Ufafanuzi wa Kujadiliana na watu wasioamini uwepo wa Mungu

Yani wewe
Sasa unataka kujadili Mungu na wasioamini Mungu, wakati hata wasio amini Mungu hawazidi 100 humu ila wanao amini Mungu wapo zaidi ya laki na bado wanapingana Mungu yupi ni sahihi🤔
 
Tutaendelea tu kuuliza na kuhoji ila kamwe hauta nikuta kanisani au msikitini nikihoji
Unakumbuka kabla ya ujio wa internet watu walidhani ujinga ni sababu ya kukosa taarifa?
 
Sasa unataka kujadili Mungu na wasioamini Mungu, wakati hata wasio amini Mungu hawazidi 100 humu ila wanao amini Mungu wapo zaidi ya laki na bado wanapingana Mungu yupi ni sahihi🤔
Nimekushindwa 😅
 
Unakumbuka kabla ya ujio wa internet watu walidhani ujinga ni sababu ya kukosa taarifa?
Africa bado sana kuna wengi tu hata hawajui matumizi ya Internet
 
Reactions: Tsh
Yaaa sana tu
Nikushauri kitu , kama unataka kubaki na imani yako kwa amani,usisome majadiliano ya atheists mahali popote pale .

Kwa sababu unaweza soma ndio na kusiwe na shida ila akili automatically tu haijawahi kutulia pale inapodanganywa na kuupata ukweli ila kwa makusudi kabisa , ikagoma kuupokea kwa kulinda imani.

Kinachofanyika sasa ni defence mechanism ya ubongo ila kuukataa ukweli na kulinda imani.

Hivyo achana kabisa kusoma hoja za atheists , ukienda reddit, qoura , jf , x na popote pale, kama unataka kuilinda imani.
 
Niliuliza maswali mawili
1. Kila kitu kiliumbwa, Mungu aliumbwa na nani?
2. Na kama dunia imeumbwa una uhakika gani aliyeiumba ni mmoja?
 
Sawa nitazingatia. Asante
 
umewahi kufanya research yoyote ya archaeology?
ok nitajibu hoja zako kwa ustaarabu sana ndugu yangu!
na nitajibu kwa maneno mengi ili uelewe tafadhali bear with me usichoke kusma..

1. Muundo wa Kikemia (Chemical Composition)
Ni kweli kabisa na sikatai kwamba mwili wa binadamu una elementi kama oksijeni, kaboni, hidrojeni na nitrojeni, na hizi pia zinapatikana ardhini. Lakini kufanana kwa elementi hakuthibitishi chanzo cha uumbaji.
kwanini?
Hizi elementi hazipo kwenye udongo tu zipo pia kwenye hewa, maji, na hata kwenye nyota. Hivyo, huwezi kuchagua udongo kama chanzo pekee yake na ukahitimisha..kwanini usiseme binadamu katokana na Maji (kama wanavyosema wale wnaoamini kwenye ANUNAKI au kwanini usiseme katokana na upepo?

sasa hiyo sio justfication Zaidi ya hapo, kujua kitu kimeundwa na nini (composition) si sawa na kujua kimetoka wapi (origin). Hii ni kama kuchambua gari ukapata chuma, halafu useme limetokana na udongo hapo unachanganya material na source ya uumbaji...
kwa kumbukumbu zangu Wanyama na mimea pia na wenyewe wana composition sawa kabisa na hizo za binadamu na kwa bahati mbaya kabisa Mnyama hakuumbwa kwa udongo (kulingana na maandiko matakatifu)..

sasa hii hoja yako inaonyesha nini inaonyesha Hoja hii inaonyesha material similarity, si proof ya creation.
kwa hii hoja hata kama ungelichukua kiumbe chochote hata kama ungeleta kiumbe kutoka sehemu nyingine kama sayari ya Mars akikaa duniani, atalazimika kuvuta hewa yenye nitrogen na oksijeni, na atakula mimea au wanyama wanaotegemea udongo.

Matokeo yake, mwili wake utaanza kuwa na hizi hizi elementi zinazopatikana duniani. Lakini hiyo haitamaanisha kwamba chanzo chake ni udongo bali inaonyesha tu kwamba mazingira anayokaa yanaathiri muundo wa mwili wake.

