realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 7,450
- 19,184
Yani weweInabidi mpatane kwanza imani zaidi ya 200000 mje na Mungu mmoja kwanza , ili mje na hoja zenye mashiko.
Yani weweInabidi mpatane kwanza imani zaidi ya 200000 mje na Mungu mmoja kwanza , ili mje na hoja zenye mashiko.
Sasa unataka kujadili Mungu na wasioamini Mungu, wakati hata wasio amini Mungu hawazidi 100 humu ila wanao amini Mungu wapo zaidi ya laki na bado wanapingana Mungu yupi ni sahihi🤔Yani wewe
Unakumbuka kabla ya ujio wa internet watu walidhani ujinga ni sababu ya kukosa taarifa?Tutaendelea tu kuuliza na kuhoji ila kamwe hauta nikuta kanisani au msikitini nikihoji
Nimekushindwa 😅Sasa unataka kujadili Mungu na wasioamini Mungu, wakati hata wasio amini Mungu hawazidi 100 humu ila wanao amini Mungu wapo zaidi ya laki na bado wanapingana Mungu yupi ni sahihi🤔
Africa bado sana kuna wengi tu hata hawajui matumizi ya InternetUnakumbuka kabla ya ujio wa internet watu walidhani ujinga ni sababu ya kukosa taarifa?
Kuna ka kitu umekapata hapo?Nimekushindwa 😅
Yaaa sana tuKuna ka kitu umekapata hapo?
Nikushauri kitu , kama unataka kubaki na imani yako kwa amani,usisome majadiliano ya atheists mahali popote pale .Yaaa sana tu
Na wanaojua?Africa bado sana kuna wengi tu hata hawajui matumizi ya Internet
Niliuliza maswali mawiliSayansi ina mipaka haiwezi kukupa majibu ya kila kitu,kuna baadhi ya mambo utahitaji dini upate majibu
Usipomjua Mungu au uwezo wake ndio hapo unapompa washirika na kuwafanya wawe wengi kwakuwa unajua mambo makubwa hufanywa na wengi
Kufupisha story,Mungu akitaka kitu husema tu KUWA na kina KUWA, kama nabii Yesu alizaliwa tu kwa neno lililotiwa kwa Bikira Maria
Sawa nitazingatia. AsanteNikushauri kitu , kama unataka kubaki na imani yako kwa amani,usisome majadiliano ya atheists mahali popote pale .
Kwa sababu unaweza soma ndio na kusiwe na shida ila akili automatically tu haijawahi kutulia pale inapodanganywa na kuupata ukweli ila kwa makusudi kabisa , ikagoma kuupokea kwa kulinda imani.
Kinachofanyika sasa ni defence mechanism ya ubongo ila kuukataa ukweli na kulinda imani.
Hivyo achana kabisa kusoma hoja za atheists , ukienda reddit, qoura , jf , x na popote pale, kama unataka kuilinda imani.
Itakua kinyume chakeNa wanaojua?
umewahi kufanya research yoyote ya archaeology?Kwanza sitaki kuamini kwamba dini imekuwa submanipulative ,ila tuliache hili kwasababu umetaka sasa tutumie tools nyingine tofauti na dini
Nakuletea hoja kwanini sisi au miili yetu ni udongo.
Kutokana na mtazamo wa kisayansi na mazingira, kuna hoja kadhaa zinazoweza kutumika kuangalia uhusiano mkubwa uliopo kati ya mwili wa binadamu na ardhi (udongo). Ingawa sayansi haitumii neno "kuumbwa" kama imani zinavyofanya, inathibitisha kuwa viungo vya msingi vinavyounda mwili wa mwanadamu vinatoka ardhini.
Hapa kuna mambo muhimu ya kimazingira na kibaolojia yanayothibitisha uhusiano huo:
1. Muundo wa Kikemia (Chemical Composition)
Mwili wa mwanadamu umeundwa na elementi mbalimbali ambazo zote zinapatikana kwenye tabaka la juu la ardhi (udongo).
Elementi Kuu: Oksijeni, kaboni, hidrojeni, na nitrojeni zinaunda asilimia kubwa ya mwili.
Madini: Madini kama kalsiamu (kwenye mifupa), chuma (kwenye damu), fosforasi, potasiamu, na magnesiamu ni elementi zilezile zinazopatikana kwenye udongo na miamba.
