Donkey
JF-Expert Member
- Dec 17, 2010
- 1,499
- 1,584
Uko vizuri sana. Unaweza kuandika makala kubwa ya kuelimisha jamii na huu utapeli wa kilokole.? Shida za jamii ndiyo na matapeli wa kidini wanapita humohumo kujitajirishaKuna saikolojia fulani inawaonesha watu wengi kuwa ni wanyama fulani tu bado.
Kuna herd mentality inafanya watu wawe kondoo.
TB Joshua alijua hii saikolojia.
1. Alitumia pesa na mafanikio kuvutia watu masikini.
2. Alitumia miujiza feki kuvutia watu wanaopenda miujiza.
3. Alitumia wazungu kuvuta akili za Waafrika wajinga wengi. Kwenye documentary wameongelea hili kwamba Muafrika mjinga mara nyingi hata kama hakuamini, akiona Mzungu kakuamini inakuwa rahisi sana kumkamata, anaona huyu mtu kama hata wazungu wanamkubali basi lazima atakuwa anasema kweli.
4. Alitumia wanasiasa ambao na wao walimuhitaji kujitakasa waonekane watakatifu. Yani ilikuwa biashara ya Pwagu na Pwaguzi. TB Joshua nabii tapeli anatumia wanasiasa kuendesha mambo yake, na wanasiasa waongo wanamtumia TB Joshua kujisafisha waoneoane wasafi wanakubalika na mtu wa Mungu.
5. Alijua kutumia mwanya wa mapungufu ya social services kwa watu masikini. Nchi isiyo na hospitali, isiyo na ajira, isiyo na elimu watu wamepigika, hawana matumaini, TB Joshua akaibuka kama mtu wa Mungu mwenye kufanya miujiza, kuwapa watu magunia ya mchele na pesa, watu wakaona huyu ndiye nabii wa kweli. Serikali zingemaliza matatizo ya watu zingepunguza mianya ya hawa matapeli kuibuka.
Tanzania na sisi tujifunze, kwa sababu tunao watu kama TB Joshua.