Ujinga ni tatizo kuu hapa Tanzania

Ujinga ni tatizo kuu hapa Tanzania

Sio mpaka foreign ila sekta binafsi inaweza kuwa na ufanisi kuliko public sector maana wao ni profit-oriented sio blah blah. Hata hao US wametoa bandari zao kwa mikataba ya miaka mpaka 50 kwa kampuni za UAE Ili kuongeza ufanisi.

Hapa Cha kuweka sawa ni mikataba tu ila kubinafsisha bandari sio kitu Cha ajabu maana hata waliopo hao TPA wamefeli kabisa.

Hata hapo TPA ni rushwa, ufisadi, madawa ya kulevya, magendo n.k yanapitishwa tu hata sahivi?! Mnavyoongelea sovereignty it's as if sahivi magendo hayapiti?
Naskia pale wafanyakazi wanarudi na mifuko ya hela majumbani mwao kila weekend. Ni wizi tu
 
Sio mpaka foreign ila sekta binafsi inaweza kuwa na ufanisi kuliko public sector maana wao ni profit-oriented sio blah blah. Hata hao US wametoa bandari zao kwa mikataba ya miaka mpaka 50 kwa kampuni za UAE Ili kuongeza ufanisi.

Hapa Cha kuweka sawa ni mikataba tu ila kubinafsisha bandari sio kitu Cha ajabu maana hata waliopo hao TPA wamefeli kabisa.

Hata hapo TPA ni rushwa, ufisadi, madawa ya kulevya, magendo n.k yanapitishwa tu hata sahivi?! Mnavyoongelea sovereignty it's as if sahivi magendo hayapiti?

Kwani kuna mtu amepinga Uwekezaji? Kwa nini mnapotosha mambo? Kelele zote watu wanazopiga ni kuhusu Mkataba ambapo wanataka uboreshwe na siyo kama ulivyo sasa watu wote hawawezi kuwa wajinga, hakuna anayepinga uwekezaji kila mtu analijua hilo hata mtoto mdogo ila tusichotaka ni kuibiwa kama tulivyoibiwa huko nyuma, hivyo watu wanataka win win situation na siyo kuibiwa, sasa hivi we know better …
 
Fikiria mtu haoni haya kuongea upumbavu kama huu hadharani
Labda kosa ni kuongea hadharani, lkn sirini tunachopinga ni Mwarabu tu otherwise mkataba kama huo huo angepewa mzungu sie ingekuwa roho kwatu!!
 
Kwani kuna mtu amepinga Uwekezaji? Kwa nini mnapotosha mambo? Kelele zote watu wanazopiga ni kuhusu Mkataba ambapo wanataka uboreshwe na siyo kama ulivyo sasa watu wote hawawezi kuwa wajinga, hakuna anayepinga uwekezaji kila mtu analijua hilo hata mtoto mdogo ila tusichotaka ni kuibiwa kama tulivyoibiwa huko nyuma, hivyo watu wanataka win win situation na siyo kuibiwa, sasa hivi we know better …
Kwani Serikali haijajibu hizo hoja? Maelezo mangapi yametolewa? Wewe hujasikia watu wakisema tunauzwa? Bandari inauzwa? Nchi inauzwa?
 
Labda kosa ni kuongea hadharani, lkn sirini tunachopinga ni Mwarabu tu otherwise mkataba kama huo huo angepewa mzungu sie ingekuwa roho kwatu!!
Pengo na Slaa are proud of you
 
Miwili? Watu wana 5 yrs hawajapata kitambulisho
Ila akitokea Kiongozi akasemq kua nawapa NIDA waarabu kutoka Dubai wakamilishe zoezi la vitambulisho ili kila anaestahili apate ndani ya mwezi tangu alipojisajili utaona vumbi litakalotimka
 
Ni wajinga hawa hawa ndiyo wamefanya tupoteze mabilioni ya dollar za Marekani kwenye makaa ya mawe ya Mchuchuma na Liganga.

Hivi Sasa makaa ya mawe yamepitwa na wakati, uhitaji wake ktk masuala ya nishati umepungua kiasi cha kutisha eti ndiyo hawa tunastuka kutafuta mwekezaji.

Mleta mada umeeleza vizuri sana ktk uzi wako huu kuwa hawa wajinga ni wa kupuuzwa.
 
