Ujinga uliowagharimu wengi kwenye maisha

Namba moja inahitaji mjadala mpana, sina uhakika kama unaweza kujadili. Otherwise tufunike kombe na tucall it a day!
 
Ahsante babaangu yaan huyu anajifanyaga kana kwamba neno lake ni sheria ,kanikwaza kutuponda single mom akat tuna bahat zetu,maisha hayana formula muache abwabwaje
 
Taikon nipumzike sasa!
Kwa wale wasiopenda kusoma nyuzi refu najaribu kufupisha.

Mtoa mada anazungumzia mitazamo mbalimbali ambayo watu wakiwa nayo inaweza kuwagharimu maishani mwao.

Mitazamo hiyo huwakilishwa k2a njia ya maneno,na hayo maneno ni kama yafuatayo.

1. Kusoma sio kufanikiwa maisha(wanabeza elimu)

2. Uliona wapi pipi ikaliwa na maganda yake(wanahamaisha ngono zembe)

3. Siwezi kujenga na kuishi kijijini Mimi(wanabeza kununua maeneo maeneo ya mbali na mji)

4. Ngoja nikupe/niolewe naye nitambadilisha au atabadilika(wwnabeti kwenye ndoa)

5. Acha Nile ujanita nitaolewa tuu(wanakataa ndoa kwa kudhani wakiolewa hawatokula ujana)

6. Pesa hainunui furaha(wanajifariji kwa sababu hawana pesa au hawajazipata)

7.Dini sio tatizo(wanadhani dini haimati kwenye ndoa kumbe si kweli)
kila mtu atakuwa na dini yake, ilimradi tunapendana

8. Kuoa single mother sio tatizo, Inategemea na Mwanamke(wanajaribu kutia mkono gizani kuoa single mother)

9.. Ninatetea na kusaidia Masikini na wanaoonewa, Mungu atanilipa(sio kazi yako kutetea masikini ni kazi ya MMungu.
 
nakazia namba 9
 
Swadakta!
Umenena vyema mkuu 😊
 


🙏🏾🙏🏾🙏🏾

MKUU nashukuru Kwa kutoa Muhtasari
 
Ahsante babaangu yaan huyu anajifanyaga kana kwamba neno lake ni sheria ,kanikwaza kutuponda single mom akat tuna bahat zetu,maisha hayana formula muache abwabwaje

Mimi nazungumzia 99/100 ndio maana nakuwa ninauhakika na nikisemacho.

Wewe unazungumzia 1/100 alafu unakuwa na uhakika nalo.

Nimeongea vile jamii yeti ilivyo, wewe Kama ni single mother hongera Kwa nafasi yako. Sijakusudia kukusema mabaya Ila nilikuwa nawatahadharisha Vijana wadogo wajiepushe na watu wa mfano wako. Hilo ndio kosa?

Kimsingi Mimi ninaamini katika falsafa ya;
Mpya Kwa mpya
Chakavu Kwa Chakavu
Jinga Kwa jinga
Single mother Kwa single Father au MGANE

Kanuni inasema kila mtu atapata wa kufanana maybe iweje kijana mpya achukue mwanamke aliyekwisha kuzaa,
Na iweje mwanamke mpya aolewe na jianaume zee?

Wewe Kama itakuuma utajua mwenyewe, wala sipo Kwa ajili ya kumfurahisha yeyote hapa, nipo Kwa ajili ya kufundisha wale wenye akili na Uelewa kama wangu.

Na Wale wanaotaka kuwa Kama Mimi.
 

Wewe Una degree lakini uwezo wako WA kuchambua mambo ni mdogo Sana.

Mimi nazungumzia 99/100 ndio maana ninaandika Kwa uhakika.

Wewe unazungumzia 1/100 alafu Kwa Uelewa wako mdogo utasema unauhakika.

Nafikiri hujui kitu inaitwa Exceptional Theory.

Unapoambiwa Jamii Fulani IPO hivi ujue watu wanangalia wengi wao, hao wachache hawawezi badili matokeo ya ukweli uliosemwa.
Au ukiambiwa Tanzania ni nchi iliyopo katika ukanda wa tabia ya nchi ya kitropiki ya Savannah ujue Maeneo mengi yanatabia hizo, sasa sio ufike Bukoba uone tabia za kiikweta useme Tanzania inatabia ya nchi ya kiikweta, utakuwa hamnazo na degree zako. Au ufike Dodoma ukute tabia ya nchi ya unusu jangwa alafu useme TANZANIA ni nchi ya unusu jangwa utakuwa hauelewi ukisemacho.

Mungu anaposema wanadamu wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wake, na hakuna mkamilifu haimaanishi hakuna wanadamu wakamilifu ndio maana akamtaja Ayubu alikuwa mkamilifu na hajawahi kutenda dhambi, lakini hawezi kumtumia mtu mmoja kufanya hitimisho lake, Kwa kusema wanadamu wote hawanadhambi kisa mtu mmoja. Ila wengi ndio huingia katika hitimisho.

Au ukiambiwa watu wa sodoma na Gomora walikuwa waovu lakini mbona alikuwepo Lutu nduguye Ibrahimu. Lakini uwepo wa lutu hauna athari katika kubadilisha matokeo ya hitimisho tunalolijua mpaka hivi leo.

Mama na Baba wakiwa Masikini kaa ukijua watoto watakuwa Masikini, hiyo IPO hivyo
Kama itatokea wakawa matajiri hiyo tunaita Exceptional.

Sasa wewe unasema kwenu wote mnadegree na mmoja anadiploma licha ya kuwa wazazi wenu hawajasoma na ni Masikini, angalia na Ndugu wa Mama zako na Baba zako ipo hivyo, angalia majirani zako ipo hivyo, angalia jamii yako ipo hivyo.