Kwa hiyo, hoja ya kwamba binadamu ni udongo kwa sababu ya hizi elementi haijathibitisha, bali inaonyesha tu kwamba binadamu anaishi ndani ya mfumo wa dunia unaompatia elementi hizo.

ngoja nikuongezee na kitu kimoja (chanzo cha kukuuliza kama umewahi kufanya archeology study yoyote)
Hivi unajua kuwa composition (muundo wa kikemia na kibaolojia) ya miili ya viumbe hai, ikiwemo binadamu mwenyewe , inaweza kubadilika na imekuwa ikibadilika kulingana na era (zama) na miaka.

Mabadiliko haya hayatokei kwa sababu elementi hizo zimeumbwa au ni udongo bali yanatokea kwa sababu ya mabadiliko katika mazingira, lishe, na teknolojia. Hapa kuna namna mbalimbali ambazo muundo wetu unabadilika,na nikuambie tu sasa hivi kuna Mabadiliko ya Kikemia (Chemical/Isotopic Signatures)ya binadamu ambayo zamani ilikuwa haipo kwahyo unataka kuniambia kuwa Mungu alibadilisha Udongo?? kwa zaman hizi?? Miili ya binadamu wa sasa ulisahau kuwa pia ina kiasi kikubwa cha elementi kama Strontium au Lead (Risasi) kutokana na uchafuzi wa mazingira na matumizi ya nishati ya fossil fuels
vipi na yenyewe tuseme kuwa mungu amebadili udongo...

sasa naomba hii niiweke kwa Rangi nyekundu kwenye hoja hii kuu ya kwako..
unafahamu kuwa Kuna
Microplastics na Kemikali Nyingine ambazo kwenye miili zamani haikuwepo ila sasa hivi ipo? wanasayansi wanaita Modern Composition
Hii ni pointi ya kipekee kwa era yetu au tunaiita The Anthropocene, Katika miaka 50 iliyopita, muundo wa mwili wa binadamu umeanza kuwa na vitu ambavyo havikuwepo kabisa katika era za nyuma tafiti za hivi karibuni zimegusa damu, mapafu, na hata kondo la nyuma (placenta) la binadamu zikionyesha chembechembe ndogo za plastiki, vipi sasa tuamini pia kwamba Mungu aliumba kwa kutumia plastic vizazi vya sasa hivi na udongo vya zamani??
Miili yetu sasa ina vitu kama PFAS ambavyo mababu zetu hawakuwa navyo. Hii ina maana "udongo" tunaokula sasa hivi kupitia chakula umechafuliwa, hivyo "composition" yetu inabadilika na inazidi kubadilika..

nadhani kwa hoja hii umenielewa hakuna justification ya uumbaji kwa just elements tu kuonekana...

2. Mzunguko wa Chakula (Food Chain)​

Ni kweli kwamba chakula tunachokula kina asili ya udongo kupitia mimea, lakini hii inaonyesha utegemezi wa mazingira (dependence), si chanzo cha uumbaji.

Kiumbe chochote kinachoishi duniani hata kama kingetoka sehemu nyingine kitalazimika kula kutoka kwenye mfumo huu huu wa chakula. Matokeo yake kitapata hizi hizi elementi mwilini.

Hivyo, uwepo wa elementi hizo mwilini unaonyesha tu kwamba tunaishi kwenye mfumo wa dunia, si kwamba tumetokana na udongo. na kula chakula hata ukitoka mars lazima utakula miili imeumwwa kwa ajili ya kupata nguvu na nishati kutoka kwenye chakula..

Samaki anaishi kwenye maji na mwili wake umejaa maji, lakini hatusemi “ametengenezwa na maji.”

kwahiyo Hoja hii yako ya pili inaonyesha nutritional cycle, si creation process.
hoja zingine nitazijibu kwa pamoja

Kuhusu mwili wa binadamu kuwa na maji mengi ni kwamba mwili unahitaji unahitaji electrolytes ili kufanya kazi, na hii ni sehemu ya physiology (jinsi mwili unavyofanya kazi), si ushahidi wa chanzo chake.

Maji na madini ni vitu vya msingi vinavyopatikana katika mazingira yote ya dunia. Hivyo, kuvitumia hakuthibitishi umetokana na udongo inaonyesha tu umeadapt kwenye mazingira ya dunia.

Ni kweli mwili hurudi katika elementi zake za msingi baada ya kifo, lakini kurudi kwenye kitu si uthibitisho kwamba ndipo ulikotoka mwanzo.

Huu ni mzunguko wa asili (natural cycle), si ushahidi wa chanzo.

