Amani iwe nanyi Wadau.
kama wote mnavyojua leo ndo siku ile ambayo watanzania kwa pamoja wameweza kushuhudia hotuba ya kwanza kutoka kwa gwiji la upinzani, ndugu Tundu Antipas Lissu. Hotuba iliyokuwa imejaa utulivu, akili, busara na hekima iliyotukuka.
Kama kawaida CCM walipanga yao, kwanza walipanga vijana wao kushambulia kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo facebook na Youtube ili tu kujaribu kuonesha umma na dunia kuwa Lissu hakubaliki ila kiukweli Lissu kwa hotuba ya leo ameonesha kuwa amejiandaa vizuri na amejipanga vizuri kuwa Raisi wa Tanzania mwaka 2020.
Lissu ameweza kuelezea kwa kifupi na kueleweka sana hoja zote zilizotikisa kwenye miaka hii Mitano ambazo sio tu Chadema ila hadi CCM na watanzania kwa ujumla zimewagusa sana.
Hakuna ambae hajui kuwa wafanyabiashara wakubwa na wakati wamenyanyaswa sana kwenye kipindi hiki cha miaka Mitano, kwenye hili Lissu kapiga mulemule, hakuna ambayo hajui kuwa awamu ya tano imeharibu sana kwenye uchumi, kilimo na diplomasia, kwenye haya tena Lissu kapiga mulemule.
Alipomaliza Lissu ni pale alipoelezea kwa jinsi gani suala la kuonea watu na kukiuka katiba limekuwa linaumiza watu na hapa tena Lissu amepiga mulemule.
Mwisho kuonesha jinsi gani amekomaa, pamoja na kupigwa risasi 16 amesema amesamehe na hatolipa kisasa. Hapa Lissu kawa sawa na Mandela aliyewasamehe makabulu na Papa John Paul 2 aliye msamehe kijana aliyempiga risasi. Lissu ameonesha amekomaa sio tu kiuongozi ila hata kihekima na busara.
Hotuba ya leo ya Lissu imegusia mambo mengi ikiwemo kurekebisha mfumo wa sheria na vyombo vya ulinzi na usalama ili vifanye kazi kwa weredi. Lissu kusema kweli kumaliza yote.
Ukweli lazima tuseme , Ingawa vyombo vya Habari vya Tanzania ikiwemo Azam , ITV na vingine vikubwa kuogopa hata kurusha Habari ya Lissu kutangaza nia leo. Ila hotuba yale imesikika na imewasisimua watu wengi nikiwemo mie. CCM wametumia mbinu ya kuvitisha vyombo hivi kwa makusudi ila Naona nguvu ya Lissu ni kubwa sana kuliko hujuma dhidi yake.
Itoshe kusema Lissu amethibitisha kuwa anatosha akiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2020
Kura yangu anayo akipitishwa na Chadema.
Ushauri kwa Chadema. Isambazeni video ya leo ya Lissu kwenye mitandao mbalimbali kuanzia Insta, Facebook, Twitter na Whatsup’ watu wengi waione maana mkitegemea vyombo vya Habari vya Tanzania vilivyobanw na Ccm mtapoteza.
Jioni Njema!
tundu lisu anakubalika na watu wachache sana mitandaoni ambao asilimia kubwa mtu mmoja anatumia majina kumi tofauti kumsifia huyo tundu lisu.
Kwenye maisha ya kawaida mitaani watu walishamsahau huyo tundu lisu, pia watu wengine hawamjui kwamba hata ni nani kwa sababu hakuna cha maana alichofanya kwenye hii nchi, au unaweza kuniambia ni mambo gani aliyofanya huyo tundu katika nchi?
Watanzania mnatakiwa mjue kwamba uongozi wa nchi sio kama kilanja wa shule, kwamba hata kilanja asipokuepo mambo shuleni hayakwami,
kwa kifupi tundu lisu hafai kua Rais sababu moja ni mtu ambae asilimia kubwa anategemea uungwaji mkono kutoka nchi za ulaya na Marekani na katika historia nchi hizo za ulaya na Marekani asilimia kubwa ndio zilizotufanya tuwe maskini kama Taifa hadi sasa.
Pili tundu lisu hafai kua Raisi sababu ni mtu kigeugeu na mwenye ndimi mbili, 2015 walimsaliti mwenzao Dr Slaa na kumuunga mkono Edward Lowasa ambae miaka yote yeye na wenzake wanachama wa chadema waliaminisha watanzania kwamba Lowasa ni fisadi mkuu.
Katika hilo jambo yeye tundu lisu ndio kinara wa kumsafisha Edward Lowasa katika mikutano mingi wakati wa kampeni 2015.
Tatu tundu lisu hafai kua Raisi sababu ni mtu msaliti , amekaa mda mrefu huko ulaya baada ya kupona akizunguka nchi mbalimbali za huko ulaya akitangaza nchi kwa wazungu kwamba nchi ya Tanzania itengwe na dunia na pia akitaka nchi inyimwe misaada ya aina mbalimbali na nchi za ulaya na Marekani kwa sababu ya yeye kupigwa risasi.
Lengo la kutangaza ubaya wa nchi kwa wazungu ni kuhakikisha Raisi anashindwa kutawala ili lengo lao kuiba mali za Tanzania wakishirikiana na nchi chache za ulaya kutimia.
Nne tundu lisu hafai kua Raisi sababu ni mtu ambae anayo ajenda ya kuifanya nchi kua kichaka cha wazungu kufanyia ushenzi wao, ukirejea hotuba zake za kuunga mkono ushoga, kuunga mkono mikataba ya kishenzi ambayo ilikua inatuibia madini, yeye tundu lisu akajitokeza hadharani kuwatetea wazungu kwamba wana haki ya kutuibia madini sababu ya mikataba ya kipumbavu.
Pia rejea namna yeye na Chama chake chadema walivyotoa muongozo kuhusu ugonjwa wa COVID 19.
Nina mambo mengi ya kuandika kuhusu udhaifu wa tundu lisu, ila mengi nitaendelea kuyaelezea kadiri mjadala unavyoendelea.
Hivyo kwa nchi changa kama yetu ni hatari sana kua na Raisi wa aina hiyo sababu kwenye hotuba yake ameelezea tu kushughulikia utawala wa kisheria, haki za wananchi, kuwalinda matajiri lakini amesahau kwamba hakuna Taifa liliwai kuendelea kwa hoja zake za kitoto na kusadikika.