Uchambuzi wa sakata la muuguzi aliyetaka kutumia vifaa tiba vilivyoisha muda ni aibu

Uchambuzi wa sakata la muuguzi aliyetaka kutumia vifaa tiba vilivyoisha muda ni aibu

Hili tukio lilikuwa limepangwa kama huyu dada lazima tumkomeshe.
Mwananchi wakaida haruhusiwi kuchukua video hospitalini au kwenye taasisi yoyote ya serikali bila idhini ya wahusika. Waliorekodi ni hao hao wafanyakazi.
Kila kazi ina maadili yake ni vyema wafanyakazi wakayamaliza wenyewe ofisini na ikishindikana waende kwenye ngazi husika.
Watu wanajitoa akili kama ilikuwa anania ya kukosoa hakutakiwa kurekodi....kurekodi au kupija picha hospitali ni kosa kubwa sana
 
Watu wanajitoa akili kama ilikuwa anania ya kukosoa hakutakiwa kurekodi....kurekodi au kupija picha hospitali ni kosa kubwa sana
Una uhakika ni yeye karekodi? Je kama ni mgonjwa aliyekuwa kakaa pembeni yao
 
Watu wanajitoa akili kama ilikuwa anania ya kukosoa hakutakiwa kurekodi....kurekodi au kupija picha hospitali ni kosa kubwa sana
Hatutakiwi kufanya kazi kwa kutegemea media. Km mfanyakazi pale wewe tayari ni kiongozi kama unaona kuna huduma inaendeshwa sivyo basi unaenda kuripoti kwa viongozi husika. Ndiyo maana ya kuwa mfanyakazi
Ni muhimu sana kila mfanyakazi ajue maadili ya kazi yake. Unaweza kwenda kutahiriwa unashangaa unakutana na video yako mtandaoni. Unabaki kushangaa
 
hata huyo aliyerekodi iwe ni mafanyakazi au mgomjwa kupija picha au kuchukua video hospitalii ninkosa kubwa
Kosa kwa mujibu wa kujilinda lakini siyo kosa kwa mujibu wa kujiimalisha
 
Hatutakiwi kufanya kazi kwa kutegemea media. Km mfanyakazi pale wewe tayari ni kiongozi kama unaona kuna huduma inaendeshwa sivyo basi unaenda kuripoti kwa viongozi husika. Ndiyo maana ya kuwa mfanyakazi
Ni muhimu sana kila mfanyakazi ajue maadili ya kazi yake. Unaweza kwenda kutahiriwa unashangaa unakutana na video yako mtandaoni. Unabaki kushangaa
Hapo siyo chumba cha upasuaji!
Sehemu ya ofisi kama ofisi zingine!
 
Sakata la wauguzi huko mkoani tabora waliokuwa wakibishana juu ya matumizi ya vifaa vilivyoisha muda wake limeibua maoni mengi sana ya watu!

Wengi wao wameishia kulitazama kwa juu juu na kumuona yule afisa binti mwenye Rafudhi ya KIJITA mix na KIKURYA kwamba ndiye mkosaji na yule mwingine yuko sahihi

Ukitaka kuwaelewa vizuri wahudumu hawa kwanza kabisa fanya kama unaheshimu mawazo ya kila mmoja wao kama ifuatavyo!

A) Anaepinga vifaa vilivyoisha visitumike!
Mawazo ya afisa huyu yapo sahihi lakini sehemu pasipo sahihi! Naposema usahihi wake ni sahihi pasipo sahihi namaanisha aliyemwambia (Binti) Je, alikuwa mtu sahihi kufanya maamuzi yoyote ya kubadilisha? Je kulikuwa na mbadala?, Je taarifa za ukomo wa matumizi mganga mkuu wa hospital alikuwa nazo? Je Shifting ya Jana yake siku hiyo walitumia nini? Kwanini havikuondolewa kama vimeisha muda wake? Ukitafta majibu ya hayo unaona kabisa yule afisa alikuwa sahihi lakini pasipo sahihi!

B) Afisa aliyetaka vitumike!

Huyu ukimtafakali kwa juu juu huwezi kuona jambo lakini kuna jambo, ukichimba unaona naye anajambo, unaona kabisa huyu kwa maoni yake hakukuwa na mbadala hivyo yupo sahihi! Au amechoka kusubili,

Huyu afisa anaishi kwenye falsafa ya Funika kombe mwanaharamu Apite!

Falsafa hii ndiyo falsafa ya serikali isiyojali maisha ya watu!

Yamkini huyu binti anataarifa zote za ukosefu wa vifaa tiba, na yamkini hakuna jitihada za kupata Leo au kesho!

Pia huwezi kuacha kujiuliza maswali haya! Kama vifaa tiba vipya vipo kwanini asingetoa vipya? Kwanini vilivyoisha vilibakia kuwepo hospitali hapo? Je anamkomoa nani? Na anamlinda nani?

