Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya Kugombea Urais - Juni 8, 2020

Uchaguzi 2020 Uchambuzi: Hotuba ya Tundu Lissu kutangaza nia ya Kugombea Urais - Juni 8, 2020

Hivi hatuwezi kuwa na mfumo mbadala wa kuendesha maisha usiohusisha siasa? Ukweli mimi binafsi siipendi siasa. Baadhi ya sababu zinazonifanya nisiipende siasa ni UNAFIKI, UONGO na UBINAFSI wa wanasiasa waliowengi.
Kama unachukia ujinga huu basi unangana na wapenda mavadiriko kuiondoa ccm madarakani kwa kuwa ccm ndo baba na mama wa mauchafu yote haya
 
Kunywa hata leo hii maana Lissu kuwa rais ni unstoppable
Thubutuuu. Lisu anaisaidia tu CCM KUWA USHINDI wake ulikuwa na upinzani mkali. Na hivyo kuonekana kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki na kikatiba.

Kama atakuwa Rais wa JMT Mimi nitajiua kwa kula sumu siyo kwa jiwe ninalolijua Mimi.
 
Mkuu yaani umepiga penyewe sina lakuongeza ngoja waje wanasaccos ya Chadema watoe mapovu ya Omo ya kutosha.

Jana nilisema leo wanaccm watajazwa humu mitandaoni kuhakikisha wanapunguza sumu ya hotuba ya Lissu. Na kwakweli hilo liko dhahiri kwa kila mtu kujionea. Pigeni kazi jamani, huyo Lissu ameongea mambo yatakayosumbua sana mbele ya safari.
 
Thubutuuu. Lisu anaisaidia tu CCM KUWA USHINDI wake ulikuwa na upinzani mkali. Na hivyo kuonekana kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki na kikatiba.

Kama atakuwa Rais wa JMT Mimi nitajiua kwa kula sumu siyo kwa jiwe ninalolijua Mimi.
Membe ndiye mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM mwaka huu ni suala la muda tu.
 
Na: Generose Nsanzugwako, Dodoma
Juni 8, 2020

Leo Tundu Lissu amehutubia kile alichoita hotuba kwa watanzania kupitia mitandao ya kijamii kuhusu kuchukua fomu ya kugombea uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA.

Kwanza nimpongeze kwa kuchukua maamuzi hayo maana ni haki na demokrasia yake japo uraisi wake ni wa mitandaoni kuanzia kutangaza nia, kuandika barua uenda hata kuchukua na kurudisha fomu.

Lakini hapa nitajikita katika vipaumbele alivyotoa katika hotuba yake iwapo itatokea akachuguliwa kuwa Rais wa nchi ya Tanzania.

Kipaumbele chake cha kwanza ni kuwa akiwa Raisi hatojificha Singida COVID-19 ikitokea. Sasa hiki ni kipaumbele au utopolo. Akili yake kwa kuwa haiko sawa anaomba Tanzania iathirike na corona atangaze vifo na wagonjwa. Hii ni akili ya mfa maji.

Kipaumbele chake cha pili ni kuwa hatolipiza kisasi akichaguliwa kuwa raisi kwa waliompiga. Hiki ndo kichekesho kwa sababu mpaka sasa a ajua waliompiga risasi ndo maana alimficha dereva wake ili asitoboe siri. Ndo maana Jeshi ya polisi linamsubiri yeye kama mhusika namba moja na dereva wake ili uchunguzi wa kesi yake ukamilike.

Kipaumbele cha tatu ni kuwa atafanya kila liwezekanalo kukuza uchumi wa nchi. Sijui ana tatizo gani au kwa kuwa akili yake kwa sasa ni mbovu. Tangu lini Lissu akawa na akili ya kukuza uchumi wa nchi wakati yeye na Zitto walikuwa makuwadi ya kampuni ya Acacia wakilipwa mabilioni ya hela ili kuhakikisha nchi inaibiwa madini. Lissu huyu huyu amelipwa pesa kuzunguka nchi za ulaya ili kupinga juhudi za Raisi Magufuli za kuibiwa madini. Sasa Lissu rudi uone kama Acacia kama bado ipo na upate takwimu za madini kwa sasa.

Ajenda yake ya nne ambayo hakuiongelea sana ni ushoga. Ikumbukwe Lissu, Maria Sarungi na Fatume Karume ni wafuasi wa ushoga na wameutetea sana kipindi cha nyuma. Anaidai akiwa Raisi ushoga utahalalishwa kama haki ya binadamu. Hili tu linatosha kukunyima kura kwa sababu taifa hili sio la mashoga bali watu wa Mungu.

Lissu ameshindwa kuelewa kuwa Uraisi ni taasisi inayohitaji mtu makini, asiyepayuka na ambaye akili yake ni timamu.

