Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Waziri mkuu mpya wa Uingereza bi Liz Truss jioni hii ameanza kuunda baraza lake la mawaziri na bwana Kwasi Kwateng ameteuliwa kuwa waziri wa Fedha huku bwana James Cleverly akichukua nafasi ya uwaziri wa mambo ya nje.
Bi Suela Braverman ameteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani kuchukua nafasi ya bi Priti Patel ambae alijiuzulu jana.
Kabla ya teuzi hizo bwana Kwateng alikuwa ni waziri wa masuala ya biashara, nishati na viwanda, bwana Cleverly akiwa waziri wa Elimu wizara ambayo ameisimamia tangu mwezi July mwaka huu. Bi Braverman aliwahi kuwa mwanasheria mkuu wa serikali
Hizi wizara tatu muhimu nchini Uingereza kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hio zimepewa raia wa Uingereza ambao wana asili ya Afrika na wazazi wao wakiwa wahamiaji. Bwana Kwateng- wazazi wote wawili wakitokea Ghana, bwana Cleverly (mama) akitokea Sierra Leone na bi Suela baba yake alitokea Kenya na mama akitokea Mauritius.
Waziri mpya wa Fedha wa Uingereza bwana Kwasi Kwateng. Chanzo cha picha -Getty Images.
Waziri mpya wa mambo ya nje bwana James Cleverly- Chanzo cha picha PA wire
Waziri mpya wa mambo ya ndani Bi Sue-Ellen Cassiana (Suela) Braverman.
Waziri mkuu bi Liz Truss bado aendelea kupanga baraza lake jipya la mawaziri ambao wengi ni wale alokuwa wakimuunga mkono katika katika kampeni yake ya kuwania nafasi hiyo ndani ya chama cha wahafidhina.