Sulayman Sangida
Member
- Feb 5, 2018
- 91
- 51
[emoji256] *BAWASIRI/MGOLO* [emoji256]Habar wana JF, kwanza kabisa nipende kuwa julia hali za mwaka huu mpya wa 2018, wengine hatujawah post. .thread yoyote toka mwaka uanze.
Somo ni kama kichwa cha habari hapo [emoji121] kinavyoeleza. Kuna jambo linaendelea kwenye mwili wangu linanitatiza kidogo. Kuna kauvimbe mfano wa jibu kwenye sehemu ya haja kubwa (puru)..na mapata maumivu kiasi wakati wa kwenda haja kubwa...hali hii imekuwa ikija na kupotea. .ila awamu hii naona kimekuwa kikubwa zaid na maumivu kuongezeka. Katika utafiti wangu mdogo nimehisi inawezekana nina matatizo ya ugonjwa ujulikanao kama BAWASIRI. .Ila kilichonifanya mpaka niingie JF kuomba ushauri kabla ya kwenda hospital, kwanza najiuliza kwanini uvimbe huu huja na kupotea? Na, je nimesoma vizur sababu za kupata ugonjwa huu ikiwa km umri. .miaka 50+ , kuzidi kwa uzito wa mwili (Obesity), Kufanya kazi inayokufanya kukaa mda mrefu bila kushughulisha mwili n.K, Lakini vyote hvy hakuna kinachonisibu, Je endapo nitabainika kuwa na tatizo tiba yake ikoje? Maana hp ninauwoga wa hari ya juu..naona aibu hata kumweleza mtu wangu wa karibu tatizo hili. Tafadhali nahutaj msaada wenu wa dhati sina raha tangu hali hii ianze kunisumbua.
Naomba kuwasilisha
[emoji298]Bawasiri ni ugonjwa unaotokea katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje.
[emoji298]Kwa kiingereza hujuliakana kama piles.
[emoji298] Na kitaalam hujulikana kama hemorrhoids
[emoji261]AINA ZA BAWASIRI[emoji261]
[emoji117]1⃣ BAWASIRI YA NJE
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina hii ya bawasiri kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.
[emoji117]2⃣BAWASIRI YA NDANI
Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu.
[emoji298]Aina hii imeainishwa katika mainisho ya madaraja manne yafuatayo:
[emoji117]Daraja la 1 - Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
[emoji117]Daraja la 2 - Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya haja.
[emoji117]Daraja la 3 - Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya haja.
[emoji117]Daraja la 4 - Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya haja.
www.sangidaherbal.blogspot.com
[emoji271]BAWASIRI HUSABABISHWA NA NINI?[emoji271]
[emoji117]Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu
[emoji117]Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa
[emoji117]Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile
[emoji117]Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu
[emoji117]Sababu za kurithi – baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni asilimia ndogo sana.
[emoji117]Kuharisha sana kwa muda mrefu
[emoji117]Kutumia vyoo vya kukaa
[emoji117]Kunyanyua vyuma vizito
[emoji117]Mfadhaiko/stress
[emoji117]Uzito na unene kupita kiasi.
[emoji271]DALILI ZA BAWASIRI[emoji271]
[emoji117]Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
[emoji117]Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia
[emoji117]Muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa
[emoji117]Uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa
[emoji117]Haja kubwa yaweza kujitokea tu muda wowote
[emoji263]ATHARI ZA BAWASIRI[emoji263]
[emoji298] Upungufu wa damu mwilini
[emoji298] Kutokwa na kinyesi bila kijitambua
[emoji298]Kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa
[emoji298]Kupungukia nguvu za kiume (kwa wanaume)
[emoji298]Kupungukiwa na uwezo wa kufanya kazi kutokana na maumivu
[emoji298]Kupata tatizo la kisaikolojia
[emoji263]NJIA ZA KUJIKINGA DHIDI YA BAWASIRI[emoji263]
[emoji298]Kula mboga za majani na nafaka zisizo kobolewa kwa wingi
[emoji298]Kunywa maji mengi lita sita hadi kumi na mbili kwa siku
[emoji298] Acha kufanya ngono kwa kutumia tundu la haja kubwa (kulawitiwa)
[emoji298] Punguza kukaa chooni kwa muda mrefu, kunaweza kuongeza shinikizo katika njia ya haja kubwa.
[emoji259]DAWA YA KUTIBU UGONJWA WA BAWASIRI [emoji259]
NB:: Kabla ya kutumia dawa hizi pata ushauri kwa wataalam kulingana na aina ya bawasiri uliyonayo.
[emoji117][emoji267]Chukua dawa inayoitwa NTOBOTOBO kisha kamua na maji yake uyaweke kwa kiti cha kienyeji kisha mgojwa ayakalie yapate kuingia vizuri sehemu ya nyuma kwa Muda usiopungua lisaa limoja ni mujarabu sana dawa hyo
Pia mizizi yake ni mujarabu kwa kuchemsha na unywe kikombe kimoja kutwa mara Tatu in shaa Allah utapona kabisa
[emoji117][emoji267]Chemsha MAKAL-ARZAK 100gm, kwa maji lita moja na nusu kunywa nusu kikombe kutwa mara tatu, na uwe unapakaa mafuta ya mbono hukooo sehemu ya nyuma.
Kwa ushauri na dawa za magonjwa mbalimbali wasiliana nami
www.sangidaherbal.blogspot.com
+255 655 821 550
Sulayman Sangida