Uchunguzi: TB Joshua aliwanyanyasa na kuwabaka wafuasi wake
Walishindwa nini kumchunguza kipindi cha uhai wake. Kanisa lilianguka akiwa hai. Leo hii hata kama ni kweli inasaidia nini?

Tatizo linakuja kuwa wanadamu tumewekeza imani kubwa sana kwa Mungu kupitia wanadamu wenzetu. Imekuwa mtu hajiamini kumuomba Mungu moja kwa moja mpaka apitie kwa nabii na mitume, hili linafanya hao manabii wajihisi kuwa na wewe ni miungu pia.

Ifikie wakati watu kwa imani zao wenyewe wavunje hizi cult za manabii na mitume na wajikumbushe na kutambua kuwa Mungu anasikia maombi bila kuhitaji madalali.
ndugu yangu malalamiko dhidi ya TB Joshua yapo kwenye YouTube siku nyingi . watu wengi wanasema eti walikuwa wapi wakati akiwa hai, ukweli ni kwamba tuhuma zipo You Tube kabla hajafa. na wanawake wanaolalamika sio kwamba walijificha, walionyesha sura zao na kujitaja majina. watu waseme lingine lakini sio hilo la kwamba eti amekufa ndo wanaibuka ! alichofanya BBC ni kufuata kanuni za uandishi wa habari kwa kufanya uchunguzi kisha kutoa majina ya watu, tarehe, na mahali n.k. ila tuhuma zipo siku nyingi
 
😂😂😂
Nacheka
Huyu mtu alijitahidi na aka file docs za ushahidi tbj akiwa hai akachemka!

Ametafuta Tena namna nyingine ya kurudi!
This time atashindwa vby zaidi ya mwanzo
Sijui hata wanapaparika Nini,waache wahangaike ila sisi tunahitaji ushahidi wa vitendo sio maneno eti walikuwa wanachapwa, mwingine eti TB kamtoa mimba Tano🙄🙄🙄Sasa wewe Hadi unaingizwa mimba Tano umekaa tu una akili au matope
 
Ushahidi wa unyanyasaji ulionea na mateso kutoka kwa mwanzilishi wa mojawapo ya makanisa makubwa ya kiinjili ya Kikristo duniani umefichuliwa na BBC.

Makumi ya waumini wa zamani wa Kanisa la Synagogue Church of all Nations - watano Waingereza - wanadai ukatili, ikiwa ni pamoja na ubakaji na utoaji mimba kwa lazima, uliofanywa na marehemu TB Joshua wa Nigeria.

Madai ya unyanyasaji katika eneo la siri la Lagos yamedumu kwa takriban miaka 20.

Kanisa la Synagogue Church of All Nations halikujibu madai hayo lakini lilisema madai ya hapo awali hayana msingi.

TB Joshua, aliyefariki mwaka wa 2021, alikuwa mhubiri na mwinjilisti mwenye mvuto mkubwa na mwenye mafanikio makubwa ambaye alikuwa na wafuasi wengi duniani.

Matokeo ya BBC katika uchunguzi wa miaka miwili ni pamoja na:
  • Masimulizi mengi ya watu waliojionea matukio ya ukatili wa kimwili au mateso yaliyofanywa na Joshua, ikiwa ni pamoja na matukio ya unyanyasaji wa watoto na watu kuchapwa viboko na kufungwa minyororo.
  • Wanawake wengi wanaosema walinajisiwa na Joshua, huku baadhi wakidai kuwa walibakwa mara kwa mara kwa miaka mingi ndani ya boma hilo.
  • Tuhuma nyingi za kutoa mimba kwa lazima ndani ya kanisa kufuatia tuhuma za ubakaji na Joshua, akiwemo mwanamke mmoja ambaye anasema alitolewa mimba mara tano.
  • Simulizi nyingi za moja kwa moja zinazoelezea jinsi Joshua alivyodanganya kuhusu "uponyaji wake wa miujiza", ambao ulitangazwa kwa mamilioni ya watu ulimwenguni kote.
Mmoja wa waathiriwa, mwanamke wa Uingereza, anayeitwa Rae, alikuwa na umri wa miaka 21 alipoacha shahada yake katika Chuo Kikuu cha Brighton mnamo 2002 na kuandikishwa katika kanisa. Alitumia miaka 12 iliyofuata kama mmoja wa wale wanaoitwa "wanafunzi" wa Yoshua ndani ya boma lake la kifahari huko Lagos.

