Ujumbe wa Afande Sele akimlilia Hayati Magufuli

Ujumbe wa Afande Sele akimlilia Hayati Magufuli

Afande amemlaumu sana Mungu kwa kutuonea waAfrica.

Ameshauri watanzania na waAfrica kuachana na dini za wazungu tuamini mizimu yetu na jua.

Amesema hayo akishangaa kwa nini Mungu aliyepewa kipaumbele na JPM ameshindwa kumlinda na husda za wazungu mpaka wakafanikiwa kumuondoa.
Kwa hiyo alitaka aishi milele. Idiot kabisa huyo mrasta.
 
Kwa Magu hata mimi imeniuma sana.. akili yangu inahisi ameuwawa kwa biological weapon.

Usalama wa taifa wamezidiwa ujanja na wazungu.

Najiuliza why yeye na msaidizi wake kijazi wafariki ndani ya muda mfupi kwa ugonjwa mmoja.. nahisi mtego waliotegwa na wakanasa ulikuwa unaenda kuvunja moyo kufanya kazi.. sitashangaa akifa mwingine kwa moyo tena
Jamani Corona ipo. Chukueni hatua hamtaki.

Mnaanza kuwasema wazungu oooh sijui nini?

Ukiwa mkaidi utakufa tu.
 
Cha msingi sayansi haiongopi.
Mnaambiwa mkiwa kwenye mikusanyiko mvae barakoa mnaleta ubishi na kuwasimanga viongozi wa dini wanaotoa angalizo.
Sasa mzee ameleta imani za kinjekitile kwenye Corona ameenda na maji alafu mvuta bange mmoja anakuja kulia-lia eti wazungu wamemuua.
Sayansi haiongopi.
huijui dunia wewe kaa kimya, endelea kuzunguka mitaani na bendera la chadema
 
huijui dunia wewe kaa kimya, endelea kuzunguka mitaani na bendera la chadema
Watanzania tumejengwa kwenye msingi ya uongo na lawama hata kama wazungu wame play part kwenye kifo chake yeye pia aliyataka kwa kauli zake na kuji expose wakati ana fahamu hali yake kiafya hakutakiwa kufanya yale aliyo kua ana fanya
 
hongera zako wewe unayeishi maisha sahihi.
 
huijui dunia wewe kaa kimya, endelea kuzunguka mitaani na bendera la chadema
Mataga dunia mnaijua nyie mnaoishi kama kinjekitile karne hii ya 21.
Haya leo mzee wenu kafa kwa korona baada ya kudharau sayansi nyie vibendera mlikua mnakenua alivyokua anadharau njia za kisayansi.
By the way nyie wajane mnatakiwa mchukue tahadhari za kisayansi na muache mihemko.
 
Ameingia kwenye vita na MUNGU ....
Siamini kama mwaka huu utaisha ...
Mungu amrehemu.
 
Mataga dunia mnaijua nyie mnaoishi kama kinjekitile karne hii ya 21.
Haya leo mzee wenu kafa kwa korona baada ya kudharau sayansi nyie vibendera mlikua mnakenua alivyokua anadharau njia za kisayansi.
By the way nyie wajane mnatakiwa mchukue tahadhari za kisayansi na muache mihemko.
endelea kukalia dyudyu za kina mbowe achana na mimi
 
Hizi ndio akili fupi fupi za watanzania walizopandikiziwa na Magufuli. Wao kila wakipata baya wanawaza kuwa wazungu ndio wamewaletea.

Sote tunajua Corona kwa sasa ndio inayouwa watu kirahisi sana. Wataalamu wamesema tuchukue tahadhari zote muhimu, Magufuli yeye anasema hakuna haja sana ya kuchukua tahadhari maana Tanzania hakuna Corona! Alikuwa anasema tujifukize na kunywa zile togwa za waganga wa kienyeji.

Haya sasa Corona imemtandika fresh na kumuua, nani tumlaumu?
Kwa hiyo kisukari,presha,Malaria,Homa za ini na Ukimwi vimeacha kuua.

Siasa kwenye kila jambo,wazee wakufuata upepo.

RIP Magu.
 
Afande amemlaumu sana Mungu kwa kutuonea waAfrica.

Ameshauri watanzania na waAfrica kuachana na dini za wazungu tuamini mizimu yetu na jua.

Amesema hayo akishangaa kwa nini Mungu aliyepewa kipaumbele na JPM ameshindwa kumlinda na husda za wazungu mpaka wakafanikiwa kumuondoa.
Afande apunguze matumizi ya mmea
Anaelekea pabaya
 
Napenda kuwapa pole kutokana na msiba wa kiongozi wetu.

baada ya Magufuli kufariki imesambaa voice clip iliyotoka kwa Afande Sele akilalamika kuhusu kifo chake akafika mbali zaidi na kutoa lugha za kumtukana Mungu. jambo hili limeonekana kuibua hisia nzito na hasira juu ya afande sele, mpaka watu wengine wameanza kulazimisha jeshi la polisi kumchukulia hatua kwa kosa la kumtukana Mungu.

Kwanza naomba niweke wazi kuwa mimi ni mkristo mwenye imani ya kipentekoste ingawa sisali mara kwa mara, naamini uwepo wa Mungu na ninamjua kwa sehemu.

Binafsi sioni sababu ya kuanza kumshambulia Afande Sele kwa alichosema maana ametoa uhalisia uliopo ndani yake sio mnafiki na mimi napenda watu hawa hata biblia imekataza kuwa mnafiki. Katika taifa kama Tanzania lenye uhuru wa maoni ingawa haikuwa hivyo kwa miaka hii ya karibuni labda kama hali itabadilika Afande sele hajafanya kosa lolote kutoa maoni yake kuhusu huyu tunayemuita Mungu.

Ni vyema tukaelewa kuwa sio lazima kila mtu aamini kuwa Mungu yupo na wanaoamini wana uhuru wa kumuabudu Mungu wanayemtaka ndio maana kuna miungu mingi, dini nyingi na ibada tofautitofauti. Sio lazima kila kinachosemwa na mtu kituridhishe au tukikatae vingine hatuna budi kuvikubali ili kuelewa mtazamo na msimamo wetu juu ya yule tunayemuamini kuwa ni Mungu. Mbona watu hawakutaka washirika wa midahalo ya waislamu na wakristo kuwa dini ya kweli na mungu wa kweli kipindi cha sheikh Mazinge wachukuliwe hatua maana sio kila wakati waliongea vizuri kuhusu upande pinzani.

Binafsi naona swala hili kuwa ni vita nyenye wahusika wawili tu MUNGU na afande sele, aliyetangaza vita ni afande sele kinachobaki ni uamuzi wa MUNGU kuamua kukaa kimya au kuingia vitani, wengine tukae kimya hatuwezi kumtetea MUNGU nafasi yetu ni kuangalia na kujifunza ili kujenga imani zetu. Serikali ina mambo mengi ya kufanya isipoteze nguvu kwa Afande Sele.

Ni jukumu la MUNGU kujitetea na kudhihirisha kuwa anafanya kazi na ana nguvu sio mwanadamu kumtetea Mungu. rejea kisa cha gideoni kwenye biblia alipovunja miungu ya jamii yake. WAAMUZI 6:28-32
 
Back
Top Bottom