Ufafanuzi wa Kujadiliana na watu wasioamini uwepo wa Mungu

mfano wako uliotoa hauendani na kinachoelezwa naomba unitajie Honi na gari mfano wake ili ufananishe na tunachokizungumzia
Kuna Mungu aliyeumba viumbe na dunia.
Ukibisha hakuna Mungu inabidi utuambie dunia ilitengenezwa na nani?hiyo ndio maana ya mfano wangu
 
same old logical fallacy aliyekuambia kuwa Mungu ametengeneza Dunia ni nani na yeye aliambiwa na nani? tuanzie hapo halafun tutaendelea...

vipi nikikuambia mimi ndo nimetengeneza dunia utaamini??
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
"Natataka kujua kama yupo " hayupo, kama yupo thibitisha.

Hii sentensi mbona kama imejitosheleza mkuu?
Ok umesema unataka kujua na kama unataka kujua ili ujue vizuri hili swali lako muulize Atheist hivyohivyo mwambie hivi

"nataka kujua kama Mungu hayupo"
kama atatumia mantiki ya kusema Theist wamesema yupo ila hawajathibitisha. hiyo hoja ni finyu sana kusema hayupo. maana yake ni kua Atheist pia hawana uhakika kama hayupo.

Mnaamini hayupo
 
Hahahahahaha
umenikumbusha mbali sana kipindi nasoma Theology na kipindi nikiwa mwanatheolojia... kuna dhana moja inaitwa "God of the gaps" unaijua hii dhana? yaani ni kuamini kama unavyoamini wewe kwamba kwa kuna infinity cycle basi kuna filler of the gap cycle ambaye lazima awe ni mkubwa kuliko wote...katika moja ya logical fallcy kubwa ni hiyo sasa..kwamba lazima kuwe kuna devine intervation kwa mambo yote ambayo ubongo wetu umeshindwa kuyatatua..tunashindwa kuchosha ubongo...
ukimaliza kusoma God of the Gaps nenda katafakari kwa kusoma theory of desire yaani tusiamini kwenye vile tunavyohisi sisi ni sawa basi tunaamini mimi hata science siiamini kwa 100%

mimi huwa ninasemsa kila siku " Argumentum ad Ignorantiam" yaani Argument from Ignorance Hii ni kosa la kimantiki (logical fallacy) yaani Kwa sababu hatujui chanzo cha jambo hili, basi lazima chanzo chake kiwe fulani..

vipi kuhusu Big bangs

BIg bangs kwa mujibu wa science ndiyo chanzo cha universe chanzo cha Space ndo chance cha time so ni chanzo cha Time and space kwahyo hakukuwa na kabla endapo hakukuwa na space wala time..
when the singularity was there muda ulikuwa hauhesabiki hakukuwa na time wala hakukuwa na universe hakukuwa na chochote its just a singularity hakuna kabl;a hakuna zaidi ya baada..

na ushsahidi wa kisayansi wa Bigbang upo kasome kuhusu Redshift na Cosmic Microwave Background (CMB)....
na kwakuendelea kujibu swali lako The bigbang theory....
ina theory 3 maarufu kazisome zimeelezea vizuri sana nilichokieleza hapo juu..

1. Niliposema Muda haukuwepo katafute ( The "North Pole" Analogy)
2.Tafuta theory nyingine ("The Big Bounce")
3.Multiverse and the cosmic inflation theory of the bigbang

shukrani
Big bang naijua sana kiundani kabisa.

Je kitu gani kilisababisha BigBang
 
Ok umesema unataka kujua na kama unataka kujua ili ujue vizuri hili swali lako muulize Atheist hivyohivyo mwambie hivi

"nataka kujua kama Mungu hayupo"
kama atatumia mantiki ya kusema Theist wamesema yupo ila hawajathibitisha. hiyo hoja ni finyu sana kusema hayupo. maana yake ni kua Atheist pia hawana uhakika kama hayupo.

