Uingereza: Waziri Mkuu Liz Truss ajiuzulu baada ya siku 45 madarakani

Uingereza: Waziri Mkuu Liz Truss ajiuzulu baada ya siku 45 madarakani

Screenshot_20221020-194128_Twitter.jpg
 
Huwezi kufikiria hata kidogo?huyo waziri mkuu kwashindwa kuja na mipango ya maana kusaidia uchumi wao unaoyumba Kwa Sababu ya hii vita.sasa ili maafa yasiendelee waache Putin ashinde na waongee naye amalize vita.maana Putin lazima ashinde.
Unaweza kuwataja Waziri wakuu wa Uingereza waliomaliza miula yao ya uongozi pasi na kujiuzulu? Au kiongozi wa Uingereza kujiuzulu kwa maslahi ya nchi yake inahusika vipi na Vita ya Ukreine na Russia?

Borison na Magreth walijuliuzulu kwasababu Putin?

Badala ya kuombea viongozi wako waige Tania ya kuwajibika pale wanaposhindwa kusimamia sera nzuri ya kuleta maendeleo kwa wananchi wewe unashangilia mambo ya Putin utafikiri mkewe. Vitu vingine ni kujiabisha tu...kabla ya Vita nchi zilizostaraabika viongozi wake walikua wanawajibika.
 
Hapa maasi ya 1964 Nyerere hakujiuzulu, kuleta Azimio la Arusha na kutaifisha mali za watu bado Nyerere hakujiuzulu, kulazimisha watu kwenda kwenye vijiji vya ujamaa kwa nguvu na kusababisha wengine kufariki dunia bado Nyerere hakujiuzulu, kutupeleka kwenye vita na Uganda ili kumrejesha rafiki yake Obote madarakani na kusababisha uchumi kufa hadi leo bado Nyerere hakujiuzulu, kuleta mfumo mbovu wa ujamaa ambao ulipelekea nchi kudumaa kiuchumi hadi leo pamoja na kuwa na rasilimali lukuki lakini bado Nyerere hakujiuzulu.

Akina Mkapa kufanya biashara kinyemela wakiwa ikulu na kukwepa kulipa kodi lakini bado hawakujiuzulu. Mkapa kuamuru watu kuuwawa Zanzibar kwa kupinga wizi wa kura bado hakujiuzulu.

Kikwete kuamuru akina Daudi Mwangosi kuuawa haikumfanya ajiuzulu na hata kuamuru akina Ulimboka kuteswa bado haikumfanya ajiuzulu na mengine mengi.

Magufuli ndio kabisaaaa, hata sitasema. Kujiuzulu tuwaachie wazungu kwani sio utamaduni wetu.
 
Hapa Tanzania majina kwenye circles za kisiasa ni yale yale toka tunapata uhuru.

Tunatawaliwa na kikundi cha watu wachache tu ambao wao ndio wanaamua hatima ya maisha yetu.

Nothing has changed since independence.
 
Kujitambua na demokrasia
Wabongo huwa tunaangalia effects ,za ushoga tu
Mambo makubwa kama haya hatuyaongelei kabisa , waziri mkuu kuacha kazi ndani ya 45 days si kitu kidogo ati , mifumo ya demokrasisa , check and balance ipo mahala pake haswaa
 
Sasa kwa taarifa yako hiyo siyo ishara ya utimamu. Ni dalili za disfunctional political system. Ni vile tu kwamba washajijengea jina kubwa na historia kama british empire na nyie mnaona kila ujinga wao ni ustaarabu kwenu.

Kaka Maghayo hujambo
Hivi huyu Maghayo ndiyo yule aliwahi kuhonga sh 7528 au nimechanganya?
 
Nyinyi mbulula , hivi mnajua hata ni sababu gani imemfanya ajiuzuru...au mnashoboka na putini kwa jinsi ya ufinyu wa kuelewa siasa za UK...
Jana kulikuwa na Fracking vote je wanajua kilichotokea?
Leo huku hakuna Habari za Putin kabisa ni siasa za ndani tu mwanzo mwisho
 
Unaweza kuwataja Waziri wakuu wa Uingereza waliomaliza miula yao ya uongozi pasi na kujiuzulu? Au kiongozi wa Uingereza kujiuzulu kwa maslahi ya nchi yake inahusika vipi na Vita ya Ukreine na Russia?

Borison na Magreth walijuliuzulu kwasababu Putin?

Badala ya kuombea viongozi wako waige Tania ya kuwajibika pale wanaposhindwa kusimamia sera nzuri ya kuleta maendeleo kwa wananchi wewe unashangilia mambo ya Putin utafikiri mkewe. Vitu vingine ni kujiabisha tu...kabla ya Vita nchi zilizostaraabika viongozi wake walikua wanawajibika.
Hakuna cha demokrasia wala uwajibikaji hapo, kama mawaziri wakuu wanajiuzulu kwa kutomaliza mihula,hilo ni tatizo siyo demokrasia. Ni udhaifu katika uandaaji wa viongozi
 
Waziri Mkuu wa Uingereza, Liz Truss ametangaza kujiuzulu nafasi yake

Liz Truss alichukua madaraka kutoka kwa Boris Johnson tarehe 05/09/2022

View attachment 2392829

Liz Truss amechukua hatua hiyo baada ya baadhi ya mawaziri na wabunge wa chama chake cha Conservative kusema kuwa hawaridhishwi na kazi yake na kumtaka ajiuzulu.

----

Liz Truss resigns as prime minister

Liz Truss has resigned as prime minister and will step down after a week-long emergency contest to find her successor, she has announced outside Downing Street.

It follows a turbulent 45 days in office during which Truss’s mini-budget crashed the markets, she lost two key ministers and shed the confidence of almost all her own MPs.

Her statement came after she met Graham Brady, the chair of the 1922 Committee of backbench Tory MPs at Downing Street, followed by her deputy PM, Thérèse Coffey, and the party chair, Jake Berry.

Truss said she had entered office with “a vision for a low-tax, high-growth economy that would take advantage of the freedoms of Brexit”.

She went on: “I recognise that, given the situation, I cannot deliver the mandate on which I was elected by the Conservative party. I have therefore spoken to His Majesty the King to notify him that I am resigning as leader of the Conservative party.

“This morning I met the chairman of the 1922 Committee, Sir Graham Brady. We’ve agreed that there will be a leadership election to be completed within the next week. This will ensure that we remain on behalf to deliver our fiscal plans and maintain our country’s economic stability and national security. I will remain as prime minister until a successor has been chosen.”

Chanzo: The Guardian
Kumekucha! Kumekucha! Kumekuuuucha!
 
Hakuna cha demokrasia wala uwajibikaji hapo, kama mawaziri wakuu wanajiuzulu kwa kutomaliza mihula,hilo ni tatizo siyo demokrasia. Ni udhaifu katika uandaaji wa viongozi
Viongozi wa CCM wameandaliwa vizuri kwa ajili yako mnyonge ili wakuminye na tozo na kodi kibao, na wanakupenda sana...
Aisee...kweli hii nchi imejaa mazwazwa....
 
Huu sasa ni ujinga,hii siyo democrasia.watajiuzulu wangp?
Hali ya maisha ndio inafanya iwe hivyo watu wanataka mtu mwenye nguvu ya kutuvusha hapa

Maisha yamekuwa juu sana na Liz sio wa kutuvushaaa
Mulete muzungu Boris
 
Back
Top Bottom