"Sote tulidhani tuko mbinguni, lakini tulikuwa katika hali inayofanana na ya kuzimu, na huko kunatokea mambo mabaya," aliiambia BBC.

Rae anasema alinajisiwa na Joshua na kuwekewa aina ya kifungo cha upweke kwa miaka miwili. Dhuluma hiyo ilikuwa kali sana, anasema alijaribu kujiua mara nyingi ndani ya boma hilo.

Kanisa la Synagogue Church of All Nations [Scoan] lina wafuasi wa kimataifa, wanaoendesha chaneli ya TV ya Kikristo iitwayo Emmanuel TV na mitandao ya kijamii yenye mamilioni ya watazamaji. Katika miaka yote ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000, makumi ya maelfu ya mahujaji kutoka Ulaya, Amerika, Kusini Mashariki mwa Asia na Afrika walisafiri hadi kanisani humo nchini Nigeria kumshuhudia Joshua akifanya "miujiza ya uponyaji".

Takriban wageni 150 waliishi naye kama wanafunzi ndani ya boma lake huko Lagos, wakati mwingine kwa miongo kadhaa.

Rae in a BBC studio interview, wearing glasses and black top

Maelezo ya picha: Rae alisalia kwa miaka 12 katika boma la Joshua

Zaidi ya "wanafunzi" 25 wa zamani walizungumza na BBC - kutoka Uingereza, Nigeria, Marekani, Afrika Kusini, Ghana, Namibia na Ujerumani - wakitoa ushuhuda wenye nguvu wa kuthibitisha waliopitia ndani ya kanisa, pamoja na matukio ya hivi majuzi zaidi katika mwaka wa 2019. Waathiriwa wengi walikuwa katika ujana wao walipojiunga mara ya kwanza. Katika baadhi ya kesi za Uingereza, usafiri wao hadi Lagos ulilipwa na Joshua, kwa ushirikiano na makanisa mengine ya Uingereza.

Rae na waliohojiwa wengine wengi walilinganisha masaibu yao na kuwa katika dhehebu la itikadi kali .
Jessica Kaimu, kutoka Namibia, anasema masaibu yake yalidumu kwa zaidi ya miaka mitano. Anasema alikuwa na umri wa miaka 17 wakati Joshua alipombaka kwa mara ya kwanza, na kwamba matukio ya baadaye ya kubakwa na TB Joshua yalisababisha atoe mimba mara tano akiwa huko.

"Haya yalifanyika kisiri... matibabu tuliyokuwa tukifanyiwa... yangeweza kutuua," aliiambia BBC.
Wengine waliohojiwa wanasema walivuliwa nguo na kupigwa kwa nyaya za umeme na mijeledi ya farasi, na mara kwa mara walikoseshwa usingizi.
Katika kifo chake mnamo Juni 2021, TB Joshua alisifiwa kama mmoja wa wachungaji wenye ushawishi mkubwa katika historia ya Afrika.

Akiinuka kutoka kwa umaskini, alijenga himaya ya kiinjilisti ambayo ilijivunia makumi ya viongozi wa kisiasa, watu mashuhuri na wanasoka wa kimataifa kati ya washirika wake.

Hata hivyo, alizua utata wakati wa uhai wake wakati nyumba ya wageni ya mahujaji wa kanisa ilipoporomoka mwaka wa 2014, na kuua watu wasiopungua 116.Uchunguzi wa BBC, ambao ulifanywa na jukwaa la kimataifa la vyombo vya habari vya Open Democracy, ni mara ya kwanza watu wengi wa zamani wa makanisa kujitokeza kuzungumza juu ya rekodi hiyo. Wanasema wametumia miaka mingi kujaribu kupaza sauti lakini wamenyamazishwa kwa ufanisi.

