Uendeshaji wa Bandari: Wabunge Wataka Rais Samia asirudi nyuma

Uendeshaji wa Bandari: Wabunge Wataka Rais Samia asirudi nyuma

WABUNGE wameishauri serikali kutosikiliza maneno ya watu wa mtandaoni kuhusu ushirikiano wa Serikali za Tanzania na Dubai katika makubaliano ya uwekezaji kwenye bandari zilizopo nchini (IGA) kwa kuwa wanaofanya hivyo hawaitaki nchi mema.

Pia, wameitaka serikali kuharakisha kusaini mikataba inayohusiana na suala hilo, ili bandari iwe sehemu ya kuchangia Pato la Taifa na kuletea maendeleo. Waliyasema hayo jana wakati wanachangia hoja ya Mapendekezo ya Serikali kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2023/24.

Mbunge wa Jimbo la Ukonga (CCM), Jerry Silaa, alishauri serikali isikubali maneno ya watu wasiotaka iendelee kiuchumi ambao wanapinga uamuzi wake wa kushirikisha sekta binafsi kwenye maendeleo, ikiwamo ushirikiano ilioyongia na Serikali ya Dubai kuhusu uwekezaji kwenye bandari nchini.

Alifafanua kuwa IGA siyo mkataba wa utekelezaji bali ni makubaliano baina ya Serikali ya Tanzania na Dubai kuhusu uwekezaji utakaofanyika kwenye bandari zilizopo katika chi hiyo na kwamba mikataba ya kwenda kutekeleza miradi bado haijaingiwa.

Silaa alisema ushirikiano huo utaongeza ufanisi wa bandari na kufikia malengo ya serikali ya kukuza uchumi wa nchi kwa kuongeza forodha na kuboresha sekta za uchumi ikiwamo kilimo.

"Niombe serikali ikubali ushauri, isikilize wananchi, lakini wakati mwingine isikubali kuyumbishwa na watu wenye nia zao za kuitaka nchi yetu isiendelee kiuchumi, ikubaliane na hoja za msingi za kutetea taifa letu, tuwe na uwekezaji na kushirikisha sekta binafsi katika ameneo ambayo wenzetu wamebobea," alisisitiza.

Kadhalika, alisema serikali haiwezi kupiga hatua bila ushirikiano na sekta binafsi huku akitoa mfano wa moja ya mafanikio ya ushirikishwaji wa sekta hiyo kuwa ni Benki ya NMB ambayo hivi karibuni serikali imevuna gawiwo la Sh. bilioni 45.5 na kodi ya Sh. bilioni 453.

Aidha, Mbunge huyo alishukuru serikali kwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwamo ujenzi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere, ambalo utekelezaji wake umefikia asilimia 96, ujenzi wa reli za umeme na adaraja la Kigogo Busisi, mradi wa mwezndo kasi awamu ya tatu, Gongo la mboto-Kariakoo.

Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Pwani (CCM), Subira Mgalu, alishauri serikali kuchukua hatua za haraka kuleta mikataba itakayotokana na IGA ili wawekezaii waje na bandari iwe na nafasi ya kuchangia katika pato la ndani la taifa na serikali ipunguze kukopa.

Kahusu hoja ya kuitwa mbunge mmoja mmoja kupigia kura muswada huo iliyotolewa na mbunge mstaafu Prof. Anna Tibaijuka, alisema hauna mashiko kwa kuwa utaratibu huo unafanyika kwenye kupitisha bajeti ya serikali pekee, masuala mengine ni utaratibu wa kuhojiwa na walishafanya hivyo.

"Lakini nataka nimkumbushe Prof. Tibaijuka alipokuwa waziri 2013 aliwasilisha mpango wa kuifanya Kigamboni kuwa mji wa trilioni 11, haukufanikiwa na tulioupitisha kwa kura za kuhojiwa kwa hiyo aiache serikali inayoongozwa na mwanamama menzie (Rais Samia Suluhu Hassan) ifanye kazi yake," alisema.

