Uingereza: Waziri Mkuu Liz Truss ajiuzulu baada ya siku 45 madarakani

Na bado simmekubalikuburuzwa na Beberu mkuu,pambaneni na hali yenu🥱
 
Bora hiyo kuliko kutawaliwa na mtu au chama kimoja kwa nusu karne
Sasa kwa taarifa yako hiyo siyo ishara ya utimamu. Ni dalili za disfunctional political system. Ni vile tu kwamba washajijengea jina kubwa na historia kama british empire na nyie mnaona kila ujinga wao ni ustaarabu kwenu.
 
Vilaza wengi hawaelewi hili
Kweli kabisa. Unajua ni kwa nini wanapenda madaraka? Kwa sababu kuwa kwenye madaraka kwa mwafrika ni kutumbua maisha. Ingekuwa wanawajibika ipasavyo wasingeng'ang'ania kwani kazi yoyote huchosha.
 
Endelea kubaki na akili zako za kidikteta za kiputin, utaendelea kubaki nyuma gizani daima ukiyashangilia madikteta
 
Sio rahisi dikteta Putin atolewe madarakani na raia wake wa kawaida, amejifanya Rais wa milele kwa nguvu ya dola.
Itahitaji jeshi, Oligarchs au FSB wamuondoe au afie madarakani.
Nikikumbukaga wale walokua wanasema Putin atatolewa madarakani na raia wake sasa yamekua kwao wenyewe.
 
Sawa, ila aina hii ya siasa ukiileta bongo mtashangaa mtakavyokuwa kama Somalia. Niamini stability ni kitu cha muhimu sana. Hao wangereza wanaafford kujiuzulu na kubadilishana kiholela hivyo kwa sababu kuna mifumo mingine inayowabeba.
Na sisi tutengeneze mifumo ya aina hiyo badala ya kutegemea watu tu.
 
Aliingia madarakani ili amzike malkia, amemaliza kazi yake anaachia madaraka.
 
Umekaa bara la gizani mpaka akili zimefubaa katika suala la demokrasia na uwajibikaji.
Inasikitisha sana.
Naona Putin amewavuruga kweli kweli! Ni mchana tu wa leo nilimsikia kupitia DW akiapa kutojiuzulu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…