Baadhi ya mashahidi wetu nchini Nigeria wanadai walishambuliwa kimwili, na katika kisa kimoja walipigwa risasi, baada ya awali kujitokeza kupinga unyanyasaji huo na kuchapisha video zenye madai kwenye YouTube.

Wafanyakazi wa BBC ambao walijaribu kurekodi picha za boma la kanisa hilo Lagos kutoka mtaa wa umma mnamo Machi 2022 pia walipigwa risasi na usalama wa kanisa hilo, na walizuiliwa kwa saa kadhaa.

BBC iliwasiliana na Scoan na madai hayo katika uchunguzi wetu. Haikuwajibu, lakini ilikanusha madai ya awali dhidi ya TB Joshua.
"Kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Nabii TB Joshua si jambo geni... Hakuna madai yoyote yaliyowahi kuthibitishwa," iliandika.

Raia wanne wa Uingereza waliozungumza na BBC wanasema waliripoti unyanyasaji huo kwa mamlaka ya Uingereza baada ya kutoroka kanisani. Wanasema hakuna hatua zaidi zilizochukuliwa.

Anneka pictured in BBC studio interview, wearing white jumper

Maelezo ya picha: Anneka anasema anaamini kuna waathiriwa wengi ambao bado hawajazungumza

Zaidi ya hayo, mwanamume Muingereza na mkewe walituma barua pepe kwa mashahidi waliojionea ushahidi wao wa mateso na video - ikiwa ni pamoja na rekodi za kushikiliwa kwa mtutu wa bunduki na wanaume wanaojiita polisi ambao pia ni wanachama wa Scoan - kwa Ubalozi wa Uingereza nchini Nigeria mnamo Machi 2010 baada ya kukimbia kanisa hilo. Katika barua pepe yake, mwanamume huyo alisema mke wake alishambuliwa kingono mara kwa mara na Joshua. Aliionya ubalozi huo kuwa raia wengine wa Uingereza bado wako ndani ya boma hilo wakikabiliwa na ukatili.

Pia anasema hakuna hatua zilizochukuliwa. Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza haikujibu madai haya, lakini iliambia BBC kwamba inachukulia ripoti zote za uhalifu, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya raia wa Uingereza nje ya nchi, kwa uzito mkubwa.

Scoan inaendelea kustawi leo, chini ya uongozi wa mjane wa Joshua, Evelyn. Mnamo Julai 2023, aliongoza ziara ya kwenda Uhispania.

Anneka, ambaye aliondoka Derby nchini Uingereza na kujiunga na Scoan akiwa na umri wa miaka 17, aliambia BBC kuwa anaamini kuna waathiriwa wengine wengi ambao bado hawajazungumza. Anatumai hatua zaidi zitachukuliwa kufichua vitendo vya Joshua.

"Ninaamini Kanisa la Synagogue Church of All Nations linahitaji uchunguzi wa kina ili kujua ni kwa nini mtu huyu aliweza kufanya kazi kwa muda mrefu kama alivyofanya," alisema.

Ripoti ya ziada ya Maggie Andresen, Yemisi Adegoke na Ines Ward
Kwa usaidizi na taarifa kuhusu unyanyasaji wa kingono, tafadhali wasiliana na Mtandao huu wa BBC Actionline nchini Uingereza. Na kwa habari zaidi juu ya madhehebu, tafadhali tazama The Family Survival Trust

BBC
Pia soma: BBC imepanga kutoa video inayoonesha Unabii Feki wa TB Joshua
ok sawa,lakini kwanini wasubiri amekufa ndo waanze kumshambulia namna hii!!!??
 