2. Mzunguko wa Chakula (The Food Chain)
Mwanadamu hawezi kuishi bila kula, na chakula chote tunachokula kina asili yake kwenye udongo:
Mimea: Huchukua virutubisho na madini moja kwa moja kutoka kwenye udongo ili kukua.
Wanyama: Hula mimea hiyo na kubadilisha virutubisho hivyo kuwa protini na mafuta.
Binadamu: Tunapokula mimea au wanyama, tunauingizia mwili wetu yale madini na elementi zilizokuwa kwenye udongo. Hivyo, mwili wako ni "udongo uliofanyiwa marekebisho" kupitia mfumo wa chakula.
3. Mzunguko wa Maji na Uhai
Udongo una sifa ya kushikilia maji, na mwili wa binadamu una takriban 60% hadi 70% ya maji. Bila madini yanayopatikana kwenye udongo (electrolytes kama chumvi na potasiamu), mwili wetu hauwezi kuhimili maji hayo kwa ajili ya mawasiliano ya neva na kazi za seli.
4. Hatima ya Mwili (Decomposition)
Moja ya uthibitisho mkubwa wa kimazingira ni kile kinachotokea baada ya kifo. Kupitia mchakato wa kuoza (decomposition), mwili wa binadamu hurudi katika hali yake ya asili.
Bakteria na viumbe hai wa udongoni huuvunja mwili na kuurejesha kuwa virutubisho, nitrojeni, na madini ambayo yanarudi ardhini kurutubisha udongo tena.
5. Uhusiano wa Kiikolojia
Binadamu anategemea mazingira ya nchi kavu ili kuishi. Hewa tunayovuta inatengenezwa na mimea iliyoota kwenye udongo. Hii inaonyesha kuwa kuna muunganiko usioweza kutenganishwa kati ya mfumo wa kibaolojia wa binadamu na mfumo wa kijiolojia wa dunia.
Kama tukiuchukua mwili wa mwanadamu na kuuvunja katika sehemu zake ndogo kabisa za kikemia, tunapata "vumbi" au elementi zilezile zinazounda dunia tunayokanyaga. Mazingira yanathibitisha kuwa sisi ni sehemu ya dunia, tunakula kutoka duniani, na mwishowe tunarejea kuwa sehemu ya udongo huo huo.
1. Kuna uthibitisho gani usio wa kisayansi? Hiyo dhana nzima ya kwamba uwepo wa Mungu upo nje ya mfumo wa jisayansi ni chaka la kupitisha uongo wowote.1. Je unataka uthibitisho wa namna gani maana unaomba uthibitisho wa kiwango cha kisayansi kwa kitu ambacho kwa definition kiko nje ya mfumo wa kisayansi. Sayansi inachunguza vitu vinavyoweza kupimwa, kurudiwa, na kuthibitishwa kwa majaribio. Mungu kama Supernatural Power kwa definition yake yenyewe yuko nje ya mfumo huo. Kuomba ushahidi wa kisayansi wa Mungu ni kama kuomba kipimo cha thermometer kupimia uzito chombo sahihi, lakini si kwa kazi hiyo. Hii haimaanishi Mungu hayupo inamaanisha kwamba mbinu yako ya kuthibitisha haifai kwa swali hili.
2. Swali lako linaonyesha kwamba unachukulia 'uovu' ni kitu halisi kwamba maumivu ni mabaya kweli kweli, kwamba haki ipo. Lakini kama Mungu hayupo kwa nini maumivu ni 'mabaya'? Kwa nini udhalimu ni 'mbaya'?
Katika ulimwengu wa atom tu bila Mungu maumivu ni kemikali tu, kuumia na kufurahi hakuwezi kwwa na defn ya uzuri na ubaya. udhalimu na ukatili ni swala la genetics tu. Hakuna 'mbaya' au 'nzuri' ni matukio tu ya kemikali. Kwa hiyo swali lako la Problem of Evil linategemea imani kwamba uovu ni mbaya kweli kweli na imani hiyo yenyewe inahitaji Mungu awepo ili iwe na maana.
