Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Matibabu ya bawasiri:

1. Aloe Vera Fresh
View attachment 842294
Chukua kipande cha jani la mmea wa Aloe vera fresh (mshubiri) na kikate ukimenye kidogo ukitumia kidole kupata kama utomvu hivi au maji maji yake na upake sehemu ya utupu wako wa nyuma baada ya kuoga kutwa mara tatu.
Jipake nyingi tu na uiache hivyo masaa kadhaa au mpaka utakpaoenda kuoga tena.
Tengeneza pia juisi freshi ya mmea huu na uchanganye nusu glasi dawa hii na nusu glasi nyingine ya juisi yoyote ya matunda uliyotengeneza nyumbani ili kupata glasi moja iliyojaa na unywe glasi 1 kutwa mara mbili kwa wiki 3 hadi 4.
Juisi freshi ya aloe vera ni nzuri kwa kuongeza kinga ya mwili na kutoa taka zote za ndani ya mwili.


2. Juisi ya limau (lemonade)
View attachment 842296
Chukua juisi ya limau na upake sehemu iliyoathirika. Juisi ya limau sifa yake kuu hapa ni kuondoa sumu na kuongeza kinga ya mwili kwakuwa ina vitamin C kwa wingi. Pia unywe glasi moja ya juisi hii kutwa mara kwa wiki 3 hadi mwezi mmoja.

Lemonade inaandaliwa kwa kutumia limau, maji, asali na mdalasini ya unga kidogo, nayo inaandaliwa hivi:

Chukua asali mbichi nusu Lita

Chukua limau kubwa 12 au zaidi, zikate katikati kila moja. Zikamuwe moja baada ya nyingine kupata maji maji ya limau mpaka umepata ujazo wa nusu lita.
Kwenye sufuria nyingine kubwa changanya mdalasini ya unga vijiko vikubwa 10 na maji lita 2 na nusu na uchemshe kama chai kisha ipua na uchuje na usubiri ipowe iwe ya uvuguvugu kidogo.
Sasa changanya pamoja asali nusu lita, juisi au maji maji ya limau nusu lita, maji ya uvuguvugu ya mdalasini lita 2 na nusu ongeza na ya maji ya kawaida lita 1 kupata lita 5, chuja vizuri. Ihifadhi katika friji isiharibike.
Kunywa robo lita (ml 250) kutwa mara 2 kwa siku 30 hivi kwa mtu mzima na glasi ndogo moja kwa siku kwa mtoto wa miaka miwili mpaka kumi.
Unaweza pia kuongeza majani kidogo ya mnanaa (mint) na mbegu za shamari (fennel seeds) ili kuongezea radha na harufu nzuri.
Kunywa juisi hii kila unapokuwa umepata chakula cha mchana cha nguvu au cha jioni.
Unaweza pia kupakaa sehemu yenye bawasiri juisi hii ukitumia pamba kutwa mara 2. Unaweza kusikia maumivu zaidi lakini pole pole yataacha.

3. Mafuta ya nyonyo
View attachment 842297
Pakaa mafuta ya nyonyo mara mbili mpaka tatu kwa siku sehemu ya utupu wako wa nyuma kwa wiki tatu hadi nne hivi.


4. Mafuta ya zeituni
View attachment 842298
Mafuta ya zeituni (Olive oil) ni moja ya dawa maarufu katika kutibu bawasiri. Mafuta haya yana viuavijasumu na huondoa pia maambukizi (infections). Yanaweza pia kusaidia kuongeza utanukani wa mishipa ya damu. Yanao uwezo pia wa kukausha kinyama cha bawasiri ya nje yakitumika kwa kupaka kwa kipindi kirefu.
Kunywa kijiko kidogo kimoja cha mafuta ya zeituni kila siku. Pia tumia pamba pakaa sehemu yenye tatizo nje na ndani kutwa mara 2 kila siku mpaka umepona

5. Kipande cha barafu
View attachment 842302
Barafu inasaidia kubana mishipa na hivyo kuzuia uvimbe pia kuondoa maumivu kwa haraka.
Chukua kipande cha barafu na ukifunge ndani ya kitambaa kisafi na uweke moja kwa moja sehemu yenye tatizo kwa dakika 10 hivi. Fanya zoezi hili mara kadhaa katika siku. Zoezi hili linaondoa maumivu ya bawasiri na dalili zake.

6. Mafuta ya nazi
View attachment 842321
Mafuta ya nazi ni moja ya dawa nzuri sana kwa kutibu bawasiri. Mafuta ya nazi ni dawa nzuri dhidi ya bakteria, virusi na vijidudu nyemelezi sifa ambazo zinayafanya kuwa bora kwa kutibu bawasiri.
Mhimu yawe ni mafuta ya asili kwa asilimia 100 bila kuongezwa kingine chochote ndani yake na hayajapita kiwandani.
Safisha vizuri sehemu yenye tatizo na ukaushe na kitambaa, chukua pamba chovya mafuta ya nazi na upake sehemu yenye tatizo nje na ndani kutwa mara 3 kwa majuma kadhaa.


