Uchunguzi: TB Joshua aliwanyanyasa na kuwabaka wafuasi wake
Walalamikaji wanatoka Uingereza, Ujerumani, Nigeria, Ghana na nchi nyingine.
Baadhi ya hao Waingereza waliripoti hayo matukio katika ubalozi wao baada ya kutoroka katika makao ya TB Joshua walipokuwa wanafungiwa/wanafugwa.
Kwanini ubalozi haukumchukilia hatua kama mashitaka yao yalikuwa credible?
 
Upuuzi mtupu. Hakuna uchunguzi wowote wala kitu cha maana, ni siasa tu za umiliki wa mali za kanisa kati ya Mke wa TB Joshua na Baraza la Wazamini wa Kanisa kwani mama aliwashinda waliokuwa wanategemea kujichotea manoti ya kanisa baada ya jamaa kufa. Sasa wanapambana kuona namna gani wataliyumbisha kanisa mbele ya jamii.

Hapa hakuna uchunguzi wa maana na huo uchunguzi ni aibu kwa BBC. Uchunguzi ungetakiwa usiwe wa maneno tu bali uwe na ushahidi tosha kama:

1. Taarifa za kidaktati zinazoonesha namna hao waathirika waliathiriwa na Nabii.

2. Case zilizofunguliwa Mahakamani na mashtaka yaliyopelekwa polisi.

3. Namna Balozi za UK,NAMIBIA na nchi nyingine zilipokea malalamiko na kurespond kuhusu malalamiko ya waathiriwa.

4. Picha na vielelezo toka kwa waathirika.

Simtetei TB Joshua kwani naye ni Bunadamu na alikuwa na mapungufu ila hiki walicholeta BBC ni blah blah na hadithi tu, kwanini wasingechunguza na kuja na hizo blah blah muhusika akiwa hai?

Blah blah hizi zinahusu mtu aliyekufa direct asiyejitetea na hazihusu taasisi. Wajunga wasiojitambua wala wenye uwezo wa kufikiria kizazi cha 1990's to 2000's ndio mtashadadia ila kwa mtu mwenye utulivu wa kiakili, hakuna kitu cha maana hapa.
✅🙏🙏🙏
 
Nimeziona hizo documentaries,
Lakini hakuna mahala ambapo ubalozi wa Uingereza ulialifiwa lakini ukashindwa kumchukulia hatua yungali hai!
Nipe ushahidi wa hilo, msilazishe mambo tu!
Mkuu,

Watu wamezuzuliwa wamekuwa brainwashed, wametishwa, wamekuwa totally broken inside a cult, wameshindwa kuwa huru mpaka TB Joshua kafa ulitaka waripoti ubalozi kivipi?

Watu wamedanganywa hata pasi zao wameshindwa kukaa nazo, unategemea wakaseme ubalozini? Unajua mentality ya cults inavyokuwa? Hawa watu huwa wanaambiwa wajiue kama na Kibwetere Uganda, Mackenzie Kenya au Jim Jones, David Koresh na Heavens Gates USA, na wanajiua, wewe unashangaa hawajaenda kushitaki ubalozini?

TB Joshua alikuwa anaongoza cult.

Unaelewa haya mambo yanavyokuwa au unafikiri wale watu wanakuwa na akili sawa na watu wazima?

Kubakwa na abuse huwa haiwi iama unavyotaka iwe. Watu wengi wanaobakwa nankuwa abused, hususan vijana wadogo, huwa wana self hate. Ma Joshua alikuwa na narrative kanisani mwake, watu wakija wakisema wamekuwa raped, yeye alikuwa anawalaumu waliokuwa raped kwamba wao ndio walikuwa na makosa ya kushawishi watu wawabake, kwa kuvaa vibaya, kuwa temptress and Jezebels. Sasa hapo wanandeal nanpowerful figure ambaye hata mtoto wake mwenyewe kamkataa na mtoto kashindwa kusema ukweli kwa kujua hataaminiwa, unafikiri ni kitu rais kumsemea?