Sio umezaliwa njombe huko Kwa vile kuna baridi ndio useme Tanzania ni nchi ya Baridi, watu watakuona hamnazo!

Kuhusu single mother, Mimi sijaandika vibaya nimeandika ukweli na kuweka jamii ikae sehemu yake.
Huwezi tumia mfano wa mtu mmoja kujumuisha na kuzima mifano elfu iliyopo kwenye jamii.
Huyo Rafiki yako ni moja Kati ya waliobahatika tuu Ila wengi WA Vijana wanalalamika katika Jambo hilo.

Ndio maana nikakuambia wewe ni Wale wanatumia 1/100
Sisi ndio wengine tunatumia 99/100

Sasa wewe na Degree yako kama hujui mambo madogo Kama haya itakuwa unashangaa mno.

Vinginevyo uniambie umetumia hisia zaidi katika hili, lakini kama ni akili basi huu mi mtihani
 
Kanuni inasema kila mtu atapata wa kufanana
Mluu mimi naomba nijenge hoja katika hii kanuni ya "kilw mtu atapata wa kufanana nae"

Neno kufanana ni neno pana ambalo hatutakiwi kulitafsiri kwa kulifinya hhata kidogo.

Kwa sababu neno kufanana upsna wake inaweza kuwa kufanana kiumri,
Inaweza kuwa kufanana kwa rangi
Inaweza kuwa kufanana kwa tabia
Inaweza kuwa kufanana kwa dini
Inaweza kuwa kufanana kwa idadi ya watoto mliokuwa nao
Inaweza kuwa kufanana kwa urefu.
Inaweza kuwa kufanana kwa unene.
Inaweza kuwa kufanana kwa hali za kipato.
Inaweza kuwa kufanana kwa makabila.
Inaweza kuwa kufanana kwa level za elimu
kufanana kwa idadi ya ndoa mlizowahi kufunga nakadhaalika.

Mkuu hizo zote hapo juu ni tafsiri zinazoingia kwenye neno kufanana.

So ni dhaahir kwamba utakapooa mtu ambaye mumefanana kwa jambo fulani maana yake kuna mambo mengi kinyume na hayo mtatofautina tu.

Mfano kijana ambae hajaoa anaoa mke ambaye hajawahi kuolewa kwa kudai tu anaoa mtu aliyefanana nae,

hapo huyu mtu katafuta mke anayefanana nae kwa mujibu wa idadi ya ndoa alizozipitia huko nyuma na akaona kwamba huyu hajawahia kuolewa kama yeye.

Lakini mbali ya kufanana hhuko hao watu kwa idadi ya ndoa za nyuma bila shaka watatofautiana kwa mambo mengine mengi

Mfano wa mambo ambayo wanaweza kutofautina ni hadhi ya familia,kipato,elimu,rangi,kimo,aina ya kazi,tabia n.k

Sasa kama hii fomula ingekuea inamata basi leo watu wasingeishi pamoja ama ingekuwa dunia yote ni taabu tupu kwa sababu hatufanani kwa yote na wala hatutofautiani kwa yote.

Nikirudi kwenye point yangu ni kwamba kuoa single mother sio tatizo kwa sababu huwenda mkatofautiana kwenye ishu ya idadi ya watoto
lakini mkafanana kwenye ishu ya tabia,kabila,levo ya elimu,hadhi ya familia na hayo mliyofanana yakawafanya muiishi vizuri kwenye ndoa kuliko hayo mliyotofautina.
 

Umenena sahihi!

Unapozungumzia ufanano hapo lazima watu waelekeane walau Kwa 70%
Sio tuu kisa dini moja ndio mmefanana.
Mpaka pawe na ufanano watu huangalia percentage kubwa ya ufanano ikizidi 70%-100 hao wanafanana

Ikiwa 40-60 wapo nusu Kwa nusu.

Nasisitiza zaidi, ikiwa kijana bado ni mdogo na ndio anataka kuingia kwenye ndoa afuate ushauri wangu, aoe kijana mwenzake ambaye Naye ni mdogo ambaye hajawahi kuolewa wala hajawahi kuzaa.

Siongei Kwa ubaya bali Kwa wema tuu.
Tena Kwa dunia ya sasa ushauri wangu ndio unanguvu zaidi na unapaswa kufuatwa Kwa sababu wanadamu wengi wameharibika.

Na Mwanamke Kama anamtoto ninamshauri atafute mume mkubwa na mwenye watoto kama yeye, au Mgane tena aliye na uwezo angalau.
Sio kuwapa Vijana wawatu shida na misongo ya mawazo
 

Tatizo baadhi ya watu ishu ikiandikwa Kwa jamii wanaichukulia personal.
Ni Sawa na mchungaji au Sheikhe awe anasema Walevi au wezi alafu mtu mwenye tabia hizo aanze kurusha mawe.

Yeye anazungumzia 1/100
Mimi nazungumzia 99/100
Alafu haoni tofauti
 
Hiyo namba 9 nilijaribu kuifanya kwakweli mpaka Leo imeniachia maumivu ingawa wakati mwingine Mungu Kuna watu kawaanda kwaajiri ya kutetea wanyonge ila huwa tunapigwa vita Sana, wapo ambao hutiwa uchizi, wapo ambao huuwawa na kujeruhiwa,kwenye maisha kama unajihisi unaamani ya kutosha basi usijaribu kuwachokonoa binadamu utajuata kuzaliwa utaiona Dunia Chungu

Usiwe Funza kwenye ridhiki za watu, watakuuwa Watu wabaya Sana.
 
Jee mwanaume akiwa na mtoto halafu Binti Hana mtoto hii Iko okey
 
mwenzako kapanic aisee, yuko deep
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…