Sijui hata wanapaparika Nini,waache wahangaike ila sisi tunahitaji ushahidi wa vitendo sio maneno eti walikuwa wanachapwa, mwingine eti TB kamtoa mimba Tano🙄🙄🙄Sasa wewe Hadi unaingizwa mimba Tano umekaa tu una akili au matope
Ndo ushangae eti mimba zote hizo nawe upo tu!
huyu dada aliposhindwa 1st time alienda mpk kuomba msamaha Kwa tbj akiwa hai 😂
Ndo maana tunawashangaa wanaoshadadia wasichokijua.
Acha tu
 
hiv inaqezekana vip mtu kubakwa mara 5 mbona story za kufukirika hizi
Ndugu unaonekana mgeni kwenye mambo ya makanisa..kaangalie documentary Ya WACO ya kanisa la marekani miaka ya nyuma..namna watu wanatumia dini kufanya ujinga na kugeuza watu mazuzu..
 
Hongera BBC kwa kuangazia utapeli.

Ila nitawapa heko zaidi mkija na report ya uchunguzi wa wizi na ufisadi wa CCM.
 
Ndo ushangae eti mimba zote hizo nawe upo tu!
huyu dada aliposhindwa 1st time alienda mpk kuomba msamaha Kwa tbj akiwa hai 😂
Ndo maana tunawashangaa wanaoshadadia wasichokijua.
Acha tu
Shetani ana anapambana kuchafua ukristo...ila Moto wa Kristo ni balaa
 
Ushahidi wa unyanyasaji ulionea na mateso kutoka kwa mwanzilishi wa mojawapo ya makanisa makubwa ya kiinjili ya Kikristo duniani umefichuliwa na BBC.

Makumi ya waumini wa zamani wa Kanisa la Synagogue Church of all Nations - watano Waingereza - wanadai ukatili, ikiwa ni pamoja na ubakaji na utoaji mimba kwa lazima, uliofanywa na marehemu TB Joshua wa Nigeria.

Madai ya unyanyasaji katika eneo la siri la Lagos yamedumu kwa takriban miaka 20.

Kanisa la Synagogue Church of All Nations halikujibu madai hayo lakini lilisema madai ya hapo awali hayana msingi.

TB Joshua, aliyefariki mwaka wa 2021, alikuwa mhubiri na mwinjilisti mwenye mvuto mkubwa na mwenye mafanikio makubwa ambaye alikuwa na wafuasi wengi duniani.

Matokeo ya BBC katika uchunguzi wa miaka miwili ni pamoja na:
  • Masimulizi mengi ya watu waliojionea matukio ya ukatili wa kimwili au mateso yaliyofanywa na Joshua, ikiwa ni pamoja na matukio ya unyanyasaji wa watoto na watu kuchapwa viboko na kufungwa minyororo.
  • Wanawake wengi wanaosema walinajisiwa na Joshua, huku baadhi wakidai kuwa walibakwa mara kwa mara kwa miaka mingi ndani ya boma hilo.
  • Tuhuma nyingi za kutoa mimba kwa lazima ndani ya kanisa kufuatia tuhuma za ubakaji na Joshua, akiwemo mwanamke mmoja ambaye anasema alitolewa mimba mara tano.
  • Simulizi nyingi za moja kwa moja zinazoelezea jinsi Joshua alivyodanganya kuhusu "uponyaji wake wa miujiza", ambao ulitangazwa kwa mamilioni ya watu ulimwenguni kote.
Mmoja wa waathiriwa, mwanamke wa Uingereza, anayeitwa Rae, alikuwa na umri wa miaka 21 alipoacha shahada yake katika Chuo Kikuu cha Brighton mnamo 2002 na kuandikishwa katika kanisa. Alitumia miaka 12 iliyofuata kama mmoja wa wale wanaoitwa "wanafunzi" wa Yoshua ndani ya boma lake la kifahari huko Lagos.

"Sote tulidhani tuko mbinguni, lakini tulikuwa katika hali inayofanana na ya kuzimu, na huko kunatokea mambo mabaya," aliiambia BBC.

Rae anasema alinajisiwa na Joshua na kuwekewa aina ya kifungo cha upweke kwa miaka miwili. Dhuluma hiyo ilikuwa kali sana, anasema alijaribu kujiua mara nyingi ndani ya boma hilo.

