Nikuulize, siku ya ibada mhubiri akienda na time bomu, akaset dakika 5 ili baada ya hapo lilipuke, akawaambia waumini likilipuka tu mtamuona MUNGU halafu yeye akakimbia, akirudi baada ya dakika 5 unadhani nini kitakuwa kimetokea?
Uwezekano ni kuwa, waumini wataachana na imani watatumia logic. Kwanini? Sababu utayari wa kufa unagusa Logic si imani pekee, so Mtasikilizana na anayekuhubiri iwapo ndani yako upo tayari kuamini sio kutumia Logic, kama ambavyo aliye tayari kufa atasubiri bomu lilipuke badala ya kutumia Logic.
Mkristo kukufata anatimiza matakwa ya kiimani ya kikristo sio matakwa ya Logic. Kwa mkristo kukuletea injili anatimiza takwa la kiimani bila kujali logic zako zinasema nini.
Mathayo 28:19–20 : “Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”