Ukiona kijana tajiri ujue ni mwizi, aliachiwa pesa na baba yake au beti

Ukiona kijana tajiri ujue ni mwizi, aliachiwa pesa na baba yake au beti

Nipo kwny fani ya madini.

ni normal sana kuona kijana ana zaidi ya million 300 under 30.

Mimi mwenyewe niliwahi kukamata million 60 nikiwa na 27 kwenye madini.

Huyu mtoa mada atakuwa mwalimu
 
Kumiliki 100m sidhan kama ni utajiri.

Binafsi umri wangu bado haujafika hapo kwenye 30. Ila kutokana na kazi na mshahara wangu nakopesheka mpaka mil 100 nikitaka.

Je hapo nakuwa tajiri?
 
Wewe unaonaje mkuu
Kuna jamaa nilimaliza nae darasa la 7, akashindwa kuendelea sekondari sababu ya maisha. Jamaa akaingia kwenye kazi za kuchimba madini tena locally na sululu tu nyundo majembe. Miaka minne baadae akiwa na miaka 21 akapata dhahabu akapata milioni 50 mi hapo nipo form 4. Akanunua trekta akaenda Kiteto akajichimbia kwenye kilimo huku akikodisha trekta. Baadae mi namaliza Chuo jamaa anamiliki pesa si chini ya milioni 400 akiwa 26yrs nilikutana nae nilimshangaa sana. Mpaka Sasa anamiliki nyumba nyingi sana mikoa tofauti.
 
Aliyesema hivyo ni mpumbavu sana na maskini wa kifikra. Siasa za ujamaa na kujitegemea ziliharibu sana fikra za watu na kudhani utajiri ni dhambi. Hadi nyakati hizi kwenye kampeni za uchaguzi wagombea hufanya maigizo kwamba wao ni maskini tu kama wapiga kura. Wapiga kura nao kwa kutaka kampani ya umaskini huishia kuwapigia kura wagombea wa aina hii. Tanzania utakuta mtu kama Fred mwenye umri wa zaidi ya miaka 35 anaitwa tajiri kijana wakati dunia ya leo ina mamilionea wenye miaka chini ya 25. Fikra kama hizo ndo zimefanya nchi kuendelea kupoteza pesa kwenye miradi kama BBT kwa kudhani kuna utajiri wa vikundi badala ya kuwawezesha vijana ambao tayari wako kwenye kilimo. Umaskini ni fedheha, tuukatae. Utajiri sio dhambi wala uhalifu.

Wazee wetu wengi hawataki kabisa changamoto mpya toka kwa vijana. Mimi niliwahi kuwa mwalimu wa sekondari kwa miezi kadhaa kabla sijaenda chuo.. nakumbuka niliandaa matokeo ya wanafunzi wa kidato cha pili nikayaweka kwenye wastani na madaraja (division). Mkuu wa shule akaniambia hiyo haifai yabadilishe kwenye report form isome wastani tu. Mambo ya division hadi form four. Nikashangaa sana na ninakumbuka waalimu wazoefu walinicheka na kusema TULIKUAMBIA. Miaka kadhaa mbele NECTA wanatoa matokeo ya form II kwa division. Kama lile wazo lingechukuliwa tungekuwa mbali sana ila kwa sababu ndo kwanza nilikuwa mdogo wa umri miaka 20 kasoro nikapuuzwa.
Ungekuw mbali kww kubadilisha wastan wa matokeo kwa devision format
 
Kuna jamaa nilimaliza nae darasa la 7, akashindwa kuendelea sekondari sababu ya maisha. Jamaa akaingia kwenye kazi za kuchimba madini tena locally na sululu tu nyundo majembe. Miaka minne baadae akiwa na miaka 21 akapata dhahabu akapata milioni 50 mi hapo nipo form 4. Akanunua trekta akaenda Kiteto akajichimbia kwenye kilimo huku akikodisha trekta. Baadae mi namaliza Chuo jamaa anamiliki pesa si chini ya milioni 400 akiwa 26yrs nilikutana nae nilimshangaa sana. Mpaka Sasa anamiliki nyumba nyingi sana mikoa tofauti.
mbona kawaida sana....་
 
Kauli hii inayotrend imenifikirisha Sana wakati mwingine nikidhani nikweli!

Embu tutazame Jambo hili kwa Tanzania kijana kuwa tajiri labda mwenye Umri wa Under 30yrs amiliki angalau 100M Jambo hili linawezekana? Je, mifumo na mazingira yanawezesha?

Bila kutarajia vilivyotajwa kwenye kichwa Cha mada hii?
Kwa hiyo, kwa mawazo yako, sisi tunaomiliki 100m ni matajiri?
Au ili mtu aitwe tajiri anatakiwa amiliki pesa kiasi gani?
 
Kuna jamaa nilimaliza nae darasa la 7, akashindwa kuendelea sekondari sababu ya maisha. Jamaa akaingia kwenye kazi za kuchimba madini tena locally na sululu tu nyundo majembe. Miaka minne baadae akiwa na miaka 21 akapata dhahabu akapata milioni 50 mi hapo nipo form 4. Akanunua trekta akaenda Kiteto akajichimbia kwenye kilimo huku akikodisha trekta. Baadae mi namaliza Chuo jamaa anamiliki pesa si chini ya milioni 400 akiwa 26yrs nilikutana nae nilimshangaa sana. Mpaka Sasa anamiliki nyumba nyingi sana mikoa tofauti.
Safi sana
 
Back
Top Bottom