Uingereza kuwa na Mawaziri watatu wenye asili ya Afrika ambao wataongoza Wizara nyeti za nchi hiyo, Fedha, Mambo ya Nje na Mambo ya Ndani

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Waziri mkuu mpya wa Uingereza bi Liz Truss jioni hii ameanza kuunda baraza lake la mawaziri na bwana Kwasi Kwateng ameteuliwa kuwa waziri wa Fedha huku bwana James Cleverly akichukua nafasi ya uwaziri wa mambo ya nje.

Bi Suela Braverman ameteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani kuchukua nafasi ya bi Priti Patel ambae alijiuzulu jana.

Kabla ya teuzi hizo bwana Kwateng alikuwa ni waziri wa masuala ya biashara, nishati na viwanda, bwana Cleverly akiwa waziri wa Elimu wizara ambayo ameisimamia tangu mwezi July mwaka huu. Bi Braverman aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali

Hizi wizara tatu muhimu nchini Uingereza kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hio zimepewa raia wa Uingereza ambao wana asili ya Afrika na wazazi wao wakiwa wahamiaji. Bwana Kwateng- wazazi wote wawili wakitokea Ghana, bwana Cleverly (mama) akitokea Sierra Leone na bi Suela baba yake alitokea Kenya na mama akitokea Mauritius.


Waziri mpya wa Fedha wa Uingereza bwana Kwasi Kwateng. Chanzo cha picha -Getty Images.


Waziri mpya wa mambo ya nje bwana James Cleverly- Chanzo cha picha PA wire


Waziri mpya wa mambo ya ndani Bi Sue-Ellen Cassiana (Suela) Braverman.

Waziri mkuu bi Liz Truss bado aendelea kupanga baraza lake jipya la mawaziri ambao wengi ni wale alokuwa wakimuunga mkono katika katika kampeni yake ya kuwania nafasi hiyo ndani ya chama cha wahafidhina.
 
Wenzetu wameendelea mifumo ipo imara ukishakuwa raia na una uwezo hata ukiwa mmasai unapewa uongoze
Elimu imara pia yachangia.

Wazazi wa hawa watatu wote walipohamia huko enzi hizo (miaka ya 60) kulikuwepo na fursa za kusoma bila kulipa ada kubwa ya shule.

Pili, fursa zilikuwepo ili mradi umesoma vyuo vikuu ambavyo ndivyo hukupa nuru ya kwenda mbele.

Mtoto yoyote aliezaliwa kabla ya 1980 huko ana maisha mazuri sana.
 
Nimeipenda hi taarifa ila waingireza wamezid kila mwak kuwafukuza mawazir jmn mkp lini ndani ya miaka mitatu wamesha watoa mawazir watatu kimya kimya kwa kashfa ndogo ndogo Kama ya huyu wa sas alieondoka bwan boris Johnson na Teresa may yey aliondolewa kwa kushindwa kuharakisha brexit Ila Boris Ni kula Bata kipind Cha. Corona sasa hyu itakuajw kwa bi tliz truss nafatilia kwa umakini sana siasa zao inagwa wazungu hawapendi ujinga wanaamini in perfectionist

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Si ndio kunaitwa kwa MAMA uko sasa kwanini watoto wasipewe nafasi kwenye Uongozi

Hongera yao
 
Huyu Jina tu linanishinda kulitamka emu naomba ulitamke tena mkuu anaitwa nani?
 
Mtazamo wake kuhusu taifa la ukraine maana. Predecessor ali devote much resource katika kuhakikisha the war torn ukraine is existing till now ??
 
Alafu atakuja mjinga anakwambia jamaa ni wabaguz,nenda China au Russia kama utaiona ngoz nyeus kwenye sehemu nyeti za nchi,sanasana wanakua sehemu nyet za majumbani kama chooni,mabanda ya nguruwe,na kutembeza nygo
 
Alafu atakuja mjinga anakwambia jamaa ni wabaguz,nenda China au Russia kama utaiona ngoz nyeus kwenye sehemu nyeti za nchi,sanasana wanakua sehemu nyet za majumbani kama chooni,mabanda ya nguruwe,na kutembeza nygo
1.Unataka China iwe na kiongozi mweusi kwa nini ? Je kuna Han Chinese mweusi ?

2. Unafahamu ni kwa nini Marekani na Ufaransa kuna raia wengi wa kimarekani na wa kifaransa weusi tofauti na China na Russia ?
 
1.Unataka China iwe na kiongozi mweusi kwa nini ? Je kuna Han Chinese mweusi ?

2. Unafahamu ni kwa nini Marekani na Ufaransa kuna raia wengi wa kimarekani na wa kifaransa weusi tofauti na China na Russia ?
Unakotaka kunipeleka so kwenywe biashara za utumwa? haya nahamishia magoli Iran, saud Arabia,na nchi nying za waaarabu,maana wao ndio waasisi
 
Diaspora kutoka Tanzania mbona wako nyuma kwenye kila jambo michezo hawapo, siasa hawapo, kwenye science hawapo yaani wapo wapo tu
Watanzania waliokuwa wakienda nje kusoma hawabaki huko, wanadunduliza wananunua vifiat/renault au akijitahidi Peugeot halafu wanarudi nyumbani kutanua. Wenzao walikuwa wanaamia kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…