Ukiwa mfanyakazi Kilimanjaro utataabika sana.
— Kilimanjaro ni Kama Ina centers chache sana ( urban areas), sehemu nyingine ni mapori tu, ya vichaka, milima, miinuko, mabinde,na mvua ikinyesha ni tope.
— Maisha ni gharama, hata Dar Kuna nafuu. Hakuna dagaa, ufugaji mgumu na samaki mpaka waletwe kutoka kwingine, hivyo Bei ni kubwa.
— Huwezi kujenga, utapanga mpaka siku ya kustaafu.
— Huwezi kulima. Kilimanjaro ardhi hakuna, na iliyopo inayofaa ni kidogo sana, nyingine imejaa pori, mabonde, milima na mawe.
— Huwezi kufuga. Kilimanjaro hakuna ardhi, hivyo hakuna ufugaji huria. Ufugaji ni mgumu,Kama unafuga ng'ombe, nguruwe, mbuzi au kuku unatakiwa kuwakatia majani kila siku. Na wewe Kama ni chasaka huna shamba, huwezi kukata majani kwa mtu, wachagga wanapenda kesi kuliko KULA.
— Unafiki na roho. Mchagga Yuko tayari hata kukusalimia shikamoo ili umpe anachotaka, ila siku ukipata mabaya atafurahi huyo.
— Ni ngumu kufanya biashara. Kwasababu kwanza vijana wengi wanaikimbia Kilimanjaro na kurudi mwisho wa mwaka tu. Mkoa umejaa wazee tupu.
— Kilimanjaro haimfai kijana mtafutaji, labda Kama unakuja kukaa tu, hasa wastaafu.