Ukitafakali kwa kina sakata hili utagundua wote wapo sahihi lakini tofauti ni kwamba!
1. Aliyekataa anatetea taaluma yake.
2. Yule binti anayeruhusu anatetea Tumbo lake!

Na Mara nyingi serikali ya kimasikini imezungukwa na watu wanaotetea matumbo kuliko wanaoetetea taaluma zao!

Mifumo ya ugavi na manunuzi vifaa tiba katika hospital na ofisi za umma imejaa milolongo mireefu ambayo ni kero kwa maafisa! (Wanachoka bora liende)

Hivyo Dawa ya hawa watumishi ni kuwahamisha ili wasije tegeneza bomu la kuhatarisha maisha yao na ya wagonjwa!

Mkosaji mkubwa katika sakata hilo nimsambazaji wa vifaa tiba, ni mganga mkuu ambaye hakuviondoa vifaa vilivyoisha muda wake hospitalini, ni serikali yenye wajibu wakupeleka vifaa tiba kwa wakati!

Sakata hilo ni kipande kidogo sana cha Uozo mwingi uliopo mahospitali karibu yote Tanzania!

Huyo binti ni kielelezo cha wahudumu walio wengi Tanzania ambao wanaijua serikali hivyo wameamua kwenda nayo kama ilivyo!

Yule kijana akiadhibiwa itavunja moyo, na yule binti akiadhibiwa napo itafedhehesha Mioyo!

Nina uhakika 100% Report ya waziri itaishia kukanusha kwamba hakukuwa na vifaa tiba vilivyoisha na wale wahudumu watahamishwa kwa migogoro binafsi!

Tunaoumia ni SISI!

Updates
Wahudumu wote waliokuwa wanabishana kuhusu matumiz ya vifaa vibovu wamesimamishwa kazi!

Hapo ndipo utaelewa huyo wa kiume kosa lake ni lipi!

Ukitaka kulielewa hilo kosa rudia kusoma Uzi huu hapo juu!
Mimi sioni umuhimu wowote wa mlolongo wa maelezo yako. Unajaribu kueleza nini?
 
Halafu hawa wana ugomvi wa muda mrefu huyu dada asionewe.Hata hivyo alimwambia akamwambie incharge ambaye ni boss wa dada, so jamaa alitakiwa kwenda huko.


Lakini kuwa na mtumishi wa afya wa aina hii anayerekodi mambo hospital ni hatari hatariiii sanaaa.Huyu anaweza mrekodi TUPU mgonjwa anayem-attend.

Sheria za kazi naye zimhusu
 
Yule dada nimemsilikiliza good sana alimwambia kama kijana yule ‘’kama hutaki kutumia nenda kwa incharge umwambie na sio mimi’’

Sema yule kijana alikuwa anatafuta humaarufu na akijiona yeye atakuwa salama kwa kufanya hivyo
 
Pita hivi bhasi! Hahahah
Siwezi kupita hivi nionapo mtu anaweka bla bla nyingi zisizo na maana yoyote. Thread inayojadili kuhusu hili ipo hapa. Wewe unakwenda kuanzisha thread isiyo na ulazima wowote na maelezo yenyewe yanajichanganya changanya huku ukidhani umeandika mambo ya maana kweli kweli.
 
Kosa la Wakubwa hapo... Hao wadogo watanyonyolewa tu... [emoji23][emoji23]
Na kama si kurekodi tusingeyajua hayo... Hao wote hawana makosa.
 
Kosa la Wakubwa hapo... Hao wadogo watanyonyolewa tu... [emoji23][emoji23]
Na kama si kurekodi tusingeyajua hayo... Hao wote hawana makosa.
Yapo sana tu hayo mambo!
Hata watu wanaokufa na kuzinduka huko mochwari unazani hawapo? Sema bhasi tu kulindana
 
Hapo kijana anajilaumu sana
Na waziri tayali kashakanusha huko kwamba hakuna kipimo kilichoisha muda wake Tanzania nzima hakipo!
Screenshot_20230107-123927.png
 
Acha watu waibue maovu, tumechoka kupoteza ndugu na jamaa zetu huko ma hospitalini.

Au nawee n muhusika wa, matukio km hayo?
Mimi sio muhusika lakn yule dada kosa lake n lipi wakati yeye sio incharge
Anyway tusubiri tuone yup atakaye rud kazin🤔🤚
 
Kosa la Wakubwa hapo... Hao wadogo watanyonyolewa tu... [emoji23][emoji23]
Na kama si kurekodi tusingeyajua hayo... Hao wote hawana makosa.
Kabla hata uchunguzi haujakamilika waziri kashakanusha KWAMBA HAKUNA KIPIMO KILICHOISHA MUDA WAKE INCHI NZIMA!
 
Back
Top Bottom