Mfano: ukichoma karatasi inakuwa majivu, lakini hatusemi karatasi ilitoka kwenye majivu.

Vivyo hivyo, mwili kurudi udongoni haimaanishi kwamba ndipo ulikotoka inaonyesha tu kwamba unaingia kwenye mzunguko wa mazingira baada ya kifo.

natumaini nimejibu Hoja zako
 
1. Kuna uthibitisho gani usio wa kisayansi? Hiyo dhana nzima ya kwamba uwepo wa Mungu upo nje ya mfumo wa jisayansi ni chaka la kupitisha uongo wowote.

Hata mimi naweza kukuambia mimi ni Mungu, ila huwezi kujua hilo kwa sababu uthibitisho wake upo nje ya mifumo ya kisayansi.

Utapingaje?

Huoni kuwa dhana nzima ya uthibitisho ni sehemu ya sayansi?

Huoni kuwa hoja ya "uthibitisho wake upo nje ya mifumo ya kisayansi" inaweza kupitisha uongo wowote?

2. Kama mimi sipendi kuumizwa na kuuawa, kuumizwa na kuuawa ni jambo baya kwangu. Kwa nini nimhitaji Mungu ili maumivu na mimi kunyimwa haki ya kuishi, kufurahia maisha na wenzangu kuwa ni jambo baya?

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kutojithibitisha wazi kiasi watu wanapigana vita za kidini kwa kuamini Mungu tofauti ni ukatili. Angeweza kujithibitisha kiasi cha kuondoa utata, lakini si kiasi cha kutisha.

Kwa nini hakufanya hivyo?

Mungu mwenye upendo wote kuachia utata utawale kiasi watu wameuana kwa mamilioni ni ukatili.

Mungu mwenye upendo wote kuwa pia mkatili hivyo ni contradiction.

Contradiction hii inaonesha Mungu huyo hayupo, katungwa na watu tu.

Hivyo, ukiona mjadala wa kujadili uwepo wa Mungu ni ushahidi kuwa Mungu hayupo.

Angekuwapo, tusingeweza hata kujadili uwepo wake, kila mtu angejua yupo kwa hakika.
 
1. Wewe mwenyewe unaamini mambo mengi ambayo hayathibitishwi kwa sayansi. Unaamini kwamba maumivu ni mabaya sayansi haiwezi kuthibitisha hilo. Unaamini kwamba ukatili ni mbaya sayansi haiwezi kuthibitisha hilo. Hizi ni imani za kimantiki na kimaadili na hisia za mmwili wako si za kisayansi. Kwa hiyo mfumo wako mwenyewe una mambo yanayokwepa sayansi. unaamini Julius Caesar alikwepo na vitu vinavyofanana na hivi ingawa haviwezi kuthibitishwa kisayansi

2.Unasema kuumizwa ni mbaya kwako nakubaliana nalo. lakini Problem of Evil haizungumzii preference yako au mapendelo yako binafsi. Inazungumzia madai ya maadili ya ulimwengu wote kwamba ukatili ni mbaya kwa kila mtu, wakati wote, mahali pote. Preference yako ya kibinafsi haifikii hapo. kuna mtu anapenda kuumiza wengine ana preference yake pia na nikitu kinachomfurahisha kwaiyo kwake ni kiziri preference yake ni halali sawa sawa na yako. Kwa nini yako ni sahihi zaidi?

3.Unasema vita za kidini ni ushahidi wa ukatili wa Mungu. lakini vita za kidini zimefanywa na binadamu si Mungu. Binadamu wamechukua jina la Mungu na kutumia kwa maslahi ya nguvu, siasa, na ubinafsi. Kulaumu Mungu kwa matendo ya binadamu wanaotumia jina lake vibaya ni kama kulaumu Einstein kwa silaha za nyuklia aliandika equations, watu wengine walichagua kuzitumia vibaya. au kumlaumu mtu aliyetengeneza kisu kwasababu kuna watu wanauawa kwa kuchomwa visi

pia una logical fallacy inayoitwa Argument from Ignorance kusema kwa sababu hatujui kwa uhakika, kitu hakipo. Lakini ukweli wa kitu hautegemei uelewa wetu wa kitu hicho. Kwa maelfu ya miaka binadamu hawakujua vijidudubkama bakteria vipo je, vijidudu havikuwepo? Hawakujua galaxies nyingine zipo je, hazikuwepo? Kutojua au kutokubaliana juu ya kitu hakuthibitishi kitu hicho hakipo.