pia una swali lako linaloukiza kwamba Mungu mwenye upendo lazima athibitishe uwepo wake kwa njia inayoondoa shaka. lakini fikiria kama Mungu angetokea mbele yako leo na nguvu zake zote wazi na akakuthibutushia bila shaka je, ungekuwa na uhuru wa kumchagua au kumkataa? Hapana. Ungekuwa unamwamini kwa sababu ya woga au nguvu yake si kwa upendo wa kweli. Upendo wa kweli unahitaji uhuru na uhuru unahitaji uwezekano wa kutokuamini. ni kama huku tz tunavodai haki ianze ndo amani ifuate Kwa hiyo kutokuwepo kwa ushahidi wa wazi kunaweza kuwa sehemu ya design.
na hayo maswalinmengume mawili ya mwanzo yameshajadiliwa humu sana hata kwenye Uzi huu na hakuna hoja ya Atheist inayojitosheleza labda kama kuna uwepo wa supernatural power
1. Wewe mwenyewe unaamini mambo mengi ambayo hayathibitishwi kwa sayansi. Unaamini kwamba maumivu ni mabaya sayansi haiwezi kuthibitisha hilo. Unaamini kwamba ukatili ni mbaya sayansi haiwezi kuthibitisha hilo. Hizi ni imani za kimantiki na kimaadili na hisia za mmwili wako si za kisayansi. Kwa hiyo mfumo wako mwenyewe una mambo yanayokwepa sayansi. unaamini Julius Caesar alikwepo na vitu vinavyofanana na hivi ingawa haviwezi kuthibitishwa kisayansi1. Kuna uthibitisho gani usio wa kisayansi? Hiyo dhana nzima ya kwamba uwepo wa Mungu upo nje ya mfumo wa jisayansi ni chaka la kupitisha uongo wowote.
Hata mimi naweza kukuambia mimi ni Mungu, ila huwezi kujua hilo kwa sababu uthibitisho wake upo nje ya mifumo ya kisayansi.
Utapingaje?
Huoni kuwa dhana nzima ya uthibitisho ni sehemu ya sayansi?
Huoni kuwa hoja ya "uthibitisho wake upo nje ya mifumo ya kisayansi" inaweza kupitisha uongo wowote?
2. Kama mimi sipendi kuumizwa na kuuawa, kuumizwa na kuuawa ni jambo baya kwangu. Kwa nini nimhitaji Mungu ili maumivu na mimi kunyimwa haki ya kuishi, kufurahia maisha na wenzangu kuwa ni jambo baya?
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kutojithibitisha wazi kiasi watu wanapigana vita za kidini kwa kuamini Mungu tofauti ni ukatili. Angeweza kujithibitisha kiasi cha kuondoa utata, lakini si kiasi cha kutisha.
Kwa nini hakufanya hivyo?
Mungu mwenye upendo wote kuachia utata utawale kiasi watu wameuana kwa mamilioni ni ukatili.
Mungu mwenye upendo wote kuwa pia mkatili hivyo ni contradiction.
Contradiction hii inaonesha Mungu huyo hayupo, katungwa na watu tu.
Hivyo, ukiona mjadala wa kujadili uwepo wa Mungu ni ushahidi kuwa Mungu hayupo.
Angekuwapo, tusingeweza hata kujadili uwepo wake, kila mtu angejua yupo kwa hakika.
1. Hujaelewa hoja. Hoja si mimi naamini au siamini nini. That is irrelevant. Logical non sequitur fallacy. Mimi naweza kuamini mambo yasiyothibitishika kisayansi. Ya uongo kabisa. Sijawahi kusema sina makosa.1. Wewe mwenyewe unaamini mambo mengi ambayo hayathibitishwi kwa sayansi. Unaamini kwamba maumivu ni mabaya sayansi haiwezi kuthibitisha hilo. Unaamini kwamba ukatili ni mbaya sayansi haiwezi kuthibitisha hilo. Hizi ni imani za kimantiki na kimaadili na hisia za mmwili wako si za kisayansi. Kwa hiyo mfumo wako mwenyewe una mambo yanayokwepa sayansi. unaamini Julius Caesar alikwepo na vitu vinavyofanana na hivi ingawa haviwezi kuthibitishwa kisayansi
2.Unasema kuumizwa ni mbaya kwako nakubaliana nalo. lakini Problem of Evil haizungumzii preference yako au mapendelo yako binafsi. Inazungumzia madai ya maadili ya ulimwengu wote kwamba ukatili ni mbaya kwa kila mtu, wakati wote, mahali pote. Preference yako ya kibinafsi haifikii hapo. kuna mtu anapenda kuumiza wengine ana preference yake pia na nikitu kinachomfurahisha kwaiyo kwake ni kiziri preference yake ni halali sawa sawa na yako. Kwa nini yako ni sahihi zaidi?