Hivi karibuni, Prof. Tibaijuka akihojiwa na chombo kimoja cha habari, alikosoa utaratibu wa kura ya pamoja uliotumiwa na Bunge katika kupitisha Azimio la Bunge kuhusu Mapendekezo ya Kuridhia Makubaliano Kati ya Tanzania na serikali ya Dubai kwenye ushirikiano wa kiuchumi na kijami kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi wa bandari Tanzania.

Aidha, aliwatoa hofu wananchi kuwa bandari haiwezi kuuzwa kwa serikali kugawana idadi ya gati na mwekezaji bali mbinu iliyotumika ni kushirikisha sekta binafsi katika kukuza utendaji kazi wa bandari na kukuza uchumi wa nchi.

Vile vile, alisema bajeti kuu imeonyesha dhamira ya serikali ya kureiesha uuzwaji wa bidhaa nje ya nchi kwa kutenga zaidi ya Sh. bilioni 800 wazalishaji wa mazao, ili kuliletea taifa fedha za kigeni na kukuza uchumi.
Pia, katika mapendekezo ya bajeti ya serikali inatarajia kukusanya Sh. trilioni 44, kati ya hizo Sh. trilioni 31 zitakusanywa kutoka mapato ya ndani na kwamba ni lazima seri-kali ishirikishe sekta binafsi katika uwekezaji.

Aliwataka wananchi kuendelea kutoa na kudai risiti wanapofanya ununuzi ili kuhakikisha kuwa wanalipa kodi na serikali isiendelee kuleta kodi mpya kwa kuwa inategemea pesa hizo kutekeleza miradi ya maendeleo. Mbunge wam Sengerema, Hamis Tabasamu, alimshauri Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, kutokatishwa tamaa na maneno yanayozunguka mitandaoni na mitaani bali kuwa na imani jambo analolifanya litakwenda kuiletea mafanikio nchi.

"Kuna watu ni majemedari wa kupiga kelele kwenye mitandao na kila maeneo, Mheshimiwa Waziri wa Fedha, maneno haya yangekuwa yanatoboa mwili wako leo ungekuwa umejaa viraka na bandeji mwili mzima, kwa hiyo unachotakiwa sasa hivi ni kuwa na ngozi ngumu tu kujenga imani halafu baadaye unatoboa," alisema.

Alimshauri waziri huyo kuwashirikisha wabunge wakati wa uandaaji wa baieti hizo ili watoe ushauri wa vitu muhimu vya kuwapo na kutokuwapo kwa kuwa wao wanajua matatizo ya wananchi ambao wengi wao kukosa pesa ndiyo kunawafanya waitukane serikali kwenye mitandao.​
Bado kulibinafsisha Bunge asirudi nyuma maana mmefeli kila kitu.
 
Bado kulibinafsisha Bunge asirudi nyuma maana mmefeli kila kitu.
Hakuna kitu kama hicho . Acha kejeli mkuu. Bunge letu tukufu limejaa uweledi wa kutosha. Nakusudia kuandaa petition ili wabunge hawa waendelee hata bada ya 2025. Unaonaje weye?
 
Huo mkataba ni wa miaka mingapi kwani? Na kwanini waseme haturuhusiwi kujiondoa kwenye mkataba huo hata Yesu akirudi?
 
Hakuna options zaidi ya kwenda mbele ...sio kurudi Kwa Ticts tena
TICTS anapambana bado ni sawa na kuku aliyekatwa shingo mwili wake unarukaruka huku damu akiisambaza mahali pote. Nadhani unamsikia Mama Tibaijuka anavyojaribu kuleta tafsiri potofu ya ujio wao hapa Tanzania.
Mnapotosha hoja kudhani wanaopinga huo mkataba ni Ticts. Hamjibu swali langu la kwa nini DPW haiwekezi kwa aina ya mkataba wa Ticts ukaboreshwa kuondoa makandokando
 
Mnapotosha hoja kudhani wanaopinga huo mkataba ni Ticts. Hamjibu swali langu la kwa nini DPW haiwekezi kwa aina ya mkataba wa Ticts ukaboreshwa kuondoa makandokando
Hujaeleweka uliza tena na weka hoja yako wazi ili upewe majibu yaliyoenda shule.
 