Unasema Mungu angekuwepo, mjadala usingekwepo. lakini hata kama Mungu yupo na anajithibitisha binadamu bado wangeweza kukataa. Hii si nadharia binadamu wanakataga ushahidi wa kisayansi ulio wazi kila siku. Watu wanaamini dunia ni flat licha ya ushahidi wote. Kwa hiyo hata ushahidi wazi haumalizi mjadala kwa sababu tatizo si ushahidi, tatizo ni binadamu na uhuru wao wa kukataa.

poa kwakonaona pattern moja katika hoja zako zote: unabeba mzigo mkubwa wa assumptions ambazo wewe mwenyewe hujazithibitisha kwamba maadili yanaweza kuwepo bila msingi wa nje ya binadamu, kwamba Mungu mwenye upendo lazima aondoe matokeo yote ya uhuru, kwamba uthibitisho wote lazima uwe wa kisayansi. Kila assumption hiyo yenyewe inahitaji mjadala mrefu.

Kwanini wewe umejiamulia ku assume hivyo ?
 
1. Hujaelewa hoja. Hoja si mimi naamini au siamini nini. That is irrelevant. Logical non sequitur fallacy. Mimi naweza kuamini mambo yasiyothibitishika kisayansi. Ya uongo kabisa. Sijawahi kusema sina makosa.

Lakini kama njia ya uhakika kujua kitu kipo kweli au hakipo ni uthibitisho wa kisayansi, bila uthibitisho wa kisayansi hujaonesha kuwa kitu hicho kipo kweli.

Zaidi, hujathibitisha Mungu yupo kwa namna yoyote, kisayansi, au vinginevyo.

Na zaidi, falsafa ya uthibitisho ni ya kisayansi, kitendo cha kupima tu kama jambo ni kweli au si kweli, hata kwa kutumia pure logic, ni scientific thinking.

Sasa utathibitishaje chochote bila kupima kama kitu ni kweli au si kweli? Na ukishaanza kupima tu, how is that not of the scientific process?

Utathibitisha kwa kukisia tu?

2. Hujaelewa hoja. The problem of evil haizungumzii preference yangu na mimi nikizungumzia the problem of evil sizungumzii preference yangu. Problem of evil inazungumzia internal contradiction katika hoja ya kuwepo Mungu. H9ja zenu wenyewe katika kumuelezea na kutetea uwepo w aNungu, tukizilinganisha na ulimwengu ulivyo, tunaona contradictions. Bila kuweka tunachotaka sisi.

Kwa nini Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea wakati logical consistency inatuambia kuwa Mungu huyu angekuwa logically consistent kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani, kwa sababu ana uwezo, ujuzi na upendo wa kufanya hivyo (kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani), na kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kuna contradict upendo wake?

Hapo hakuna preference yangu.

Story yenu inasema Mungu kasema anaenda kulia, halafu tukiangalia dunia tunaona huo uumbaji mnaosema ni wa Mungu unatuonesha, kama Mungu yupo, Mungu kakata kona kushoto badala ya kwenda kulia kama mnavyosema aliosema.

Mimi nikiuliza mbona hapa tunaona dunia inayotuonesha Mungu kakata kushoto badala ya kwenda kulia kama alivyosema kwenye stories zenu, utasema mimi naweka preference yangu ya kulazimisha Mungu aende kulia?

Mngesema Mungu ni mkatili anapenda kuua watu ovyo ningeona dunia hii iliyopo ni sawa tu, haija m contradict Mungu huyo, kwa sababu ipo logically consistent na dunia iliyoumbwa na Mungu mkatili anayependa kuua watu ovyo.

Lakini kati ya hadithi ya Mungu wenu mwenye upendo wote na dunia tunayoiona tunaona kuna contradiction, kuna logical inconsistency, sasa kwa nini tuki point out contradiction hiyo mnasema tunataka preference yetu wakati sisi si tuliosema Mungu ana upendo wote?

3. Hujaelewa hoja. Unaposema vita vya kidini zimefanywa na binadamu na si Mungu, lakini Mungu ndiye aliyeumba dunia ambayo vita vya kidini vinaweza kufanyika.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hakuumba dunia ambayo vita vya kidini haviwezi kufanyika, kwa mfano kwa kuwapa watu wote uelewa mzuri kuhusu Mungu ni nani, kiasi kusiwezekane kuwapo na utata wowote kuhusu Mungu wa kweli ni nani, na vita ya kidini isiwezekane kuwapo?

