxOHEzejlz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…