Watu huwa hawabakwi na kukimbia kusema polisi kama wameibiwa, kuna saikolojia nzito sana ambayo ni vigumu sana kuielewa.
 
Mtu mzima miaka 12 unafanyiwa ukatili na umetulia tu.
Unaenda sokoni unarudi ndani kufanyiwa ukatili.
Unaenda kanisani unarudi kufanyiwa ukatili.
Unaenda mjini unapita vituo vya polisi kibao unarudi ndani kufanyiwa ukatili.

Huu sio ukatili ni makubaliano.

Hapa mtu anataka Urithi wa Mali tu.
 
Kweli dunia ina mazezeta mengi no wonder hawa manabii feki wanaendelea ku exist, btw sidhani kama umezitazama documentrary zote tatu ama yawezekana ulizitazama tayari ukiwa na majibu yako kichwani. Kondoo mtaendelea kuliwa supu hadi akili ziwakae sawa
Wacha weeeeee
 
Umetazama hizo episodes zote tatu za BBC?
Wewe nilishakupuuziaga. Huna ujualo humu duniani. Hilo bichwa limejaa makamasi. Kuargue na wewe ni kupoteza muda na ni bora niargue na mwanangu manka.
 
Mtu mzima miaka 12 unafanyiwa ukatili na umetulia tu.
Unaenda sokoni unarudi ndani kufanyiwa ukatili.
Unaenda kanisani unarudi kufanyiwa ukatili.
Unaenda mjini unapita vituo vya polisi kibao unarudi ndani kufanyiwa ukatili.

Huu sio ukatili ni makubaliano.

Hapa mtu anataka Urithi wa Mali tu.
Kuna mtu kasema hapo juu eti hii sio uchunguzi, ni ubuyu wa Dada yetu Nifah . Hapa watalishika puuzi Kiranga tu ila mtu mwenye akili timamu hawezi ukubali huu ushuzi.
 
Wewe nilishakupuuziaga. Huna ujualo humu duniani. Hilo bichwa limejaa makamasi. Kuargue na wewe ni kupoteza muda na ni bora niargue na mwanangu manka.
1. Hujajibu swali nililouliza.

2. Hujanipuuza, ndiyo maana umenisoma na kunijibu.

3. Nakufundisha jinsi ya kumpuuza mtu. Nakupeleka ignore list, kuanzia hapa sitaona utakachoandika. Hivi ndivyo unavyotakiwa kumpuuza mtu.
 
Kisheria ukiishi na mtu mzima wa jinsia tofauti miaka mitatu ndani ya nyumba moja, mnapika mnapakua, mnakula na kunywa na kulala pamoja.

Nyie mtakuwa Wanandoa halari kabisa.
Sembuse miaka 12.
Ila Urithi wameukosa, hawakuandikishana popote.
 
Kuna mtu kasema hapo juu eti hii sio uchunguzi, ni ubuyu wa Dada yetu Nifah . Hapa watalishika puuzi Kiranga tu ila mtu mwenye akili timamu hawezi ukubali huu ushuzi.
Aliyekuambia ubuyu wangu hauna uchunguzi nani?
Hivi mnafikiri naandika tu blah blah?
Mngejua!
 
Kitengo Cha uchungu Cha BBC eye kimeendelea kufichua uovu wa yule Nabii tapeli wa watu wavivi TB Joshua.

Inadaiwa kwamba bwana TB Joshua alidanganya mamlaka na kulipa pesa Ili ionekane Helikopta iligonga jengo l Kanisa lake na kisha kusababisha vifo vya watu 116.

Hata hivyo Uchunguzi wa BBC eye umeonesha kwamba jengo Hilo kiliporomoka kutokana na ujenzi duni na kuongeza Gorofa (floors) nyingi zaidi kuliko uwezo wake ,amri ambayo ilitolewa na TB Joshua licha ya kuonywa na mamlaka na wasimamizi wa Ujenzi.