7. Maziwa ya mbuzi
View attachment 842322
Kama unasumbuliwa na bawasiri ya ndani na inakusababishia kuwa unapata choo chenye damu unatakiwa ujaribu maziwa ya mbuzi. Hii ni moja ya dawa rahisi zaidi za kutibu bawasiri ya ndani.

Chukua nusu kijiko kidogo kimoja cha unga wa mharadali (mustard) uchanganye na vijiko vikubwa 10 vya maziwa ya mbuzi na unywe kabla ya chakula cha asubuhi kila siku.

8. Binzari
View attachment 842328
Binzari au manjano inao uwezo wa kuzuia na kutibu magonjwa. Hivyo inaweza kutumika pia kutibu sehemu iliyoathirika na bawasiri.
Namna ya kutumia: chukua binzari ya unga kijiko kidogo kimoja changanya na mafuta ya mharadali na maji maji ya kitunguu maji na upate uji mzito (paste). Pakaa moja kwa moja huu mchanganyiko sehemu yako ya utupu wa nyuma na uache huko kwa dakika kadhaa.
Hii inasaidia kutibu majeraha na kupunguza uvimbe mara moja. Tumia kwa majuma kadhaa.

9. Unga wa Kokwa la Embe
View attachment 842330
Kutumia mbegu kubwa za maembe ni namna nyingine rahisi ya kutibu bawasiri hasa ya ndani inayotoa damu.

Tumia kama ifuatavyo:

Chukua mbegu za maembe (kokwa) toka katika maembe yaliyoiva, zianike juani kwa siku kadhaa na zikikauka kabisa zitwange au peleka mashineni upate unga wake na uuhifadhi unga ndani ya chupa isiyopitisha hewa.
Kisha changanya gramu 2 za unga huu na kiasi kidogo cha asali na ulambe yote. Fanya hivi kutwa mara 2 kwa majuma kadhaa.
Kwa faida ya ziada ni kuwa Unga huu wa mbegu za maembe hutumika pia kukaza uke uliolegea au ulioongezeka sana ukuwa.










Sent using Jamii Forums mobile app
asante sana ushimen

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wakuu

kuna rafiki yangu amepata na jambo la kushangaza ameniambia kuna kinyama kimetokeza kwenye anus ambacho akikigusa kinaumaa. Ila kutembea na kukaa hakuna maumivu yoyote

Nimemuuliza maswali machache amesema ameshindwa kwenda kupata choo kwa sababu panauma.

Ila nimemshauri kwenda hospita this week

Swali langu kwenu ni tatizo litakuwa ni nini.!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo sio wewe ? Mbona kila mtu ana rafiki yAke kila siku humu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari zenu wakuu

kuna rafiki yangu amepata na jambo la kushangaza ameniambia kuna kinyama kimetokeza kwenye anus ambacho akikigusa kinaumaa. Ila kutembea na kukaa hakuna maumivu yoyote

Nimemuuliza maswali machache amesema ameshindwa kwenda kupata choo kwa sababu panauma.

Ila nimemshauri kwenda hospita this week

Swali langu kwenu ni tatizo litakuwa ni nini.!?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tafuta mafuta ya nyonyo, chovya na pamba usiku iweke maeneo ilale hadi asubuhi kisha itoe.

Ila kunywa glass ya maji yalichanganywa na punje za vitunguu swaumu kama 5 hivi.

Anywe hivyo kutwa mara tatu, afanye kwa wiki.
Hana haja ya kwenda kukata nyama hiyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi anus ni tafsida au lugha mbadala mzungu nae akisoma inakuwaje?
nawashangaaga mod ukiandika kwa kiswahili wanachukulia umeandika tusi ila kiungo hichohicho ukikiandika kwa kizungu eti unakua umepunguza ukali wa maneno hahahaha
 
ahaa poa nimemuambia aende hospital ila uchumi wako hauko gud but nimemuambia this week ajitahidi kwendaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ajitahidi kunywa maji mengi, ale matunda ya kulainisha choo, asikae chooni muda mrefu
Mtafutie mafuta ya mzaituni, akikosa kwa leo hata ya nazi apakae, kama kuna poda ya watoto apake maumivu yatapungua. Pia asikae muda mrefu, kama ni mtu wa kutumia pikipiki au baiskeli apunguze.
Vitamsaidia kwa uwezo wa Allah kipindi hiki hana pesa
 
Back
Top Bottom