Uchambuzi: Uyahudi alizaa watoto wawili, mkubwa aliitwa Ukristo na mdogo akaitwa Uislam

Uchambuzi: Uyahudi alizaa watoto wawili, mkubwa aliitwa Ukristo na mdogo akaitwa Uislam

Kristo ndio njia ya kweli na uzima..hakuna atakaye pata ufalme wa mbinguni bila imani na haki katika kristo Yesu.

Uislamu uliletwa na shetani ili kuchakachua maandiko na kuwapoteza watu katika njia ya upotevuni.

Ndio matendo ya hizi dini mbili nanajionyesha wazi..ukristo umejikita kwenye upendo furaha na amani kwa wote....ila hali ukiristo umejikita kwenye chuki wivu na ugomvi fitna na utengano haya yako wazi kabisa na tunajionea sasa jinsi gani dunia inahangaika na matendo ya kigaidi yatokanayo na imani hii.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
God iz Good All the time
Binadam amebadilisha vingi katika kutafuta ahueni na faida yake katika jambo fulan
Cha msingi jifunze kwa utashii mkubwaa sana maana miluuzi ni Mingi sana ukishindwa (Ishi katka upendo)
 
Mleta mada ameonyesha ni jinsi gani Ukristo ulivyo tofauti na uyahudi na uislam
Lakini uyahudi unafanania sana na Uislam,ila ukristo haufananii kabisa na uyahudi na uislam. Hasa kwenye falsafa ya Mungu ni nani na yupoje.
 
Braza angu alinipa hadithi ya Yacobo na Yusuph nikiwa chalii tukisubiri gemu za Uefa nilimuelewa sana akasema hao ni ndugu na hata hapa unaona wanatofautiana sana ni kwa kuwa wengi hawana uelewa wa hizi dini zetu wamekaririshwa kuchukiana wakati ni ndugu moja...baadae nikafatilia kwenye Biblia nikakuta ni kitu kile kile hata mitume wengi ni wale wale...
Umechanganya madesa wewe, rudi akakusimulia upya !
 
Wivu, chuki na roho mbaya iliyokujaa ktk moyo dhidi ya uislamu, na ndio maana bila ya hata muna sema eti (maria mama wa mungu) mungu wenu ana2 mama, baba mlezi , bibi, babu napia alikufa
Hoja dhaifu sana hii
 
Uelewa wako wa sababu iliyopelekea Yesu kuja duniani na matokeo ya kufa na kufufuka kwake ni mdogo sana, completely negligible.

Ushauri wangu ni aidha uyatoe maisha yako kwa Yesu Kristo au uende ukajipatie mabikira 72 kwa Allah.
Be honest, jiwe limekupata penyewe. Usione aibu, kubali tu.
 
Wewe jamaa kumbe ni empty head. Shabik maandazi.
Wewe uko level ya chini sana kufanya mdahalo na mimi. Angalia wanazuoni wako wanavyohangaika huku.

 
Anaandika Robert Heriel,

Ukristo na Uislam ni watoto wa baba mmoja aitwaye Uyahudi.
Licha ya kuwa Ukristo ulitangulia kabla ya Uislam lakini Uislam kwenye ishu ya maadili upo makini zaidi kuliko Ukristo, na dini hizo zote mbili baba yao ni dini ya Kiyahudi (Judaism).

Ukisema Ukristo ni mtoto mtundu au mkaidi aliyegundua mavumbuzi mengi hautokuwa unakosea. Labda kwa vile ni mtoto wa kwanza. Uislam ni lastborn wa Uyahudi ambao umeendelea kushika baadhi ya Falsafa na principles za baba yake.

Dini ni maadili ambayo yamejengwa kwa msingi wa imani. Kuamini katika miungu, lakini lengo kuu la dini ni ishu ya maadili.

Ukristo na Uislam hauwezi kusimama wenyewe bila kutegemea Uyahudi, hiyo haiwezekaniki kwani huyo ndiye baba yao. Hata hivyo kama utatazama kwa jicho lisilo la makengeza, unaweza kuona bila ya shaka kuwa Ukristo unahangaika kujitegemea wenyewe pasipo kufuata misingi ya baba yake Uyahudi.