3.Unasema vita za kidini ni ushahidi wa ukatili wa Mungu. lakini vita za kidini zimefanywa na binadamu si Mungu. Binadamu wamechukua jina la Mungu na kutumia kwa maslahi ya nguvu, siasa, na ubinafsi. Kulaumu Mungu kwa matendo ya binadamu wanaotumia jina lake vibaya ni kama kulaumu Einstein kwa silaha za nyuklia aliandika equations, watu wengine walichagua kuzitumia vibaya. au kumlaumu mtu aliyetengeneza kisu kwasababu kuna watu wanauawa kwa kuchomwa visi
pia una logical fallacy inayoitwa Argument from Ignorance kusema kwa sababu hatujui kwa uhakika, kitu hakipo. Lakini ukweli wa kitu hautegemei uelewa wetu wa kitu hicho. Kwa maelfu ya miaka binadamu hawakujua vijidudubkama bakteria vipo je, vijidudu havikuwepo? Hawakujua galaxies nyingine zipo je, hazikuwepo? Kutojua au kutokubaliana juu ya kitu hakuthibitishi kitu hicho hakipo.
Unasema Mungu angekuwepo, mjadala usingekwepo. lakini hata kama Mungu yupo na anajithibitisha binadamu bado wangeweza kukataa. Hii si nadharia binadamu wanakataga ushahidi wa kisayansi ulio wazi kila siku. Watu wanaamini dunia ni flat licha ya ushahidi wote. Kwa hiyo hata ushahidi wazi haumalizi mjadala kwa sababu tatizo si ushahidi, tatizo ni binadamu na uhuru wao wa kukataa.
poa kwakonaona pattern moja katika hoja zako zote: unabeba mzigo mkubwa wa assumptions ambazo wewe mwenyewe hujazithibitisha kwamba maadili yanaweza kuwepo bila msingi wa nje ya binadamu, kwamba Mungu mwenye upendo lazima aondoe matokeo yote ya uhuru, kwamba uthibitisho wote lazima uwe wa kisayansi. Kila assumption hiyo yenyewe inahitaji mjadala mrefu.
Kwanini wewe umejiamulia ku assume hivyo ?
Kwa asilimia kubwa umejibu hoja zangu,usijali kuhusu maandiko marefu huwa hayanipi shida huenda kwasababu kusoma ni sehemu ya hobby yanguumewahi kufanya research yoyote ya archaeology?
ok nitajibu hoja zako kwa ustaarabu sana ndugu yangu!
na nitajibu kwa maneno mengi ili uelewe tafadhali bear with me usichoke kusma..
1. Muundo wa Kikemia (Chemical Composition)
Ni kweli kabisa na sikatai kwamba mwili wa binadamu una elementi kama oksijeni, kaboni, hidrojeni na nitrojeni, na hizi pia zinapatikana ardhini. Lakini kufanana kwa elementi hakuthibitishi chanzo cha uumbaji.
kwanini?
Hizi elementi hazipo kwenye udongo tu zipo pia kwenye hewa, maji, na hata kwenye nyota. Hivyo, huwezi kuchagua udongo kama chanzo pekee yake na ukahitimisha..kwanini usiseme binadamu katokana na Maji (kama wanavyosema wale wnaoamini kwenye ANUNAKI au kwanini usiseme katokana na upepo?
sasa hiyo sio justfication Zaidi ya hapo, kujua kitu kimeundwa na nini (composition) si sawa na kujua kimetoka wapi (origin). Hii ni kama kuchambua gari ukapata chuma, halafu useme limetokana na udongo hapo unachanganya material na source ya uumbaji...
kwa kumbukumbu zangu Wanyama na mimea pia na wenyewe wana composition sawa kabisa na hizo za binadamu na kwa bahati mbaya kabisa Mnyama hakuumbwa kwa udongo (kulingana na maandiko matakatifu)..
sasa hii hoja yako inaonyesha nini inaonyesha Hoja hii inaonyesha material similarity, si proof ya creation.
kwa hii hoja hata kama ungelichukua kiumbe chochote hata kama ungeleta kiumbe kutoka sehemu nyingine kama sayari ya Mars akikaa duniani, atalazimika kuvuta hewa yenye nitrogen na oksijeni, na atakula mimea au wanyama wanaotegemea udongo.
Matokeo yake, mwili wake utaanza kuwa na hizi hizi elementi zinazopatikana duniani. Lakini hiyo haitamaanisha kwamba chanzo chake ni udongo bali inaonyesha tu kwamba mazingira anayokaa yanaathiri muundo wa mwili wake.
Kwa hiyo, hoja ya kwamba binadamu ni udongo kwa sababu ya hizi elementi haijathibitisha, bali inaonyesha tu kwamba binadamu anaishi ndani ya mfumo wa dunia unaompatia elementi hizo.
ngoja nikuongezee na kitu kimoja (chanzo cha kukuuliza kama umewahi kufanya archeology study yoyote)
Hivi unajua kuwa composition (muundo wa kikemia na kibaolojia) ya miili ya viumbe hai, ikiwemo binadamu mwenyewe , inaweza kubadilika na imekuwa ikibadilika kulingana na era (zama) na miaka.
Mabadiliko haya hayatokei kwa sababu elementi hizo zimeumbwa au ni udongo bali yanatokea kwa sababu ya mabadiliko katika mazingira, lishe, na teknolojia. Hapa kuna namna mbalimbali ambazo muundo wetu unabadilika,na nikuambie tu sasa hivi kuna Mabadiliko ya Kikemia (Chemical/Isotopic Signatures)ya binadamu ambayo zamani ilikuwa haipo kwahyo unataka kuniambia kuwa Mungu alibadilisha Udongo?? kwa zaman hizi?? Miili ya binadamu wa sasa ulisahau kuwa pia ina kiasi kikubwa cha elementi kama Strontium au Lead (Risasi) kutokana na uchafuzi wa mazingira na matumizi ya nishati ya fossil fuels
vipi na yenyewe tuseme kuwa mungu amebadili udongo...
sasa naomba hii niiweke kwa Rangi nyekundu kwenye hoja hii kuu ya kwako..
unafahamu kuwa Kuna Microplastics na Kemikali Nyingine ambazo kwenye miili zamani haikuwepo ila sasa hivi ipo? wanasayansi wanaita Modern Composition
Hii ni pointi ya kipekee kwa era yetu au tunaiita The Anthropocene, Katika miaka 50 iliyopita, muundo wa mwili wa binadamu umeanza kuwa na vitu ambavyo havikuwepo kabisa katika era za nyuma tafiti za hivi karibuni zimegusa damu, mapafu, na hata kondo la nyuma (placenta) la binadamu zikionyesha chembechembe ndogo za plastiki, vipi sasa tuamini pia kwamba Mungu aliumba kwa kutumia plastic vizazi vya sasa hivi na udongo vya zamani??
Miili yetu sasa ina vitu kama PFAS ambavyo mababu zetu hawakuwa navyo. Hii ina maana "udongo" tunaokula sasa hivi kupitia chakula umechafuliwa, hivyo "composition" yetu inabadilika na inazidi kubadilika..
nadhani kwa hoja hii umenielewa hakuna justification ya uumbaji kwa just elements tu kuonekana...
2. Mzunguko wa Chakula (Food Chain)
Ni kweli kwamba chakula tunachokula kina asili ya udongo kupitia mimea, lakini hii inaonyesha utegemezi wa mazingira (dependence), si chanzo cha uumbaji.
Kiumbe chochote kinachoishi duniani hata kama kingetoka sehemu nyingine kitalazimika kula kutoka kwenye mfumo huu huu wa chakula. Matokeo yake kitapata hizi hizi elementi mwilini.
Hivyo, uwepo wa elementi hizo mwilini unaonyesha tu kwamba tunaishi kwenye mfumo wa dunia, si kwamba tumetokana na udongo. na kula chakula hata ukitoka mars lazima utakula miili imeumwwa kwa ajili ya kupata nguvu na nishati kutoka kwenye chakula..
Samaki anaishi kwenye maji na mwili wake umejaa maji, lakini hatusemi “ametengenezwa na maji.”
kwahiyo Hoja hii yako ya pili inaonyesha nutritional cycle, si creation process.
hoja zingine nitazijibu kwa pamoja
Kuhusu mwili wa binadamu kuwa na maji mengi ni kwamba mwili unahitaji unahitaji electrolytes ili kufanya kazi, na hii ni sehemu ya physiology (jinsi mwili unavyofanya kazi), si ushahidi wa chanzo chake.
Maji na madini ni vitu vya msingi vinavyopatikana katika mazingira yote ya dunia. Hivyo, kuvitumia hakuthibitishi umetokana na udongo inaonyesha tu umeadapt kwenye mazingira ya dunia.
Ni kweli mwili hurudi katika elementi zake za msingi baada ya kifo, lakini kurudi kwenye kitu si uthibitisho kwamba ndipo ulikotoka mwanzo.
Huu ni mzunguko wa asili (natural cycle), si ushahidi wa chanzo.
Mfano: ukichoma karatasi inakuwa majivu, lakini hatusemi karatasi ilitoka kwenye majivu.
Vivyo hivyo, mwili kurudi udongoni haimaanishi kwamba ndipo ulikotoka inaonyesha tu kwamba unaingia kwenye mzunguko wa mazingira baada ya kifo.
natumaini nimejibu Hoja zako
Niliuliza maswali mawili
1. Kila kitu kiliumbwa, Mungu aliumbwa na nani?
1. Uwiano na Umoja wa Kanuni za Asili (The Argument from Design)2. Na kama dunia imeumbwa una uhakika gani aliyeiumba ni mmoja?
Got it, Mungu hakuumbwa1. Mtazamo wa Kidini (Theolojia)
Katika imani nyingi za kidini (kama Uislamu na Ukristo), sifa kuu ya Mungu ni kwamba yeye ni wa milele—hana mwanzo wala mwisho.
Mungu kama Chanzo: Imani hizi zinafundisha kuwa kila kitu kilichopo kiliumbwa, lakini lazima kuwe na "Chanzo kisichochimbika" (Uncaused Cause). Ikiwa Mungu angekuwa ameumbwa, basi huyo aliyemuumba angekuwa "Mungu" zaidi yake, na mfululizo huo ungeendelea bila mwisho.
Nje ya Muda na Nafasi: Dini zinaeleza kuwa "kuumbwa" ni tendo linalohitaji muda na nafasi. Kwa kuwa Mungu anachukuliwa kama muasisi wa muda na nafasi, yeye yuko nje ya sheria hizo. Kwa hiyo, swali "aliumbwa na nani" halimtahini yeye kwa sababu yeye si kiumbe.
2. Mtazamo wa Kifalsafa na Mantiki
Wanafalsafa hutumia hoja ya Mstari wa Sababu (Infinite Regress):
Sababu ya Kwanza: Ili ulimwengu uwepo, lazima kuwe na kitu cha kwanza ambacho hakikuhitaji kusababishwa na kitu kingine. Kama kila kitu kingehitaji muumbaji, basi tusingekuwa na mwanzo kabisa, na ulimwengu usingekuwepo leo.
Hoja ya Aristoteli: Mwanahisabati na mwanafalsafa Aristoteli aliita dhana hii kama "Unmoved Mover" (Mwenye kusogeza asiyesogezwa). Ni nguvu au hulka ambayo ilianzisha kila kitu bila yenyewe kuanzishwa.
3. Mtazamo wa Kisayansi
Sayansi (kama Fizikia ya Quantum) mara nyingi haijibu swali la "Mungu," bali huangalia chanzo cha ulimwengu (kama vile Big Bang). Hata hivyo, changamoto inabaki pale pale: Nini kilisababisha Big Bang? Wanasayansi wengine wanahoji kuwa nishati au kanuni fulani za kifizikia zinaweza kuwa zilikuwepo daima.
Kimantiki, ikiwa Mungu aliumbwa, basi huyo aliyemuumba ndiye angekuwa Mungu wa kweli. Ili kuepuka mfululizo usio na mwisho wa waumbaji, hitimisho la kifikra ni kwamba lazima kuwe na asili ya kwanza ambayo haikuumbwa na yeyote—na hiyo asili ndiyo watu wanaiita "Mungu."