1. Wanaoshuhudia madhila na utapeli ni walioukuwa watumishi na wanafunzi wa TB Joshua mwenyewe na kanisa lake, sio watu baki. Mmojwapo ni watu waliokuwa karibu kabisa naye kama mtu namba mbili baada TB Joshua.
2. Kwenye baadhi ya sehemu za clips zilizorekodiwa na kanisa hilo na ambazo ni public zilizotumiwa na BBC TB Joshua anaonyeshwa akifanya mambo ya ajabu mbele ya hadhara kama kupiga watu makofi kama sehemu ya huduma!
3. TB Joshua alikuwa akiishi kwenye jumba mfano wa gereza na kundi kubwa la wanaoitwa "disciples" wanafunzi wake, wengi wakiwa wanawake vijana na vigori, walivyokuwa wanapatikana anajua yeye mwenyewe ila mmoja wa wahojiwa anasema alipewa na kazi na TB Joshua ya kuleta wanafunzi wa kike mabikira. Watu kuzuiliwa kama wako kifungoni na viongozi wa cults sio jambo jipya, mifano ni mingi sana kuanzia kwa jirani zetu hapa Kenya katika kisa cha Shakahola, huko kwingine duniani wamewahi kuwepo kina Jim Jones wa people's temple, David Koresh wa Waco n.k
4. Hakuna mgogoro wowote ndani ya kanisa la SCOAN unaohusishwa na waathirika hawa walioamua kusema yaliyokiwa yanatendeka nyuma ya pazia, hivyo huwezi kusema hata ni watu wenye nia ovu ya kulimega hilo kanisa na kuanzisha lao.
5.BBC wanasema waandishi wao walirushiwa risasi na walinzi wa kanisa hilo walipokuwa wanachukua video. Kanisa lolote linaloweza kufikia kiwango hichi cha kujificha kutoka waandishi wa habari ni taa nyekundu.
6.Ni kweli jengo la kanisa la TB Joshua liliwahi kuanguka na kuua mamia ya watu kwa sababu ya kutofuata taratibu sahihi za ujenzi na TB Joshua akasema kulikuwa na ndege ndogo iliyokuwa ikizunguka katika jengo hilo iliyopelekea kuporomoka na kwamba pia lilikuwa na jaribio la mauaji dhidi yake. Hata hivyo Ushahidi wa wazi ni kwamba taratibu nyingi za ujenzi wa jengo hilo zilikiukwa lakini kwa sababu matapeli wa kidini kama yeye wamekuwa na nguvu na ushawishi mkubwa sana katika serikali za Africa hakuna hatua yoyote aliyochukuliwa.
7. BBC wamefanya uandishi wa kiuchunguzi "investigative journalism" sio utafiti "research" au forensic investigation ambayo sasa inapaswa kufanywa na polisi kuthibitisha zaidi yaliyoletewa hadharani na BBC. Yani kazi kubwa iliyofanywa na BBC ni kuwasikiliza waathirika takribani 30 kutoka sehemu mbalimbali, kuhakikisha hawajapanga "conspire" kusema walichosema, kufanya kuoanjsha wanachosema"corroboration" na kisha kuwapa fursa kanisa la SCOAN la TB Joshua kuzungumzia tuhuma hizo ambapo walikataa kuwapa ushirikiano wowote.
Kazi ya ushahidi mwingine unaodaiwa na baadhi ya member hapa jukwaani kama ushahidi wa video wa watu wakibakwa ni suala la forensic investigation na mahakamani kama polisi wa Nigeria wataamua kufuatilia kesi hiyo. BBC wamefanya kazi yao uandishi wa kiuchunguzi kwa weledi mkubwa na wamemaliza.