Uchambuzi: Uyahudi alizaa watoto wawili, mkubwa aliitwa Ukristo na mdogo akaitwa Uislam

Ukristo sio dini bali ni uhusiano (relationship) na ushirika (fellowship) na Mungu aliyehai. Kukaa makanisani bila kuwa na hivi vitu ni sawa na kuwa mpagani.
 
Kumbe hata Uislamu wenyewe huujui. Waulize kama hicho nilichoandika hapo sio kweli.

Mkuu hizo dini nilishazifanyia uhakiki tangu nipo Darasa la sita miaka hiyo. Uliza wanaonijua. Hivyo ukiona Jambo naliandika ujue nimeshalipatia Hesabu yake. Wala sina ushabiki Mimi. Ninachoangalia ni ukweli tuu
 
Kama lengo lako lilikuwa ni kujaribu kujipima katika matumizi ya lugha pengine umefanikiwa,nimesema pengine kwa sababu nimewaachia wataalamu wa lugha waamue mimi sio mtaalamu.Lakini kuhusu content umeonyesha kuwa ni kichwa kitupu. Next time kabla hujaandika mambo yanayokuzidi uwezo wa kuelewa nenda kajifunze kwanza then ndo uende mbele za watu ukazungumze vinginevyo utakuwa unaaibisha tu ukoo wako.
 

Tupe hoja ili tupime na watu wahakiki kuwa kweli kichwa changu ni kitupu.
Kama ni hizi porojo zako basi ni Sawa Mimi ni mtupu
 
Hebu tuelimishe sisi tusiojuwa lolote, kabla ya Yesu kusulubiwa akisema ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke lakini kama nu mapenzi yako basi yatimizwe.

Pale msalabani pia akasema her Mungu wangu mbona umeniacha? Na kabla ya kukukata roho Yesu akasema Baba mikononi mwako roho yangu naiweka akafa.

Hebu nifafanulie huyu Mungu naye ana Mungu wake? Ana baba yake? Je ni yupi ndio Lord?
 
😂😂😂
Unajua maana ya Dini Kwanza Mkuu?
Wewe na vijukuu vya jamaa wa mapangoni mtasema dini ni mfumo wa maisha.😂 Hiyo definition inamaanisha kila mtu anayo dini.

Mimi nakupa tafsiri yangu, dini ni jitihada za mwanadamu kufanya mambo mazuri akiamini kwamba kwa namna hiyo anampendeza na kumuabudu huyo mungu wake kwa kufuatisha taratibu fulani zilizowekwa.
 
Yakobo na Yusuph hawa sio brothers bali ni baba na mwanaye.(Next time msizungumze vitu sensitive wakati wa kusubiri game ya UEFA).

Pengine ulitaka kusema Isaka na Ishmael.Hawa kweli walikuwa watoto wa baba mmoja ingawa mmoja alikuwa ni mtoto wa mke halali na mwingine mtoto wa kijakazi.

Kimsingi ahadi zote ambazo Mungu alimpa Abraham zilikuwa juu ya uzao wake kupitia kwa Isaka lakini ndugu zetu walipokuja baadaye wakatwist kwamba ahadi zote zile zilikuwa ni kwa Ishmael.

Biblia yote kimsingi inazungumzia uzao wa Isaka kisha Yakobo mwanawe. Baada ya hapo story yote ya Israel inatoka na watoto wa Yakobo ambaye alibadilishwa jina na kuitwa ISRAEL na Mungu (Hence the nation ISRAEL)

Kimsingi both can't be true. So kama tukitaka kupata ukweli tutatumia ushahidi wa kihistoria na pengine hata kisayansi kuujua ukweli ni upi. But,the is no need kwa sababu majibu yalishatafutwa na ukweli ushajulikana.


The bible has never been Wrong and hence everything written in there is an ABSOLUTE TRUTH.
 
Mungu ni mmoja, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
 
Tupe hoja ili tupime na watu wahakiki kuwa kweli kichwa changu ni kitupu.
Kama ni hizi porojo zako basi ni Sawa Mimi ni mtupu
Hakuna hoja ya kukupa hapo, everything you have written is garbage.

Christainity is not a religion,its a FAITH.Ukristu ni IMANI. Kama umeshindwa kutofautisha DINI na IMANI chochote utakachoandika after hakiwezi kuwa sahihi.

Pengine unaufahamu Uislam kwa kiasi unachokijua wewe which still is almost nothing,lakini umeprove hujui chochote kuhusu IMANI ya kikristu.

Kiufupi ni kwamba hakuna uhusiano wowote kati ya hiyo dini na Imani ya kikristu ,sio kihistoria,kifalsafa wala kimaadili and on top of that they do not worship the same GOD.
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120] Hakika umenena vyema ingawa siamini.
 

Mkuu ulichoeleza ni Kama unaelewa upande mmoja wa shilingi alafu upande mwingine huujui.

Mungu aliumba Imani mwanadamu kupitia Imani akaunda Dini
Akaumba Akili mwanadamu akaunda Elimu
akaumba Uzuri binadamu akaunda urembo
Akaumba Sauti binadamu akaunda Lugha

Huwezi tenganisha Imani na Dini.
Ukristo ni Imani iliyounda Dini ya Ukristo.

Unapofafanua Jambo lazima ulijua Kwa mapana yake.
Sipo hapa kuleta ushabiki au kutetea kundi lolote isipokuwa Ukweli
 

Hilo fundisho la Trinity unajua liliingia mwaka gani kwenye Ukristo?
Maana usiwe unazungumzia mambo usiyoyaju.
Ni lini mtazamo wa Mungu yupo katika Nafsi tatu uligundulika, na ipi asili ya Dhana hiyo?
 
Kusema kila kilichopo kwenye biblia ni ukweli ni kutoijua biblia,kutoisoma Wala kujua historia yake
 
Nini tofauti ya Imani na dini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…