Licha ya kuwa lastborn Uislam anaonekana kuwa alimpinga na hamtaki baba yake Myahudi lakini ukiangalia mtazamo na falsafa zake bado zinajikita kwa baba yake. Wakati huo Ukristo yeye kwa vile ni firstborn ambaye kisheria ndiye mrithi kwa nje anaonekana kumkubali baba yake Myahudi lakini kimatendo na kifalsafa anampinga baba yake.

Baada ya watoto kukua wanahama na kwenda kuanzisha miji yao. Ukristo boma/mji wake aliuita KANISA
Uislam boma/mji wake akauita MSIKITI. Wakazaliwa watoto, Ukristo ukazaa Wakristo wakati Uislam ukazaa watoto Waislam ambaye babu yao ni Uyahudi.

Falsafa chache za baba Uyahudi ukilinganisha na watoto wake wawili:
1. Mungu ni mmoja,
Ukristo hauamini katika Mungu mmoja isipokuwa mmoja katika utatu Mtakatifu. Baba, mwana, na roho mtakatifu.

Uislam unaungana na Baba yake Uyahudi kuwa Mungu ni mmoja na wapekee asiye na mshirika. Yaani hakuna cha utatu wala upili. Katika falsafa hii Ukristo unapingana na baba yake huku Uislam ukiungana na Baba yake.

2. Mungu ni mtakatifu/msafi
Ukristo: Mtoto huyu anasema kwa mdomo jambo hilo lakini kivitendo anapingana nalo.
Ukristo huweza kumruhusu hata mtu aliyejinyea asimame madhabahuni, mtu mchafu wa mwili na mavazi.

Ukristo mtu huweza kwenda kanisani akaingia na viatu lakini akifika kwake akavua viatu.
Ukristo umejijenga zaidi katika kanuni ya kusafisha ndani zaidi kuliko nje. Lakini umesahau kuwa uchafu unatokea nje kwenda ndani.

Ukristo unaruhusu mtu kula jambo lolote kwa imani, siyo ajabu Ukristo mtu kula nguruwe au panya au mbwa kwa sababu ni kwa imani.

Uislam: Mtoto huyu anasema mdomoni na kutekeleza kwa vitendo. Falsafa na kanuni hizi amezitoa kwa baba yake aitwaye Uyahudi. Mungu ni msafi/mtakatifu na anataka watu wake wawe watakatifu/wasafi.

Uislam umeiga tabia ya baba yake kugawa vitu visafi na vichafu. Kipi chafaa kula na kipi hakifai. Uislam hauwezi kula uchafu.

3. Ndoa na mahusiano.
Ukristo: Mtoto huyu amemuasi baba yake dhahiri shahiri. Uyahudi kuna sheria ya talaka lakini Ukristo kaamua kuiweka kapuni. Hii inafanya watu wawe watumwa kwenye mahusiano yasiyo na tija.

Ikiwa siyo lazima kuwa na mahusiano na Mungu iweje iwe lazima ukioa mke au kuolewa na mume muishi maisha yote? Ndoa ni mkataba wa hiyari kwasababu unahusu upendo. Upendo ni hiyari, kama watu watapishana waachane. Uyahudi unaeleza hivyo, Ukristo hautaki.

Ukristo huyu mtoto kapingana na baba yake. Uyahudi haukatazi mtu kuoa wake wengi, unaruhusu ndiyo maana kunasheria zinazohusu mtu atakayetaka kuoa wake wengi.
Ukristo hautaki na umepinga jambo hilo.

Uislam: Mtoto huyu licha ya kuonekana kama muasi kwa babaye lakini bado anatumia kanuni zilezile za baba yake.
Mtoto huyu anaruhusu Talaka kama kuna mambo yanaenda ndivyo alivyo. Pia mtoto huyu anaruhusu wake wengi ingawaje ameweka kikomo kuwa ni wake wanne.

4. Mavazi
Ukristo: Mtoto huyu anatumia u-firstborn wake vibaya. Ukristo unaruhusu mtu avae atakavyo kwani Mungu haangalii mavazi, anaangalia moyo wa mtu.
Siyo ajabu wafuasi wa Ukristo kuwaona wakivaa nguo zisizo na stara.

Hii ni tofauti na baba yake Uyahudi ambaye alikuwa na sheria za mavazi na kusisitiza watu wavae kwa adabu hasa wanawake wajistiri kutokana na maumbile yao kuwa na ushawishi.