Kanisa la Synagogue Church of All Nations [Scoan] lina wafuasi wa kimataifa, wanaoendesha chaneli ya TV ya Kikristo iitwayo Emmanuel TV na mitandao ya kijamii yenye mamilioni ya watazamaji. Katika miaka yote ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000, makumi ya maelfu ya mahujaji kutoka Ulaya, Amerika, Kusini Mashariki mwa Asia na Afrika walisafiri hadi kanisani humo nchini Nigeria kumshuhudia Joshua akifanya "miujiza ya uponyaji".

Takriban wageni 150 waliishi naye kama wanafunzi ndani ya boma lake huko Lagos, wakati mwingine kwa miongo kadhaa.

Rae in a BBC studio interview, wearing glasses and black top

Maelezo ya picha: Rae alisalia kwa miaka 12 katika boma la Joshua

Zaidi ya "wanafunzi" 25 wa zamani walizungumza na BBC - kutoka Uingereza, Nigeria, Marekani, Afrika Kusini, Ghana, Namibia na Ujerumani - wakitoa ushuhuda wenye nguvu wa kuthibitisha waliopitia ndani ya kanisa, pamoja na matukio ya hivi majuzi zaidi katika mwaka wa 2019. Waathiriwa wengi walikuwa katika ujana wao walipojiunga mara ya kwanza. Katika baadhi ya kesi za Uingereza, usafiri wao hadi Lagos ulilipwa na Joshua, kwa ushirikiano na makanisa mengine ya Uingereza.

Rae na waliohojiwa wengine wengi walilinganisha masaibu yao na kuwa katika dhehebu la itikadi kali .
Jessica Kaimu, kutoka Namibia, anasema masaibu yake yalidumu kwa zaidi ya miaka mitano. Anasema alikuwa na umri wa miaka 17 wakati Joshua alipombaka kwa mara ya kwanza, na kwamba matukio ya baadaye ya kubakwa na TB Joshua yalisababisha atoe mimba mara tano akiwa huko.

"Haya yalifanyika kisiri... matibabu tuliyokuwa tukifanyiwa... yangeweza kutuua," aliiambia BBC.
Wengine waliohojiwa wanasema walivuliwa nguo na kupigwa kwa nyaya za umeme na mijeledi ya farasi, na mara kwa mara walikoseshwa usingizi.
Katika kifo chake mnamo Juni 2021, TB Joshua alisifiwa kama mmoja wa wachungaji wenye ushawishi mkubwa katika historia ya Afrika.

Akiinuka kutoka kwa umaskini, alijenga himaya ya kiinjilisti ambayo ilijivunia makumi ya viongozi wa kisiasa, watu mashuhuri na wanasoka wa kimataifa kati ya washirika wake.

Hata hivyo, alizua utata wakati wa uhai wake wakati nyumba ya wageni ya mahujaji wa kanisa ilipoporomoka mwaka wa 2014, na kuua watu wasiopungua 116.Uchunguzi wa BBC, ambao ulifanywa na jukwaa la kimataifa la vyombo vya habari vya Open Democracy, ni mara ya kwanza watu wengi wa zamani wa makanisa kujitokeza kuzungumza juu ya rekodi hiyo. Wanasema wametumia miaka mingi kujaribu kupaza sauti lakini wamenyamazishwa kwa ufanisi.

Baadhi ya mashahidi wetu nchini Nigeria wanadai walishambuliwa kimwili, na katika kisa kimoja walipigwa risasi, baada ya awali kujitokeza kupinga unyanyasaji huo na kuchapisha video zenye madai kwenye YouTube.

Wafanyakazi wa BBC ambao walijaribu kurekodi picha za boma la kanisa hilo Lagos kutoka mtaa wa umma mnamo Machi 2022 pia walipigwa risasi na usalama wa kanisa hilo, na walizuiliwa kwa saa kadhaa.

BBC iliwasiliana na Scoan na madai hayo katika uchunguzi wetu. Haikuwajibu, lakini ilikanusha madai ya awali dhidi ya TB Joshua.
"Kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Nabii TB Joshua si jambo geni... Hakuna madai yoyote yaliyowahi kuthibitishwa," iliandika.

Raia wanne wa Uingereza waliozungumza na BBC wanasema waliripoti unyanyasaji huo kwa mamlaka ya Uingereza baada ya kutoroka kanisani. Wanasema hakuna hatua zaidi zilizochukuliwa.