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hajaumba dunia hivyo, kwa nini hajajidhihirisha wazi kwa watu wote kiasi tusiwe hata na haja ya kubishana kama Mungu yupo au hayupo, na kama yupo ni yupi? Maana hapa hata mnaoamini Mungu yupo hamkubaliani ni yupi.

Sina argument from ignorance kwa kusema kwa sababu hatujui kwa uhakika Mungu hayupo.

Nakuonesha kuwa problem of evil ina contradiction inayotuonesha kuwa Mungu hayupo.

Argument kwamba kila kilichopo kinahitaji kuwa na muumba inatuonesha Mungu muumba vyote hawezi kuwapo.

Hoja kwamba Mungu kaumba ulimwengu wakati hamjaweza kuthibitisha kuwa ulimwengu umeumbwa na haujakuwepo milele ni logical non sequitur fallacy.

Hoja ya kuuliza kama tunaweza kuwa na maadili bila Mungu kuwapo wakati hujathibitisha Mungu yupo ni circular reasoning.

Thibitisha Mungu yupo kwanza, kabla hujathibitisha mimi nakuambia hizo moral systems zote zilizopo ni za watu tu, hata zinazosemwa zimetoka kwa Mungu ni watu wameziweka tu na kuzipa utukufu wa Mungu asiyepo, kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.

Hoja nyingi mnazozileta kuonesha Mungu yupo zimejengwa katika ujinga wa kuchambua mambo kimantiki tu.
 
Kwa asilimia kubwa umejibu hoja zangu,usijali kuhusu maandiko marefu huwa hayanipi shida huenda kwasababu kusoma ni sehemu ya hobby yangu

Pamoja na maelezo mazuri ambayo yamejibu hoja zangu,kuna sehemu nataka kukuchallenge.

Katika hoja yako ya mwili wa binadamu sasa kuwa na elements ambazo hazikuwepo miaka kadhaa nyuma ikiwemo plastics na element nyingine ambazo umezitaja sina haja ya kuzirudia hapa

Umenichallenge kwa kusema je,Mungu atakuwa amebadilisha udongo katika uumbaji? Sasa hoja yako au maelezo yako yangekuwa na uzito kama bado mpaka leo hii tungekuwa tumeumbwa au kutokana na udongo,kwa maana ya kwamba kungekuwa hakuna kuzaliana na sote tungeumbwa kwa udongo hapo sasa ndio tungejiuliza je,udongo umebadilishwa?

Kwahiyo utaona kwamba kama hoja ya binadamu ametokana na udongo ni sahihi,basi tutasema udongo wa mwanzo ndio ambao tunaupa kipaumbele,kwasababu kizazi kilichofuatia kimetokana na maji kwahiyo ni sahihi kizazi kuwa na element ambazo huko nyuma hazikuwepo,na hii ni kutokana na mabadiliko ya mazingira na mwanadamu kuwa exposed na mambo mbalimbali katika zama hizi
 
Niliuliza maswali mawili
1. Kila kitu kiliumbwa, Mungu aliumbwa na nani?

1. Mtazamo wa Kidini (Theolojia)
Katika imani nyingi za kidini (kama Uislamu na Ukristo), sifa kuu ya Mungu ni kwamba yeye ni wa milele—hana mwanzo wala mwisho.

Mungu kama Chanzo: Imani hizi zinafundisha kuwa kila kitu kilichopo kiliumbwa, lakini lazima kuwe na "Chanzo kisichochimbika" (Uncaused Cause). Ikiwa Mungu angekuwa ameumbwa, basi huyo aliyemuumba angekuwa "Mungu" zaidi yake, na mfululizo huo ungeendelea bila mwisho.

Nje ya Muda na Nafasi: Dini zinaeleza kuwa "kuumbwa" ni tendo linalohitaji muda na nafasi. Kwa kuwa Mungu anachukuliwa kama muasisi wa muda na nafasi, yeye yuko nje ya sheria hizo. Kwa hiyo, swali "aliumbwa na nani" halimtahini yeye kwa sababu yeye si kiumbe.

2. Mtazamo wa Kifalsafa na Mantiki
Wanafalsafa hutumia hoja ya Mstari wa Sababu (Infinite Regress):
Sababu ya Kwanza: Ili ulimwengu uwepo, lazima kuwe na kitu cha kwanza ambacho hakikuhitaji kusababishwa na kitu kingine. Kama kila kitu kingehitaji muumbaji, basi tusingekuwa na mwanzo kabisa, na ulimwengu usingekuwepo leo.