Uislam: Mtoto huyu mwenye madeko ambaye yeye kila kitu lazima aone anaonewa, yeye anaungana na baba yake katika hilo. Uislam unazingatia maadili ya mavazi. Wafuasi wa mtoto huyo wamekuwa wastaarabu/waungwana sana katika hilo.

5. Mwanaume ndiye kuhani.
Ukristo: Ukristo kadiri siku zinavyoenda unazidi kuonyesha kupuyanga na kutumia urithi wa u-firstborn vibaya kama alivyofanya Esau. Ukristo unaruhusu mtu yeyote kuwa kuhani hata kama ni mwanamke. Wakati baba yake Uyahudi jambo hilo kwake kamwe lisingewezekana.

Nafasi ya mwanaume kwenye Ukristo huchukuliwa kuwa sawa na mwanaume. Wakati mzee Uyahudi hilo kwake lilikuwa ni ushetani.

Uislam: Ni kufuru kubwa kwa mtoto wa kike kusimama madhabahuni kuwahutubia wanaume. Hilo uislam alilichukua kama lilivyo na analitekeleza. Uislam umempa nafasi kubwa mwanaume kama ilivyo kwa baba yake Uyahudi.

6. Mungu hakuzaa wala hakuzaliwa.
Ukristo: Unatanabaisha kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, kupitia kwa Bikra Maria aliyepewa mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu. Hoja hii ndiyo mzizi wa utatu mtakatifu na wengine hufikia hatua ya juu kabisa kufikiri au kusema Yesu ni Mungu, ilhali hilo kamwe hata kwa akili ya panzi haliwezekaniki.

Baba yao Uyahudi kama ungesikika ukisema maneno hayo, basi ilikuwa umeamua kutaka kuuawa kwa kupiga mawe kwani ungekuwa umekufuru na kufanya dhambi kubwa mno.

Uislam: Mtoto huyu yeye anabaki na msimamo wa baba yake kuwa Mungu hajazaa wala hajazaliwa. Na Hilo ni kosa kubwa la kukufuru.

7. Neema
Ukristo: Ukristo huu ndiyo msingi namba moja yaani huwezi tenganisha Ukristo na neema.
Kwamba mtu akifanya kosa basi anastahili kupewa nafasi ya pili, neema pasipo kuhukumiwa.
Wakati baba yake Uyahudi yeye kanuni yake ni haki. Kwamba mtu akikosea basi aadhibiwe, na mtu akipatia basi apewe zawadi yake (thawabu).

Uyahudi ulijikita kwenye mwili na roho. Wakati Ukristo unajikita katika roho pekee. Hii ni kumaanisha kinachopewa neema ni roho sio mwili. Yaani mtu akiomba neema ya msamaha, basi roho yake ndio ipewe second chance lakini mwili uadhibiwe.

Lakini wafuasi wa Ukristo wakalazimisha kuwa mwili na roho vyote vipewe neema[emoji23][emoji23]. Huku wakishikilia kanuni isemayo usihukumu usije ukahukumiwa au samehe saba mara sabini. Wakisahau kuwa mwili ndio unafanya makosa wakati huo roho ndiyo hufanya dhambi[emoji23][emoji23]. Mwili huadhibiwa na dunia kwa makosa yake wakati huohuo roho huadhibiwa na Mungu kwa dhambi zake.

Uislam: Mtoto huyo yeye kafuatisha kwa kiasi kikubwa kanuni na sheria na falsafa za baba yake. Mwenye makosa aadhibiwe kulingana na makosa yake na vile sheria zisemavyo.

Zingatia, binadamu hawezi kusamehe dhambi isipokuwa Mungu. Ila anasemehe makosa kwa sababu ya mwili ndiyo hufanya makosa na roho ndiyo itendayo dhambi. Kumaanisha, roho ndiyo inamuasi Mungu halafu mwili unamfanyia makosa binadamu mwenzako au kiumbe au mazingira yanayokuzunguka.

8. Hukumu
Ukristo: Mtoto huyu anajieleza kuwa atakayehukumu ulimwengu ni Kristo/Yesu.
Na Yesu ndiye atakuwa mtawala wa kila kitu. Hii ni tofauti na falsafa ya baba mtu Uyahudi. Yeye anajua Mungu ndiye mtawala na ndiye atakayehukumu viumbe vyake kwa haki. Zingatia neno viumbe inamaanisha vinavyoonekana na visivyoonekana. Hata Yesu pia ni kiumbe.