Anneka pictured in BBC studio interview, wearing white jumper

Maelezo ya picha: Anneka anasema anaamini kuna waathiriwa wengi ambao bado hawajazungumza

Zaidi ya hayo, mwanamume Muingereza na mkewe walituma barua pepe kwa mashahidi waliojionea ushahidi wao wa mateso na video - ikiwa ni pamoja na rekodi za kushikiliwa kwa mtutu wa bunduki na wanaume wanaojiita polisi ambao pia ni wanachama wa Scoan - kwa Ubalozi wa Uingereza nchini Nigeria mnamo Machi 2010 baada ya kukimbia kanisa hilo. Katika barua pepe yake, mwanamume huyo alisema mke wake alishambuliwa kingono mara kwa mara na Joshua. Aliionya ubalozi huo kuwa raia wengine wa Uingereza bado wako ndani ya boma hilo wakikabiliwa na ukatili.

Pia anasema hakuna hatua zilizochukuliwa. Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza haikujibu madai haya, lakini iliambia BBC kwamba inachukulia ripoti zote za uhalifu, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya raia wa Uingereza nje ya nchi, kwa uzito mkubwa.

Scoan inaendelea kustawi leo, chini ya uongozi wa mjane wa Joshua, Evelyn. Mnamo Julai 2023, aliongoza ziara ya kwenda Uhispania.

Anneka, ambaye aliondoka Derby nchini Uingereza na kujiunga na Scoan akiwa na umri wa miaka 17, aliambia BBC kuwa anaamini kuna waathiriwa wengine wengi ambao bado hawajazungumza. Anatumai hatua zaidi zitachukuliwa kufichua vitendo vya Joshua.

"Ninaamini Kanisa la Synagogue Church of All Nations linahitaji uchunguzi wa kina ili kujua ni kwa nini mtu huyu aliweza kufanya kazi kwa muda mrefu kama alivyofanya," alisema.

Ripoti ya ziada ya Maggie Andresen, Yemisi Adegoke na Ines Ward
Kwa usaidizi na taarifa kuhusu unyanyasaji wa kingono, tafadhali wasiliana na Mtandao huu wa BBC Actionline nchini Uingereza. Na kwa habari zaidi juu ya madhehebu, tafadhali tazama The Family Survival Trust

BBC
Pia soma: BBC imepanga kutoa video inayoonesha Unabii Feki wa TB Joshua
Simsaidii TB, ila kwa maelezo haya ya BBC ni kama kulipaka matope kanisa lake, swali la kujiuliza hapa ni kwanini walalamikaji waweza wakutoka Uingeleza na ni wazungu pekee???
 
Acha upotoshaji wapo hadi waafrika hadi binti yake tb Joshua.
 
No research, no right to speak!

BBC wamefanya uchunguzi wao, mnaopinga, leteni scientific counter arguments!

Nilianza kumshtukia huyu jamaa, baada ya kusikia his net worth, ndo nikaamini ni mwizi! So called manabii wengi ni janja janja na uhuni mtupu, wakichuma mapesa ya waumini wao akiwemo TB Joshua!

Poleni sana waumini wake!
 
Kuna Siri iliyofichika kwenye hiki knachoitwa "repoti ya Uchunguzi" ya BBC. Hebu jiulize nini kinatafutwa pale SCOAN kama BBC wanashambulia upande huu na upande mwingine DSTV wanapanga kuiondoa channel ya Emmanuel tv kwenye king'amuzi chao hapo tarehe 17/01/2024?
 
Shetani ana anapambana kuchafua ukristo...ila Moto wa Kristo ni balaa
Hataweza
Kinachowtsa ni mbegu aliyoiacha imekuwa balaa kuliko alivyokuwepo!.
Na hawakutegemea km mama atapiga kazi kuliko mumewe!.
Hawaamimi wanachokiona!.
Tupo hapa,subiri majibu!
 
