Bila shaka hili swali linaonyesha pia umri, tuliokuwepo miaka hio hakuna mtu aliyechukiwa kama Nyerere, kimsingi magufuli ni mtoto kwa Nyerere, yule alikuwa anawanyofoa madarakani hadi Marais wa nchi nyingine, sijui Kama umewahi kumsikia Binaisa, Tito Okelo n.k
Waliokoswakoswa humu ndani kina Kasanga Tumbo, fundikira, Tuntemeke. Waliokimbia nchi ni wengi, waliokula Shaba labda uwaulize wazenji nini kilimkuta Karume alipotaka kuvunja muungano
Huyo Mwinyi ndio mlezi mkuu wa ujambazi na madawa ya kulevya, enzi hizo jambazi anakutumia barua kuwa saa flani anakuja akute fedha kadhaa, ole wako useme polis, na wanakuja kweli kuchukua hela zao!!! Wengi wa polisi waliamua kuwa majambazi, lakini wamasai wanamjua vizuri alichowafanyia huko loliondo
Kuna mwandishi aliyeandika habari za Mwinyi kuuza mbuni wa ikulu kwa waarabu, wa gazeti la mfanyakazi, kesho yake maiti ilikutwa kwenye mtaro
HAKUNA RAIS MPOLE