Uislam: Huyu mtoto anaungana na baba yake Uyahudi kwa kusema, hukumu atakayoitoa ni Mungu. Na kila kiumbe atahukumiwa kulingana na yale aliyoyafanya.

9. Urithi na mirathi
Ukristo: Umejikita zaidi katika mambo ya kiroho na kusahau mambo ya kimwili. Ukristo unajikita katika urithi wa Ufalme wa mbinguni pekee. Ilhali baba yake akijikita kwa yote mawili.
Uyahudi ilitoa utaratibu wa namna ya kurithisha mali kwa haki, na namna ya kutoa mirathi endapo mtu atakufa.

Ukristo jambo hilo limeachwa liamuliwe kidunia, hapohapo dunia kwa mujibu wa Ukristo inaongozwa na shetani[emoji23][emoji23]. Unaona mambo hayo!

Uislam: Mtoto huyu kamuiga baba yake na kuongeza baadhi ya vitu. Kajikita kiroho na kimwili.
Urithi na mirathi kwa uislam imefafanuliwa namna itakavyogawiwa. Uislam haujaliacha jambo hilo liamuliwe na walimwengu kwani shetani ndiye mlimwengu mwenyewe.

Mpaka hapo sina la ziada, siyo kazi yangu kukuambia kipi chakuamini au kipi ni sahihi na kipi sio sahihi. Nilikuwa naeleza habari za watoto hao wawili wenye wafuasi wengi.

Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es Salaam.
Kusema uyahudi umezaa uislamu ni kukosea sana, Kwasababu uislamu unatokana na Mtoto wa Ibrahim anayeitwa Ismail ambaye hajawahi kuwa MYAHUDI kabisa. Uyahudi unatokana na Mtoto wa YAKOBO anayeitwa YUDA.
Ila ni sahihi, kwa upande wa UKRISTO( kuwa UKRISTO ni mwendelezo unaotokana na maboresho ya dini ya KIYAHUDI).
Kwahiyo, UKRISTO unatokana na Mtoto wa kiimani (KIROHO) wa Ibrahim ( ISAKA ) na UISLAMU unatokana na Mtoto wa kimwili wa Ibrahim ( ISMAIL).
 
Roma waliichakachua sana biblia wakapunguza vitabu wakabadili baadhi ya maneno,mwisho wa Kitabu wakaandika" Ole wake aongezaye au apunguzae neno ndani ya Kitabu hiki"how bright are they?
 
Kusema uyahudi umezaa uislamu ni kukosea sana, Kwasababu uislamu unatokana na Mtoto wa Ibrahim anayeitwa Ismail ambaye hajawahi kuwa MYAHUDI kabisa. Uyahudi unatokana na Mtoto wa YAKOBO anayeitwa YUDA.
Ila ni sahihi, kwa upande wa UKRISTO( kuwa UKRISTO ni mwendelezo unaotokana na maboresho ya dini ya KIYAHUDI).
Kwahiyo, UKRISTO unatokana na Mtoto wa kiimani (KIROHO) wa Ibrahim ( ISAKA ) na UISLAMU unatokana na Mtoto wa kimwili wa Ibrahim ( ISMAIL).
Jamani haya maelezo mnayatoaga wapi? Uyahudi umetokea kwa YUDA mtoto wa Yakobo? How? YUDA ni mtoto tu kati ya watoto 12 wa kiume wa Yakobo lakini unaposema wayahudi unajumuisha wa Israel wote ambao ni muendelezo wa vizazi vya hao watoto wote 12 wa Yakobo.

Ibrahimu alikuwa na watoto 8,Pamoja na kwamba Ismael( Mtoto wa kijakazi) ndiye aliyezaliwa kwanza Isaka ndio mtoto wa ahadi ambaye Mungu alimuahidi angemzaa kupitia Sara.

Hapa wasituyumbishe UISLAM hauna origin yoyote umeibuka ghafla tu na mtu kaja kuedit story za kale ili ionekane ina uhusiano na dini na imani zilizotangulia kwa lengo la kupata credibility. Na hii ndo sababu iliyopelekea story nyingi za Quran kuwa zinamakosa makubwa sana ya kihistoria.
 