Hapa ndio tuna apply ule mfano wa mpazi...hii ni Ile mbegu iliyozaa Moja mia,sitini Moja themanini....wataipata
 
Kitengo Cha uchungu Cha BBC eye kimeendelea kufichua uovu wa yule Nabii tapeli wa watu wavivi TB Joshua.

Inadaiwa kwamba bwana TB Joshua alidanganya mamlaka na kulipa pesa Ili ionekane Helikopta iligonga jengo l Kanisa lake na kisha kusababisha vifo vya watu 116.

Hata hivyo Uchunguzi wa BBC eye umeonesha kwamba jengo Hilo kiliporomoka kutokana na ujenzi duni na kuongeza Gorofa (floors) nyingi zaidi kuliko uwezo wake ,amri ambayo ilitolewa na TB Joshua licha ya kuonywa na mamlaka na wasimamizi wa Ujenzi.

On top of that Idadi kubwa ya Watu ilikufa tofauti na walioripotiwa ambapo miili ya watu ilisafirishwa usiku usiku Ili kukwepa vyombo vya habari na mamlaka huku hayo yakifanyika chini ya maelekezo ya TB Joshua na Ulinzi wa maofisa wake.

Taarifa hizi zinakuja kufuatia kufichuliwa Kwa habari za ubakaji na mateso ambayo bwana Joshua alikuwa akiwafanyia waumini wake.

Ukiwa na akili timamu afu huongozwi na hisia, Wala haitakusumbua kujua kuwa hizi ni feki news.
 
Kama mna nguvu mkabomoe makanisa yao na kuwafungia, pilipili usiyoila inakuwashia nini? Kama dini yako iko safi hao ambao unaona hawako safi waombwe. Hizo clip za Tb Joshua mbona hazina kitu cha ajabu ni yale yale tunayoyaona kwenye ibada zake zinazokuwa live, hao wanaosema walibakwa na kupigwa makofi na kufungwa minyororo tunawaaminije kama ni kweli? Pia ikumbukwe wengine walikuwa wanapelekwa pale wakiwa vichaa kwa usalama inabidi wafungwe kamba ili wasilete madhara kwa watu, wazungu wameshazoea kuwakandamiza watu weusi hasa wenye mali, mtu anakaa akiona maisha yamepiga ana miaka 50 anafungua kesi kuwa nilibakwa nikiwa na miaka 17 ili alipwe pesa, wao BBC wanajuaje miujiza fake na miujiza ya kweli? Ni shirika la kiroho? Miujiza fakes halafu uaminiwe na watu toka Africa, American, Ulaya, Asia
Mkuu, siku zote mtumishi wa MUNGU ambaye yupo very spiritual na ameyakabidhi maisha yake katika kumpendeza na kumtumikia MUNGU kwa moyo wake wote. Huwa wanaandamwa sana kwa uongo mwingi.

Marehemu tb Joshua alivyokua hai alikuwa akiwaombea na kuwaponya mashoga, hivyo walichoweza nikuishia kuzifungia chaneli zake za YouTube na kushindwa kuendelea kupambana nae.

Sasa hivi hayupo hai tena ndio wameona wafufue uongo mpya wakiwatumia ma albino wa kizungu. Kitu tusichokijua watu weusi hasa waafrika Huwa hatupendwi na wazungu sababu sisi uzao wetu umetokana na utaratibu aliopanga MUNGU.

Hawa wazungu uzao wao umetokana na dhambi, ndio maana wanatuchukia sana ni marangapi viongozi wa Afrika wamekua wakichafuliwa na BBC hata kwa Yale mazuri waliyofanyia nchi zao, ijapokua hatukatai kuwa wanamapungufu yao Kama binadamu.

Je, ufalme wa uingereza na viongozi wa nchi za magharibi hasa USA wanautakatifu gani mpaka kuonekana wema, mbona hatuoni episodes zenye shuhuda za watu kuhusu mabaya ya Vatican na pope kupitia BBC.
 
nimeiangalia yote,na pia nimeangalia maoni kadhaa yaliyotolewa na watu kadhaa,ama hakika nimeshindwa kabisa kujua mkweli nani
 
Back
Top Bottom