Nadhani wazanzibari Wana moyo tofauti na wabara. Huku bara tulikiwa na rais mwenye moyo wa kishetani kwelikweli.
Sio kweli.
Vifo vya Robert Mzungu??
na Makatta nani alizima uchunguzi...Transparency
Damu zoa zimo mikononi mwake.
Wakati waganda wakiangamizwa na Kony kule Uganda-
Rais mwinyi aliviondoa vikosi vya maJeshi ya Tz vilivyokuwa vikisaidia majeshi ya Uganda katika mafunzo na mbinu zingine za kivita, kulikopeleka mauaji ya kikatili ya Joseph Kony kutokea.
Taarifa hizi huzisikii na zipo.
Sio hivyo tu, vita vya maziwa makuu yalianza wakati wa kipindi chake. Ameandika mwenyewe kuwa kilikuwa kipindi kigumu kwake, kwani alikuwa na nafasi ya kuzima mauaji ya kimbari Rwanda.
Hakufanya hivyo.
Inasadikika makontena yale ya mapanga yalipita Bandari ya DSM under his watch.
Damu za wa Rwanda zimo mikononi mwake.
Ingali ukitafakari hayo, Mwendazake Ali Hassan Mwinyi, wakati wale Mujahedeen wa Sudan wakiwaangamiza watu wa Sudan kusini, alisuasua kuwasogezea Usaidizi makundi kama ya SPLA na kupeleka Operesheni za kumtwanga Mwarabu wa Sudan, kuchelewa na kupeleka mauji mengine huko.
Damu za Wasudani zimo mikononi mwake.
Itoshe kusema, hakuwa ana roho ya umalikia kama unavyotaka kuaminisha kadamnasi.
Vilevile hakuwa Mzanzibari, ila tu kama unataka kusema alikuwa "Mwislamu' kitu ambacho ni hatari na kinaweza kujenga uhasama, kama ulivyotumia matamshi yako hapa, basi sawa
Yaani hisia zako, vinyongo vyako vya kibinafsi ndivyo vilivyo kupeleka kuhara Chuki.