Ukiogea chumvi ya mawe kila mtu hukuona ni mtu mwenye amani

Sahihi!
nilisoma mahali sikumbuki,unapokoga asubuh ujeukie jua linapochomoza. Nahisi ni humu humu ama youtube.

Yuko jamaa alifanya kazi sehemu zaidi ya nane na zote wanamfukuza bila sababu,mke kamwachia mtoto mdogo kachukuliwa na rafiki yake wa karibu..
Ni rafiki nilimsikiliza kwa kina,amekwenda kwa waganga wengi na amekunywa makombe(sijui vikombe) vingi vya wataalam ila hakupata msaada..

Hapa ofisini kwetu alikaa mwezi na nusu wakamfukuza"ilinisikitisha",sikuona sababu ya msingi ni alionewa tu,iko siku alipigwa na dereva wa staff bus kisa alimgusa bega..utawala ukasimama upande wa dereva.

Jamaa sijui alikua na nyota gani?hakuna zuri atakalofanya likaonekana..moyoni nikahisi ni "karma" inamwinda.

Siku niliona uzi wa Mshana Jr
Nikamshauri aogee maji ya chumvi.

Mwaka huu mwanzoni nilonana nae akanishukuru imemsaidia amepata kazi na amedumu anaendea mwezi wa sita.
 
Sadaka yangu natoa kwa wahitaji tu..sipeleki kanisani hata siku moja.

Naamini nitabarikiwa nikipeleka kwa wagonjwa,mayatima n.k

Hata sahani moja ya chakula kwa mwenye uhitaji ama kilo ya unga ni sadaka kubwa sana.

Wachungaji wanachangiwa masikini wanaombewa.
#ubatili
 
Kwani we ukiwa unapeleka pale kanisa moyoni umeamua kumtolea nani? Mtu hajiongozi yeye pakupeleka kutoa sadaka ila kama amekaa kwenye network nzuri yakusikia atasikia wapi pakupeleka kwahiyo hata akiambiwa apeleke kanisani haitomsumbua nani atakaye pokea hapo kanisani. Niongeze sauti ??
 
Sauti inatosha,
Wapelekee wakakuombee
 
Huwa inategemea na neno la Mungu na maelekezo ya Roho Mtakatifu atakayompa kuitumia hiyo chumvi...

Inaweza ikawa siku 3 au 7

Nyingine sio kuoga ni kula
mimi nimeifanya kuiogea kila siku..yaani ndio style ya maisha yangu kwa sasa...nilikuwa napigwa vita mbaya sana kuanzia kwenye familia ya baba yangu mpaka kwenye mfumo(system)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…