Mimi nakuona wewe ndio mjinga Fulani hivi unaejifanya una akili. Wapi watanzania wamekataa wawekezaji?
Huzisikii hizi kelele za Do World? Wapumbavu wanasema nchi imeuzwa na wazanzibari 3.

Sasa wazanzibari wameuza vipi nchi? Ni kwasabb wajinga wanaamini kumpa mwekezaji ni sawa na kuuza nchi.
 
Una uhakika hizo hoja hazijajibiwa? Au zimejibiwa na hujataka kukubali hayo majibu?
Mkuu,kazi ya kukalili kama kasuku
Labda umuulize alipotoa hizo hoja maana yy kazikopi sehemu , naona kila mmoja anarudiarudia hoja hizo hizo
 
Kwani Serikali haijajibu hizo hoja? Maelezo mangapi yametolewa? Wewe hujasikia watu wakisema tunauzwa? Bandari inauzwa? Nchi inauzwa?

Kwa hiyo hawa wote wanaopiga kelele na kupaza sauti ni wajinga na hawajui chochote au?
 
Kweli wawekezaji wana nguvu ajabu, swali la kujiuliza...wakati viwanda vinabinafsishwa kuna wengi walipiga makofi, madini yanachibwa lakini yote ni ujinga mtu...leo watu wanapiga kelele kuhusu kurekebishwa kwa baadhi ya vifungu kwenye makubaliano ya DPW ili tusije tukaumia mbele ya safari ila kuna watu mipumbavu kama mleta mada wao kutwa kuleta lawama jumuishi kuwa watu wanakataa uwekezaji.

Tusaidie serikali kwa kuwashauri pa kuboresha na siyo kuleta stori jumuishi bila kuonesha sehemu zenye matatizo, hizi mikataba zinaandaliwa na watu hivyo wanaweza kukosea.
 
Enzi za Mao, China ilikuwa nchi ya kikomunisisti iliyoamini katika Sera za Ukomunisti.

Pamoja na Ukomunisti wa China, Rais wa kwanza wa China, Mao aliamini kuwa ni lazima apeleke vijana nje ya China wakajifunze Dunia inaendaje na ikoje ili warudi kufanya mabadiliko China.

Moja ya vijana hao alikuwepo Den Xiapoing ambaye alikuja kuwa Rais wa China baada ya Mao. Den alipelekwa Ulaya na akajifunza sana namna uchumi wa Ulaya ulivyokuwa unaenda.

Alipokuja kurudi China, Den alianzisha mfumo wa Private Property na Uwekezaji wa Sekta binafsi katika mfumo wa Uchumi wa China. Kipindi chake ndo makampuni mengi ya Marekani yalienda kufungua viwanda na kufanya uwekezaji China.

Kwa wachina wengi walimuona Deng ni msaliti wa Mao kwa kuwa wengi walikuwa wanaamini kila kitu ni cha wachina na mwekezaji kutoka nje ni mwizi. Den aliwajibu haijalishi kama paka ni mweupe au ni mweusi ili mradi anakamata panya basi huyo anatufaa

Pamoja na wachina kupata shida kuelewa Sera za Den Xiapoing ila leo ndo wachina wanamsujudu kama The Father of Modern China.

Ukiacha China kuna nchi za Singapore na Umoja wa Falme za Kiarabu ambao Dubai ni nchi mojawapo za umoja huo.

Hizi nchi nazo miaka ya 1960 ilikuwa kama sisi! Ila watawala wao walipata akili kuwa kwa akili za kuwaza sisi ndo sisi hatutafika popote. Kupitia rasilimali ya mafuta Dubai walibadilisha Sera zao kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi. Leo hii kila mtu Duniani anakwenda kutalii Dubai na si kwa sababu ya mafuta tu ila kutokana na namna ikivyojengwa , inavyopendeza na ilivyo na uchumi mkubwa na maendeleo makubwa.

Ukija Tanzania. Hapa ndo shida ilipo. Nchi hii ilianzishwa katika misingi ya kijamaa. Misingi hii iliwaaminisha watu kuwa kila kitu ni Serikali na Serikali ni kila kitu. Mfumo huu ambao unaamini katika state capture umedumaza akili za Watanzania wengi sana kiasi ambacho kuna Watanzania leo hawajifunzi hata dunia ikoje, inaenda wapi na itakuwa wapi miaka hata 50 mbele.

