Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya Kugombea Urais - Juni 8, 2020

Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya Kugombea Urais - Juni 8, 2020

Wakuu upo usemi kwamba Mungu akupi vyote. Aghalabu Wazungumzaji wazuri huwa si watendaji wazuri.

Watu wengi waliovizuri mdomoni si watendaji wazuri.

Nawasilisha.
Huu utafiti ulifanya lini? Tupe reference.
 
Hivi hatuwezi kuwa na mfumo mbadala wa kuendesha maisha usiohusisha siasa? Ukweli mimi binafsi siipendi siasa. Baadhi ya sababu zinazonifanya nisiipende siasa ni UNAFIKI, UONGO na UBINAFSI wa wanasiasa waliowengi.
 
Kwa ushawishi wa Makundi yepi Hali ameyaumiza yote
Wafanyakazi wakihoji nyongeza za mishahara yao wapi atawajibu kwani hamuoni ndege za ATCL? Wakulima wakiulizia kufa kwa mazao yao ya biashara na kutolipwa madeni yao atawajibu kwani SGR inadondoka toka mbinguni?
Yaani kila swali lina jibu na mkibisha polisi watawashughulikia.
Kiukweli hana hoja ya msingi ukilinganisha na plan za Lissu.
 
Ila tusibweteke na magoli haya ya kuongoza ktk mechi hii ya 2020 maana CCM Mpya ina wachezaji 13 badala ya 11, yaani refa, mshika kibendera, kamisaa wa mechi wote wapo timu CCM Mpya huku sisi tuna wachezaji 11 kama sheria za football zinazosema.
 
Wafanyakazi wakihoji nyongeza za mishahara yao wapi atawajibu kwani hamuoni ndege za ATCL? Wakulima wakiulizia kufa kwa mazao yao ya biashara na kutolipwa madeni yao atawajibu kwani SGR inadondoka toka mbinguni?
Yaani kila swali lina jibu na mkibisha polisi watawashughulikia.
Kiukweli hana hoja ya msingi ukilinganisha na plan za Lissu.
Pesa za nyongeza ya mishahara hakuna.
Pesa za kulipa mafao Hakuna.
Za kuwashughulikia wapinzani zimejaa tele
Za kujenga majengo yasiyo na faida kiuchumi zaidi ya sifa ya kukumbukwa zimejaa tele.
Sasa mfanyakazi kipi cha kujivunia.
Yeyeto anaweza ongoza nchi, kinachoongoza ni katiba na sheria na sio mtu.
 
Wakuu upo usemi kwamba Mungu akupi vyote. Aghalabu Wazungumzaji wazuri huwa si watendaji wazuri.

Kwenye ujengaji hoja Lissu yupo vizuri sana lakini ikulu hayahitajiki maneno pekee bali matendo zaidi. Tumpime Lissu kwenye rekodi zake za utendaji na ndio kitu muhimu zaidi.

Unaweza ona Lissu anafaa kuwa Rais wa JMT kwa kuwa tu anajenga hoja vizuri lakini kumbe nafasi inayomfaa Lissu ni kuwa mshauri tu wa Rais.

Watu wengi waliovizuri mdomoni si watendaji wazuri.

Nawasilisha.
Tumpime kwa push up basi! Si atakuwa na washauri? Labda awatishe na kuwatumbua wasimwambie ukweli! Reasoning ya Lisu ni kubwa, he is capable of making sense out of rubbish
 
Lisu anajiandaa 2025 sio hii awamu bado saana
 
Lissu hawezi kushinda urahisi hata tume ikisimamiwa na Pompeo.

Akaanza kuhesabu kura moja moja tuseme tumpe miezi mitatu ahesababu kura zote mwenyewe.

Mie nimejionea mafuriko ya Lowassa Arusha kisha nikakaa nikasimamia kura na kuzihesabu vituo ambavyo nilitarajia angepata 95% ya kura zote....mwisho akapata 53%.

Lissu hapa JF anashinda mchana kweupe tu ila tulitoka kwenye server atacharazwa vibaya.

Magufuli hana mpinzani mwaka huu tena umaarufu wake utambeba saana kwa kipindi hiki....
 
Pamoja na kwamba Magufuli hafai Urais, Sikuwai kuona kama Lissu anafaa, though tunataka mbadala lakin, Wakipangwa wawili Ntamchagua tu Lisuu kama Nilivyomchagua Magufuli nikamuacha Lowassa,

Hawa wawili wakilinganishwa naona Lissu ana Unafuu kidogo angalau 25% ya sifa za urais anazo
Kusema ukweli nilikuwa Team Magufuli 2015. Baada ya hapo kuna maeneo Mengi sikuona amefanya sawa kwa miaka hii 5. Sikuwai kuona mbadala wake na nilishakata tamaa. Ila kiukweli Lissu amenishawishi sana. He is very matured kwa sasa kisiasa na nafikiri anastahili nafasi hii ya juu.

Vyombo vya ulinzi visimuwekee kauzibe waache watanzania waamue kwa haki na Nina uhakika tutapata maendeleo ya kweli
 
Back
Top Bottom