Mnaamini hayupo
Ulijaribu kujiweka tofauti na wanao amini kwenye dini ila bado umeingia kwenye mtego ule ule, kwa nini napaswa kuamini thibitisha uwepo wa Mungu.
 
sijasema unapaswa kuamini ila nimesema nawewe pia ukisema Mungu hayupo unaamini vilevile

ndo maana nilikwambia nitakuelewa ukisema hauna uhakika kama yupo au hayupo

unasema hayupo na huwezi kuthibitisha. hapo ni unaamini hayupo
 
Mungu hayupo kama yupo thibitisha ,mzigo wa kuthibitisha upo kwa anae toa madai

Kusema sina uhakika mimi sio Agnostic hivyo usitake kunipa label zako
 
kwaiyo nisipo thibitisha yupo, maana yake automatically "Hayupo" interesting
 
Kama unaijua Bigbang kiundani kabisa huwezi uliza swali hili la ki-Amateur kabisa
Hapana nijibu kwa faida ya wengi, na mimi pia hata kama najua bado kuna la kujifunza, wewe pia uliniuliza hiyo supreme power imetoka wapi ukaniambia mambo ya "God of the gaps"

nami nakuuliza Bigbang imesababishwa na nini
 
kwaiyo nisipo thibitisha yupo, maana yake automatically "Hayupo" interesting
Polisi : ndani kwako kuna bangi

Mtuhumiwa , ingia kagua ukiikuta nitie pingu

Polisi , siwezi kuthibitisha ila nina amini kuna bangi , na wewe thibitisha kama hakuna bangi

Swali kwa akili ya kawaida tu huyo police una ona ana akili timamu?
 
Hapana nijibu kwa faida ya wengi, na mimi pia hata kama najua bado kuna la kujifunza, wewe pia uliniuliza hiyo supreme power imetoka wapi ukaniambia mambo ya "God of the gaps"

nami nakuuliza Bigbang imesababishwa na nini
sasa kwa muktadha wa kielimu siwezi kukupa jibu la moja kwa moja kwa kuwa natamani upate maarifa..
nakuagiza kapitie hizi theory chini zina majibu mengi na ya ziada kuhusu swali lako..
  • Brane Cosmology theory
  • Cosmic Inflation theory
  • Quantum Fluctuation theory
zisome zote ukimaliza natamani uje na maswali sasa kwa ulichokisoma nitayajibu
 
Polisi : ndani kwako kuna bangi

Mtuhumiwa , ingia kagua ukiikuta nitie pingu

Polisi , siwezi kuthibitisha ila nina amini kuna bangi , na wewe thibitisha kama hakuna bangi

Swali kwa akili ya kawaida tu huyo police una ona ana akili timamu?
Mtabishana sana shubamiit.

Ni hivi, wewe ni nani? wewe ni electrons plus structure. Electrons zilikuwepo kabla yako, zitakuwepo baada yako, structure ambayo electrons zinaexist ndo temporary, ikifika mwisho ndo tunasema umekufa, sasa hoja ya uwepo wa MUNGU inaexist kwenye ufahamu, swali linakuja, ufahamu unaexist kwenye electrons au structure? Hapa si wazee wa logic wala wazee wa imani wana hili jibu, na mtabishana mpaka structure inayohifadhi electrons itakapoharibika.
 
Polisi : ndani kwako kuna bangi

Mtuhumiwa , ingia kagua ukiikuta nitie pingu

Polisi , siwezi kuthibitisha ila nina amini kuna bangi , na wewe thibitisha kama hakuna bangi

Swali kwa akili ya kawaida tu huyo police una ona ana akili timamu?
huu mfano umeuweka juu chini.

Theist anaona dunia ulimwengu na complexity yote kutokea DNA hadi tabia za viumbe mbalimbali

simu ipo barabarani
Atheist mind: Hii simu ilikwepo tu hapa haijawai kutengenezwa kiwandani wala kununuliwa ( thibitisha kama ilitengenezwa )

theist asipothibitisha ( maana yake simu ilikwepo tu hapo )

hii ndo mantiki yako
 
Mungu yupi Kaumba Dunia na ulimwengu?

Usije sema tuu Mungu ni Mmoja. Kwa sababu hapo utakuwa umejichanganya zaidi kuliko Yule asiyeamini kabisa kama Mungu au miungu ipo
Wewe ni unaamini Mungu huamini Mungu.

