Kuna populatipn kubwa sana ya watu wa Kanda ya Ziwa ambayo haikufurahia kabisa utawala wa Magufuli.
Tusidanganyike na fikra kama vile watu wote wa Kanda ya Ziwa walimfurahia Magufuli, halafu tukaanza kuleta chuki dhidi ya Watanzania wenzetu walioumizwa na utawala dhalimu wa Magufuli kama ilivyo kwa wengine wengi.
Ifahamike kuwa Magufuli hakuwa msukuma, lakini alitumia ujanja ule ule, kuwaona wasukuma ni wajinga, akiwadanfanya kuwa na yeye ni msukuma, ili wamwunge mkono kwa sababu ya kabila lake.
Baba na babu yake marehemu walihamia Nzera (Sengerema), wakitokea Kigoma. Na huko Kigoma, mzee Machalila, babu yake marehemu, alihamia akitokea Burundi.
Hivyo mambo ya ajabu ya marehemu kuyahusisha na kabila la wasukuma, ni kutowatendea haki wasukuma.
Mfahamu kuwa marehemu ni wa ukoo wa mzilankende (yaani ngedere), na hakuna ukoo wa namna hiyo usukumani.