Hoja ya Aristoteli: Mwanahisabati na mwanafalsafa Aristoteli aliita dhana hii kama "Unmoved Mover" (Mwenye kusogeza asiyesogezwa). Ni nguvu au hulka ambayo ilianzisha kila kitu bila yenyewe kuanzishwa.

3. Mtazamo wa Kisayansi
Sayansi (kama Fizikia ya Quantum) mara nyingi haijibu swali la "Mungu," bali huangalia chanzo cha ulimwengu (kama vile Big Bang). Hata hivyo, changamoto inabaki pale pale: Nini kilisababisha Big Bang? Wanasayansi wengine wanahoji kuwa nishati au kanuni fulani za kifizikia zinaweza kuwa zilikuwepo daima.

Kimantiki, ikiwa Mungu aliumbwa, basi huyo aliyemuumba ndiye angekuwa Mungu wa kweli. Ili kuepuka mfululizo usio na mwisho wa waumbaji, hitimisho la kifikra ni kwamba lazima kuwe na asili ya kwanza ambayo haikuumbwa na yeyote—na hiyo asili ndiyo watu wanaiita "Mungu."
 
2. Na kama dunia imeumbwa una uhakika gani aliyeiumba ni mmoja?
1. Uwiano na Umoja wa Kanuni za Asili (The Argument from Design)
Wataalamu wengi wa fizikia na falsafa huashiria kuwa ulimwengu unafuata kanuni zilezile za kifizikia kila mahali.
Sheria ya Maumbile: Sheria ya uvutano (F = G \frac{m_1 m_2}{r^2}) au kasi ya mwanga ni thabiti iwe uko hapa duniani au kwenye galaksi ya mbali.

Mantiki: Kama kukiwa na waumbaji wengi wenye mamlaka sawa, kungekuwa na "migongano ya kikanuni." Uwepo wa mfumo mmoja unaotegemeana (ecosystem) unaashiria mpango kutoka chanzo kimoja.

2. Hoja ya Mantiki ya "Mamlaka Kamili"
Katika falsafa ya kidini (kama vile kazi za Thomas Aquinas au Ibn Sina), kuna hoja kuwa muumba lazima awe na mamlaka yasiyo na kikomo.
Ikiwa wangekuwa wawili, na mmoja akitaka jambo fulani litokee (mfano: jua lichomoze) na mwingine akakataa, basi mmoja lazima ashindwe.
Yule aliyeshindwa hawezi kuitwa "Mungu" au "Muumba Kamili" kwa sababu ana udhaifu. Ili kuwe na utaratibu usio na vurugu, lazima kuwe na utashi mmoja mkuu.

3. Kanuni ya "Occam's Razor"
Hii ni kanuni ya kisayansi na kifalsafa inayosema: "Maelezo rahisi zaidi yenye kudhania mambo machache ndiyo yanayoelekea kuwa ya kweli."
Ili kuelezea asili ya ulimwengu, kudhania kuwepo kwa chanzo kimoja (Singularity au Muumba mmoja) ni rahisi na haina utata mwingi kuliko kudhania kundi la waumbaji, jambo ambalo lingehitaji maelezo zaidi ya jinsi wanavyoelewana, wanavyogawana majukumu, na asili yao.

4. Mitazamo Tofauti
Ni muhimu kukumbuka kuwa si kila mtu anakubaliana na dhana hii:
Washirikina (Polytheists): Kihistoria, baadhi ya tamaduni ziliamini miungu wengi wakigawana majukumu (mungu wa bahari, mungu wa anga, n.k.).
Wana-agnostiki/Wana-atheist: Wao huhoji kuwa ulimwengu unaweza kuwa ulitokana na michakato ya kifizikia isiyohitaji "mtu" au "utashi" wa kuumba, bali ni matokeo ya mabadiliko ya nishati na mata kwa mabilioni ya miaka.

Uhakika wa kuwa muumba ni mmoja unajengwa zaidi juu ya utaratibu thabiti (order) wa ulimwengu. Ikiwa ulimwengu ungekuwa na fujo au sheria zinazobadilika-badilika bila mpangilio, hapo ndipo kusingekuwa na uhakika wa chanzo kimoja.
 
Got it, Mungu hakuumbwa
Kwa hiyo sio lazima kila kitu kiumbwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…