Ebu tuambia who are you maana,unanichanganyaga sana kwenye hii mijadala.
 
sasa kwa muktadha wa kielimu siwezi kukupa jibu la moja kwa moja kwa kuwa natamani upate maarifa..
nakuagiza kapitie hizi theory chini zina majibu mengi na ya ziada kuhusu swali lako..
  • Brane Cosmology theory
  • Cosmic Inflation theory
  • Quantum Fluctuation theory
zisome zote ukimaliza natamani uje na maswali sasa kwa ulichokisoma nitayajibu
doctor naimba utujibu hapa si moaka tukaanze kusoma mitandao ndo elimu hivyyo utuambie tena kwa upole kabisa

fanya kama unamuelekeza mtito wa darasa la 2, hata kwa mifano. imagine kila moja anaekuja hapa aende kwanza akasome hivyo vitu
 
same old logical fallacy aliyekuambia kuwa Mungu ametengeneza Dunia ni nani na yeye aliambiwa na nani? tuanzie hapo halafun tutaendelea...

vipi nikikuambia mimi ndo nimetengeneza dunia utaamini??
Ok, nikuulize, kwanini nisiamini kwamba umeumba dunia? Nini kinazuia nisiamini kwamba hujaumba dunia iwapo imani yangu inakubali kwamba umeumba dunia? Suala la usahihi wa anachoamini mtu sio suala la logic, ni suala la imani. Ndo maana muislamu hawi mkristo kwa sayansi, anakuwa mkristo kwa mahubiri ya kiimani.

Watu msio amini MUNGU huwa mnashangaza sehemu moja tu, mnashindwa kuja na Logic ya kufuta sababu ya uwepo wa imani ya uwepo wa MUNGU. Huwa mnategemea udhaifu wa waamini kufinalise kuwa hakuna MUNGU ilihali waamini MUNGU hawaamini kwa logic.

Mfano 1. Swali lako " aliyekuambia kuwa Mungu ametengeneza Dunia ni nani na yeye aliumbwa na nani" Hili ni swali ambalo lina logic, na majibu yake lazima yawe yenye logic, sasa unalielekeza kwenye faith, ukitegemea ujibiwe logic. Hapa ndipo udhaifu ulipo.

Mfano 2. "Vipi nikikuambia mimi ndo nimetengeneza dunia utaamini?" Hili ni swali la kiimani, haliitaji logic kujibiwa lakini unalielekeza kwenye logic. Udhaifu mwingine.
 
huu mfano umeuweka juu chini.

Theist anaona dunia ulimwengu na complexity yote kutokea DNA hadi tabia za viumbe mbalimbali

simu ipo barabarani
Atheist mind: Hii simu ilikwepo tu hapa haijawai kutengenezwa kiwandani wala kununuliwa ( thibitisha kama ilitengenezwa )

theist asipothibitisha ( maana yake simu ilikwepo tu hapo )

hii ndo mantiki yako
Tusiende mbali sana sana yeye Mungu unaemdai katengezwa na nani?
 
Ok, nikuulize, kwanini nisiamini kwamba umeumba dunia? Nini kinazuia nisiamini kwamba hujaumba dunia iwapo imani yangu inakubali kwamba umeumba dunia? Suala la usahihi wa anachoamini mtu sio suala la logic, ni suala la imani. Ndo maana muislamu hawi mkristo kwa sayansi, anakuwa mkristo kwa mahubiri ya kiimani.

Watu msio amini MUNGU huwa mnashangaza sehemu moja tu, mnashindwa kuja na Logic ya kufuta sababu ya uwepo wa imani ya uwepo wa MUNGU. Huwa mnategemea udhaifu wa waamini kufinalise kuwa hakuna MUNGU ilihali waamini MUNGU hawaamini kwa logic.

Mfano 1. Swali lako " aliyekuambia kuwa Mungu ametengeneza Dunia ni nani na yeye aliumbwa na nani" Hili ni swali ambalo lina logic, na majibu yake lazima yawe yenye logic, sasa unalielekeza kwenye faith, ukitegemea ujibiwe logic. Hapa ndipo udhaifu ulipo.

Mfano 2. "Vipi nikikuambia mimi ndo nimetengeneza dunia utaamini?" Hili ni swali la kiimani, haliitaji logic kujibiwa lakini unalielekeza kwenye logic. Udhaifu mwingine.
Udhaifu upo kwa watu wa imani hakuna Atheist hata mmoja anahubiri imani kwenye logic ila kuna maelfu na makumi elfu ya theist wanahubiri imani kama logic , wanatumia vitisho na ahadi ili kupumbaza wanaotaka kuhoji
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom