Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 89,019
- 156,726
1. Mtazamo wa Kidini (Theolojia)
Katika imani nyingi za kidini (kama Uislamu na Ukristo), sifa kuu ya Mungu ni kwamba yeye ni wa milele—hana mwanzo wala mwisho.
Mungu kama Chanzo: Imani hizi zinafundisha kuwa kila kitu kilichopo kiliumbwa, lakini lazima kuwe na "Chanzo kisichochimbika" (Uncaused Cause). Ikiwa Mungu angekuwa ameumbwa, basi huyo aliyemuumba angekuwa "Mungu" zaidi yake, na mfululizo huo ungeendelea bila mwisho.
Nje ya Muda na Nafasi: Dini zinaeleza kuwa "kuumbwa" ni tendo linalohitaji muda na nafasi. Kwa kuwa Mungu anachukuliwa kama muasisi wa muda na nafasi, yeye yuko nje ya sheria hizo. Kwa hiyo, swali "aliumbwa na nani" halimtahini yeye kwa sababu yeye si kiumbe.
2. Mtazamo wa Kifalsafa na Mantiki
Wanafalsafa hutumia hoja ya Mstari wa Sababu (Infinite Regress):
Sababu ya Kwanza: Ili ulimwengu uwepo, lazima kuwe na kitu cha kwanza ambacho hakikuhitaji kusababishwa na kitu kingine. Kama kila kitu kingehitaji muumbaji, basi tusingekuwa na mwanzo kabisa, na ulimwengu usingekuwepo leo.
Hoja ya Aristoteli: Mwanahisabati na mwanafalsafa Aristoteli aliita dhana hii kama "Unmoved Mover" (Mwenye kusogeza asiyesogezwa). Ni nguvu au hulka ambayo ilianzisha kila kitu bila yenyewe kuanzishwa.
3. Mtazamo wa Kisayansi
Sayansi (kama Fizikia ya Quantum) mara nyingi haijibu swali la "Mungu," bali huangalia chanzo cha ulimwengu (kama vile Big Bang). Hata hivyo, changamoto inabaki pale pale: Nini kilisababisha Big Bang? Wanasayansi wengine wanahoji kuwa nishati au kanuni fulani za kifizikia zinaweza kuwa zilikuwepo daima.
Kimantiki, ikiwa Mungu aliumbwa, basi huyo aliyemuumba ndiye angekuwa Mungu wa kweli. Ili kuepuka mfululizo usio na mwisho wa waumbaji, hitimisho la kifikra ni kwamba lazima kuwe na asili ya kwanza ambayo haikuumbwa na yeyote—na hiyo asili ndiyo watu wanaiita "Mungu."
Ukishasema Mungu ni wa milele umesha contradict habari kwamba kila kilichopo kina muumba.
Ukisema Mungu ni special, yeye tu hahitaji muumba, hiyo ni special pleading logical fallacy.
Ukisema Mungu amekuwapo milele, swali linakuja, kama unasema Mungu kawepo milele, ushakubali kwamba kuwapo milele kunawezekana, sasa, kwa nini ulimwengu usiwe umekuwapo milele bila Mungu, haujaumbwa na Mungu? Ushakubali kuwapo milele kunawezekana. Sasa kwa nini ulimwengu usiweze kuwa umekuwapo milele na haujaumbwa na Mungu?
Maana katika hoja kubwa za kutetea uwepo wa Mungu ni kwamba Mungu ndiye kaumba ulimwengu.
Huoni kuwa ukishakubali kuwepo milele kunawezekana, hata kwa Mungu, unaondoa umuhimu wa Mungu kuwepo kama muumba ulimwengu, kwa sababu inawezekana ulimwengu ukawa ulikuwepo milele na haumuhitaji Mungu kuuumba?
2. Infinite regress haituoneshi kuwa Mungu lqzima awepo, inaonesha tu kuwa mambo hayawezi kurudi nyuma bila chanzo chabasiki. Chanzo cha asiki si lqzima kiwe Mungu, kusema hivyo ni logocal nonnsequitur fallacy. Kama ulimwengu umekuwapo milele bila kuhitaji muumba hapo hakutakuwapo na infinite regress wala Mungu.
Umekimbikia kusema ulimwengu umeumbwa na Mungu kabla hata ya kuonesha ulimwengu hauwezi kuwa umekuwapo tu milele.
3. Bog Bang haielezei chanzo cha ulimwengu inaelezea bdeakdown ya sayansi kueleea ulimwengu umeanza vipi katika singularity ambapo sayansi yetu ya Einsteinian Relativity na Quantum Physics haiwezi kujibu tunahitaji sayansi moya ya Quantum Gravity.
Zaidi, Big Bang inaelezea ulimwengu huu tu wakati kuna nadharia za multiverae zinazoelezea kuwa Big Bang na ulimwengu huu ni kioande kidogo tu katika multiverae iliyo na malimwengu mengine kama haya matrilioni na matrilioni yenye Bog Bang zake tofauti na sheria za fizikia zake tofauti. Nilikiwekea video post namba 27 lakini naona hujaiangakia na kama umeiangakia hujaielewa.
Ikiwa asili iliyoumba vyote ni ulimwengu ambao hauna muumbaji, ipo tu miele, utasema ulimwengu huo ndio Mungu?
Na utakubali kuwa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na uoendo wote hayupo?