Mnapotosha hoja kudhani wanaopinga huo mkataba ni Ticts. Hamjibu swali langu la kwa nini DPW haiwekezi kwa aina ya mkataba wa Ticts ukaboreshwa kuondoa makandokando
Wewe ni Mtaalam wa mikataba?
Lazima uonavyo wewe ndo best and only best way forward??
 
Neno kuaza achana nalo mkuu. Hapa ni uwekezaji. Acha kupotosha mkuu. We are talking about investment. Basi.
Tofautisha uwekezaji na uwekezaji. Kama wanataka kuwekeza, wapelekwe huko Bagamoyo, wakafanye ujenzi wa bandari mpya, siyo kuja kudandia bandari ambayo tayari nchi imewekeza matrioni ya pesa.

Hawa ni sawa uwe na lorry lako, mtu akuambie kuwa anataka umpe aliendeshe, wakati wa uendeshaji atagharamia matengenezo yote, halafu wewe mwenye lorry eti usipate chochote kutoka kwenye faida itakayopatikana.
 
Wewe ni Mtaalam wa mikataba?
Lazima uonavyo wewe ndo best and only best way forward??
Hujajibu swali langu. Sheria zilizopo za uwekezaji kama hazikidhi mahitaji ya uwekezaji wa DPW suala lipelekwe bumgeni
 
Tofautisha uwekezaji na uwekezaji. Kama wanataka kuwekeza, wapelekwe huko Bagamoyo, wakafanye ujenzi wa bandari mpya, siyo kuja kudandia bandari ambayo tayari nchi imewekeza matrioni ya pesa.

Hawa ni sawa uwe na lorry lako, mtu akuambie kuwa anataka umpe aliendeshe, wakati wa uendeshaji atagharamia matengenezo yote, halafu wewe mwenye lorry eti usipate chochote kutoka kwenye faida itakayopatikana.
Mifano na maelezo yako haviendani kabisa.
 
Jambo la ukomo kutokuwa bayana lilishabainika litafanyiwa kazi. Kuwa na subra na acha uchochezi.
 
Mnapotosha hoja kudhani wanaopinga huo mkataba ni Ticts. Hamjibu swali langu la kwa nini DPW haiwekezi kwa aina ya mkataba wa Ticts ukaboreshwa kuondoa makandokando
TICTS wameshindwa kwenda sambamba na kile walichoahidi kukifanya tangu 2017. Ni muda wa kuingia mkataba na mwekezaji mwingine mwenye teknolojia mpya na za kisasa.
 
TICTS wameshindwa kwenda sambamba na kile walichoahidi kukifanya tangu 2017. Ni muda wa kuingia mkataba na mwekezaji mwingine mwenye teknolojia mpya na za kisasa.
Vyema wameshindwa, je, sababu za kushindwa zimelezwa? Kama wameshindwa wapewe wenye uwezo kwa mkataba wa "win-win situation"
 
Mimi naunga mkono makubaliano ya ushirikiano na maendeleo na Dubai katika yote yaliyoainishwa kwenye mkataba uliojadiliwa bungeni.

Wewe unaepinga unapinga nini? (Hatutaki ngonjera).
Sawa.....usimjaze upepo mheshimiwa Raisi.....mwacheni afanye kile anachoona kinafaa,ukipinga wewe ulikuwa na maslahi,ukitetea wewe ni chawa....taifa la hovyo Sana hili.
 
Back
Top Bottom