Uislamu umeanzishwa na Vatican featuring Muhammad and creating a god called Allah.
Isingekuwepo Qu'ran ningekubaliana na mawazo yako ila kila nilisoma Qu'ran moja na nikiitafakari elimu na madini yalikuwepo mule aya Moja tu au mbili unaweza kugusa maeneo kibao na kutoka humo pakapatikana mada na vitabu zaidi ya 200, ufasaha wa Qu'ran haiwi mwanadamu kufikia uwezo wa kutunga vilevile ibada na concepts nzima za uislamu huko mbali na unayoyasema japo hayo madai nimewahi kusoma andiko lakini Qur'an inatosha kuprove wrong madai hayo yote..
 
Isingekuwepo Qu'ran ningekubaliana na mawazo yako ila kila nilisoma Qu'ran moja na nikiitafakari elimu na madini yalikuwepo mule aya Moja tu au mbili unaweza kugusa maeneo kibao na kutoka humo pakapatikana mada na vitabu zaidi ya 200, ufasaha wa Qu'ran haiwi mwanadamu kufikia uwezo wa kutunga vilevile ibada na concepts nzima za uislamu huko mbali na unayoyasema japo hayo madai nimewahi kusoma andiko lakini Qur'an inatosha kuprove wrong madai hayo yote..
Umesoma pia namna Quran ilivyokusanywa baada ya mtume kufariki?
 
Kuhusu ndoa na mahusiano hasa suala la talaka hata wayahudi walihusiwa kuwa na mke mmoja ila kwasababu ya ukaidi wa moyo yao na kuongeza uzao kwa haraka ilibidi hili kiachwe litokee.

Ila baada ya kristo alikuja akakumbushia kuwa ndoa ni mke mmoja ila kwasababu ya ugumu wa mioyo yao ndio mana walikaza fuvu kuwa na wake zaidi ya mmoja

Pia kuhusu talaka Mungu anachukia kitengana..kama hakuna sababu ya msingi ambazo zilianinishwa kama uzizi basi kifo kiwatenganishe..lengo hapa ni kujenga familia imara yenye upendo imani na nguvu.

Talaka inaruhususiwa ila itolewe ikiwa tu unaushahidi wa dhati kuwa mke/mume alizini.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Umesoma pia namna Quran ilivyokusanywa baada ya mtume kufariki?
Nimeisoma tena kitabu kizima chenye pages zaidi ya 500 kikieleza mwanzo mwisho historia ya Qu'ran mpk kukusanywa na mambo mengine kuhusu Qu'ran kama uchambuzi ,aya zilizofutwa hukumu ,jinsi ilivyokusanywa Ktk lahaja na kwa nini iwe hivyo na nyingine kuteketezwa kila kitu nimesoma.

Vipi ulitaka kusemaje ?
 
Isingekuwepo Qu'ran ningekubaliana na mawazo yako ila kila nilisoma Qu'ran moja na nikiitafakari elimu na madini yalikuwepo mule aya Moja tu au mbili unaweza kugusa maeneo kibao na kutoka humo pakapatikana mada na vitabu zaidi ya 200, ufasaha wa Qu'ran haiwi mwanadamu kufikia uwezo wa kutunga vilevile ibada na concepts nzima za uislamu huko mbali na unayoyasema japo hayo madai nimewahi kusoma andiko lakini Qur'an inatosha kuprove wrong madai hayo yote..
Mkuu nakuomba hebu achana nao , hao wote wapo empty hakuna Mwenye IQ yoyote eti ulinganishe Qur-an na bibilia?, narudia hakuna kitabu cha dini kinacho kinachoelezea mwanadamu ninani ila Qur-an, sasa hao wanao mmfanya binaadamu (yesu) kuwa mungu ndio waliopotea hata hao ma royal wao (wayahudi) hawalikubali hili
 
Hoja dhaifu sana hii
Wewe mkuu ndio dhaifu, yesu yeye ni mtu tena ni maskini, tena ana kula na kunya mimi na wewe tena anasikia maumivi iweje awe mungu?, yesu wako alisha ukana uungu mara kibao, au aumini?, kasome


LUKA 18:18
YOHANA 17:3
YOHANA 14:28

Hzo sio hoja za Qur-an lahasha hicho ni katabu chenu kilicho jaa udhaifu , mashaka na magumashi kila page ya kitabu
 
Back
Top Bottom