Akili hizi zinaamini kuwa Sera ya uwekezaji ni kuuza nchi, Uwekezaji ni uuzaji wa nchi. Sera hii imewafanya Watanzania kuwa nyuma sana. Nchi yetu kuwa nyuma sana, mifumo yetu ya huduma kuwa nyuma sana.

Leo hii Tanzania, unatoka Dar hadi Kigoma kwa masaa zaidi ya 15 kwenye treni ambayo muda wowote unaweza kuambiwa leo hakuna usafiri. Ndani ya hiyo treni vyoo vichafu, huduma ni mbovu ila mtanzania hana shida ili mradi tu inamilikiwa na Serikali

Leo hii nchi yetu ina bandari zinayoweza kuhudumia ipasavyo nchi hadi 8 zinazotuzunguka, ila meli zinakaa wiki 2 hadi 3 kushusha mizigo, wafanyabiashara wanapoteza mizigo yao, hakuna mapato makubwa nchi inaweza kupata na kufanya maendeleo makubwa ila watu wanaona sawa tu ili mradi iwe chini ya Serikali. Hawajali hata wakiambiwa meli zinakimbia zinaenda Bandari za nchi jirani ili mradi waone au wasikie Serikali ndo mmiliki. Huu ni ujinga uliotukuka sana.

Kibaya zaidi pamoja na ujinga huu wa Watanzania, nchi jirani zinazotuzunguka zinakimbia sana ili kukamata fursa za kiuchumi sisi tusiwe na kitu. Rwanda amejenga Bandari kavu kubwa sana ili mizigo ya Congo Mashariki ipite kwake . Bandari hii kawapa wawekezaji. Sasa Rwanda anajenga uwanja wa Ndege mkubwa zaidi Afrika Mashariki ambao utaendeshwa pia na Sekta binafsi.

Huku Kenya amejenga Bandari ya Lamu ambayo ataiendesha kwa sehemu kubwa kupitia sekta binafsi, Msumbiji kaomba vikosi vya Rwanda vilinde Bandari zake ili wawekezaji waweze kuwekeza na zifanye biashara. Hawa wakifanya haya Serikali ikichukua hatua kuboresha utendaji wa Bandari kuna watu wanaaza kusema nchi inauzwa.

Serikali ikiwasikiliiza hawa watu kuna hatari kubwa sana huko mbeleni nchi yetu kuja kuwa kituko cha mwisho zaidi kuliko hata sasa, kutokana na kusikiliza wajinga huku nchi ikitakuwa ikimbie iendane na mabadiliko ya Dunia ya sasa.

Kwa Dunia inavyokwenda sasa, Tanzania haipaswi kurudi nyuma tena! Ujinga usipewe tena nafasi Tanzania!
Hata China ingeingia mikataba dizaini hii leo ingekuwa maskini zaidi
 
Kwani kuna mtu amepinga Uwekezaji? Kwa nini mnapotosha mambo? Kelele zote watu wanazopiga ni kuhusu Mkataba ambapo wanataka uboreshwe na siyo kama ulivyo sasa watu wote hawawezi kuwa wajinga, hakuna anayepinga uwekezaji kila mtu analijua hilo hata mtoto mdogo ila tusichotaka ni kuibiwa kama tulivyoibiwa huko nyuma, hivyo watu wanataka win win situation na siyo kuibiwa, sasa hivi we know better …
Hapana wengi wanapinga bandari kupewa mwekezaji wanadai mambo ya usalama sijui nchi itauzwa n.k yaani sio tu mkataba uboreshwe hawataki kabisa DP world aje bandarini.

2. Wanadai tuliibiwa sana na wawekezaji yes ni kweli lakini kwa Sasa Kuna sheria nzuri zimewekwa mfano Ile ya 16% hisa kwa serikali, local content kwamba lazima ratio Fulani ya tender na ajira zitoke nchini, Kuna sheria kali za transfer pricing 2018 zimepunguza mianya ya kukwepa kodi walau kwenye haya makampuni ya nje etc. So mjadala uwe mkataba utakaoingiwa basi uwe na maslahi kwa nchi lakini sio kupinga mwekezaji apewe bandari.

3. Hao TPA ndio Wezi kuliko hata makampuni ya kigeni, so mbadala wa bandari usiwe TPA tena Bali muwekezaji serious otherwise tunachokwepa kubwa na DP ndio kinachoibiwa na hao wahuni wa TPA.
 
Back
Top Bottom