Lissu unahitaji kuelewa kuwa watanzania wanahitaji kusikia vituo vingapi vya afya vimejengwa.

Watanzania wanahitaji kusikia kuwa wana madawa ya kutosha mahospitalini.

Watanzania wanahitaji kusikia watoto wakisoma bure shule ya msingi na sekondari na walimu wakilipwa stahiki zao.

Watanzania wanahitaji kusikia wakipata maji salama kwa afya zao.

Watanzania wanahitaji kusikia wakitengenezewa miundo mbinu ya barabara, majini na angani ili kusafiri na kusafirisha bidhaa zao.

Watanzania wahitaji kusikia wakiwashiwa umeme vijijini kwao tena kwa bei rahisi.

Watanzania wanahitaji kusikia wakifaidi matunda ya rasilimali zao za madini.

Watanzania wanahitaji kusikia vibaraka vya mabeberu kama Lissu, Zitto na wengineo mnafishwa mahakama kujibu tuhuma za uchochezi na uaini.

Hayo na mengine niliyotaja hapo juu ukirudi Tanzania ndo utakuta watanzania walishayapata kwa serikali ya awamu ya tano.

Sanasana utakachovuna ni hela ya mabeberu ya kufanyia kampeni ambayo mmeivuna. Hii hela itamsaidia sana baada ya kampeini kwani hatokuwa na chanzo cha mapato na bado anahitaji matibabu ya akili.

Mwisho nikukaribishe nchini ushindane na watu wenye akili ili ugalagazwe uamini kuwa uraisi sio wa kukurupikia bali ni mkakati
Sijui umeandika nini chuki zenu mtakufa nazo,hotuba yake umeisikia au umeadithiwa? Kumbuka aliyehaidi kutoa milioni 50 kwa kila kijiji,kutoa mikopo kwa wanachuo wa Elimu yajuu pamoja na kupambana na mafisadi na mahakama ya mafisadi hajagusia ata moja.Tulia dawa iingie.
 
Miongoni mwa hotuba bora kwangu hapa Tanzania ni pamoja na hii,lisu chaguo LA wengi hasa ambao tumekosa ajira ktk serikali hii
 
Uchaguzi ungekuwa wa HURU na HAKI mchuano ungekuwa mkali.

Tume ya uchaguzi - sisiemu
Mahakama - sisiemu
Vyombo vya dola - (wakuu wa mikoa/wilaya)makada wa sisiemu
Ingekuwa watu wanaogopa hilo basi leo hii DRC wangekuwa bado wanatawaliwa na Kabila
 
Pamoja na kwamba Magufuli hafai Urais, Sikuwai kuona kama Lissu anafaa, though tunataka mbadala lakin, Wakipangwa wawili Ntamchagua tu Lisuu kama Nilivyomchagua Magufuli nikamuacha Lowassa,

Hawa wawili wakilinganishwa naona Lissu ana Unafuu kidogo angalau 25% ya sifa za urais anazo
Tatizo ana mihemko mno, kitu kingine aliharibu sana kuwatetea Acacia na kuwa mtetezi wa ushoga.
 
Nilionya na ninaendelea kuonya. Huyu asipodhibitiwa anaweza kusababisha machafuko hapa nchini. Inaonesha wazi mabeberu wanataka kumtumia kuhujumu amani yetu.
Amani ikose kuvurugwa na anayeteka na kuua watu ije ivurugwe na mtu anatekekeza wajibu wake wa kikatiba?umevimbiwa na maharage ya wapi wewe?
 
Jana nilisema leo wanaccm watajazwa humu mitandaoni kuhakikisha wanapunguza sumu ya hotuba ya Lissu. Na kwakweli hilo liko dhahiri kwa kila mtu kujionea. Pigeni kazi jamani, huyo Lissu ameongea mambo yatakayosumbua sana mbele ya safari.
Lissu ni sawa na wanasaccos asiye na uwezo wa kuchambua hoja ni utopolo tu umemzidi
 
Membe siyo mwanachama wa CCM tena labda kama atagombea kupitia CDM?
Mkutano Mkuu ndio wenye mamlaka ya kumuondolea uanachama wake, subiri utashangazwa Mkuu. Mwenyekiti wetu Magufuli mwoga sana.
 
Huwa sipendi ushabiki wa mapenzi ya mtu. Naweza kupenda CCM ishindwe lakini kumbe hakuna uwezekano. Mpasuko sijui kama upo lakini kama upo ni kwa viongozi. Wale wapiga kura, kwetu vijijini hawajui lolote kiasi cha kuwafanya wawe na hasira hizo. Ukisema wanafahamu mpasuko huo, utakuwa unawapa ufahamu mkubwa sana kinyume na tunavyojifahamu wa-TZ.
Ila wamepigika hatari awamu hii, kumbuka maisha yao yanawategemea wa mjini
 
Back
Top Bottom