UCHAMBUZI: Hoja za NECTA kufuta utaratibu wa kutangaza shule bora na wanafunzi bora hazina mantiki kwa 100%

Naunga mkono hoja yako. Kama wanaona uwanja hauko Sawa basi watenge makundi 2. Kuwe na orodha ya shule za serikali na ya shule binafsi.
 
Unachokiongea ni sahihi kabisa.
 
Mvaa Kobaz kawekwa pale kwa mikakati maaalum. Yaaan Mekkha akae kusoma shule za Vatican zilizojazana top ten?
Halafu baadae Sheikh akae kusoma shule za Istiqama 10 zilizopo mkiani🤣🤣 mnajisumbua nyie.
Hii ni kauli ya hovyo na ya kipumbavu kupata tolewa week hii. Sidhani kama kuna Wakristo wenye kufikiri kipumbavu namna hii. Mimi nina marafiki Wakristo wengi wana akili hawawezi andika upumbavu kama huu.
 
Eeh!! Swala ni watu wanaondaliwa katika mazingira tofauti na kuja kufanya mtihani mmoja sio sawa.

Mkenda huwezi kumlaumu kwani yeye ndo hawezi kufanya reforms za haraka katika elimu ni taratibu kaanza na hilo .
Wewe kwa akili yako umeona ni sawa aanze na kuondoa ushindani wa ubora wa elimu na kuficha takwimu?
Badala ya kuanza na kuboresha mazingira kwanza
Usiunge tu mkono sio kila kiongozi anakuwa sahihi
 
Ukitaka kujua ubora wa skuli uitakayo kila matokeo yakitoka fanya kutafuta mwenyewe siyo serikali ikuwekee ubaoni na kukutangazia skuli yako.

Wewe amka na walimu wako fanyeni recruit search alafu iteni media zote pigeni ukunga.
Tusiingize chuki za kijinga kwenye serikali ya wananchi
Ni jambo la aibu serikali kuwa na chuki na shule ilizozisajili zinazofanya vizuri
Hizi chuki za kijinga ndo zilikuwepo kwenye awamu Fulani kwenye sekta binafs tuzikatae
 
Hii ipo vizuri sana, hizo shule zinazojisifu kwamba zinafaulisha vizuri mitihani ya necta Sasa zirudi kutufurahisha sisi wazazi kwa kufundisha vizuri watoto wetu, Kila matokeo ya darasani watoto wote wawe wanashika namba moja na hayo masomo kama hesabu watoto wote wapate A hapo watakuwa wameonyesha uwezo wa shule zao Bora.
 
Mlikuwa mnalobby bana ..

Utaratibu huu mpya hakika ni safiii
 
Naunga mkono hoja yako. Kama wanaona uwanja hauko Sawa basi watenge makundi 2. Kuwe na orodha ya shule za serikali na ya shule binafsi.
Ahsante mkuu,
Hapo wakifanya hivyo wataleta ubaguzi
Hapo dawa ni serikali iboreshwe mazingira ya elimu yafikie ubora unaotakiwa
Sio kulazimisha na kukasirikia shule binafsi
 
Mimi nadhani NECTA wameshindwa tu kusema Ukweli kwa kuhofia baadhi ya sintofahamu

Ukweli ni kwamba hakuna fair competition, mashule mengi ya private yanafanya mtihani kabla ya siku ya mtihani

Japo sio shule zote ila shule nyingi wanafanya umafia sana na inaonekana ni ngumu kuzuia


Binafsi nimesoma government, ila wakati nipo form five, form six walipokuwa wanatoka chumba Cha mtihani wanafurahi sana kwa kusema possible (mitihani uliovuja) ni WA kweli

Wakati nipo form six , nilibahatika kusolve mtihani Usiku (Tena discussion) na kesho yake tukaukuta huo huo Hadi nukta.

Sasa Kama hiyo ni government, ambapo watu wametumiwa, je private kupoje???


Binafsi sikatai juhudi za shule za private katika kufundisha, miundombinu nk, ila Wana umafia sana
 
Huo utakuwa ni upambuvu mkubwa sana,
Kujaribu kuua ubora wa elimu kwa ajili kumfurahisha mtu mmoja
 
Changamoto Pia ipo kwa hao baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya. Kuna baadhi ya shule japo zinakuwa za mwisho katika wilaya zao au mikoa yao unakuta zimefanya vizuri ila wao hawaelewi na walimu wa shule hizo au wakurugenzi wanakiona cha mtema kuni sasa sijui huwa wanataka shule zote ziwe za kwanza.

Hivyo hata kama NECTA wakirudisha huo utaratibu wa kutangaza nafasi za shule basi hao wakuu na wafuatiliaji ngazi zote waelimishwe kuangalia ufaulu wa shule na sio Nafasi ya shule imekuwa ya ngapi.

Ndio maana uamuzi wa NECTA unaweza kuwa mzuri japo sababu zilizotumika ndio zikawa na ukakasi.
 
Huo utakuwa udhaifu wa necta , dawa ni kushughulikia huo udhaifu
 
Tujadiri kwa kina kidogo hili kwa kuangalia na kuzingatia majukumu ya hao NECTA, kama kazi yao ni kutunga, kusimamia, kusahihisha na kutoa matokeo kwa ujumla, kusimamia ubora wa mitihani, sasa ni kwa namna gani wanakuja na hoja ya ubora wa mazingira ya kujifunzia, huoni kama kuna idara/taasisi imetegea hapo?
 
Kutotangaza shule bora na shule dhaifu na wanafunzi bora na wanafunzi dhaifu ni utaratibu wa KIPUMBAVU! PERIOD!!
 
Siasa za bongo hazijawahi kuleta Jambo la msingi
Kila MTU akiamka anakuja na agenda zake za kidwanzi.

Watu wanatakwimu Hadi za shoot off targets sembuse best students
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…