On top of that Idadi kubwa ya Watu ilikufa tofauti na walioripotiwa ambapo miili ya watu ilisafirishwa usiku usiku Ili kukwepa vyombo vya habari na mamlaka huku hayo yakifanyika chini ya maelekezo ya TB Joshua na Ulinzi wa maofisa wake.

Taarifa hizi zinakuja kufuatia kufichuliwa Kwa habari za ubakaji na mateso ambayo bwana Joshua alikuwa akiwafanyia waumini wake.

 
Kwanini ubalozi haukumchukilia hatua kama mashitaka yao yalikuwa credible?
Ubalozi hauwezi kumchukulia hatua mtu katika nchi nyingine hasa akiwa sio raia wao na katika mambo tata kama hayo yanoyohusu cults. Kuchukuliwa hatua ni kazi ya polisi na mamlaka za Nigeria, TB Joshua alikuwa ameiweka serikali ya Nigeria mfukoni kwake ndio maana hata jengo lake lilipoanguka na kuua mamia ya raia hakuchukuliwa hatua yoyote japo taarifa ya wazi kabisa ilionyesha kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu za ujenzi.
 
Mtu mzima miaka 12 unafanyiwa ukatili na umetulia tu.
Unaenda sokoni unarudi ndani kufanyiwa ukatili.
Unaenda kanisani unarudi kufanyiwa ukatili.
Unaenda mjini unapita vituo vya polisi kibao unarudi ndani kufanyiwa ukatili.

Huu sio ukatili ni makubaliano.

Hapa mtu anataka Urithi wa Mali tu.
Waulize wafanyakazi wa ndani wanaofanyiwa hivyo uarabuni kama huwa inakuwa ni makubaliano. Human trafficking, na ubakaji uliochanganyika kwenye cults sio jambo rahisi kwa waathirika kutoka kama unavyofikiri.

Wafanyakazi wa bongo tu hapa wengi wanafanyiwa mambo ya ajabu na hawaendi popote wanakuwa kama kuku waliofungwa kamba mguuni.
 
Walalamikaji wanatoka Uingereza, Ujerumani, Nigeria, Ghana na nchi nyingine.
Baadhi ya hao Waingereza waliripoti hayo matukio katika ubalozi wao baada ya kutoroka katika makao ya TB Joshua walipokuwa wanafungiwa/wanafugwa.
Baada ya kutipoti kwenye ubalozi wao , ubalozi wao ulichukua hatua gani? Ubalozi wa Uingereza nchini Nigeria ungeweza kuibua kama kulikuwa na uhalifu dhidi ya raia wake at a diplomatic level na hatua stahiki kuchukuliwa.
Waliripoti kabla au baada ya kufa T.B .Joshua?
Nia ya BBC kutangaza malalamiko haya wakati muhusika mkuu amefariki ni nini?
 
Kama mna nguvu mkabomoe makanisa yao na kuwafungia, pilipili usiyoila inakuwashia nini? Kama dini yako iko safi hao ambao unaona hawako safi waombwe. Hizo clip za Tb Joshua mbona hazina kitu cha ajabu ni yale yale tunayoyaona kwenye ibada zake zinazokuwa live, hao wanaosema walibakwa na kupigwa makofi na kufungwa minyororo tunawaaminije kama ni kweli? Pia ikumbukwe wengine walikuwa wanapelekwa pale wakiwa vichaa kwa usalama inabidi wafungwe kamba ili wasilete madhara kwa watu, wazungu wameshazoea kuwakandamiza watu weusi hasa wenye mali, mtu anakaa akiona maisha yamepiga ana miaka 50 anafungua kesi kuwa nilibakwa nikiwa na miaka 17 ili alipwe pesa, wao BBC wanajuaje miujiza fake na miujiza ya kweli? Ni shirika la kiroho? Miujiza fakes halafu uaminiwe na watu toka Africa, American, Ulaya, Asia
 
Back
Top Bottom