Aliyesema hivyo ni mpumbavu sana na maskini wa kifikra. Siasa za ujamaa na kujitegemea ziliharibu sana fikra za watu na kudhani utajiri ni dhambi. Hadi nyakati hizi kwenye kampeni za uchaguzi wagombea hufanya maigizo kwamba wao ni maskini tu kama wapiga kura. Wapiga kura nao kwa kutaka kampani ya umaskini huishia kuwapigia kura wagombea wa aina hii. Tanzania utakuta mtu kama Fred mwenye umri wa zaidi ya miaka 35 anaitwa tajiri kijana wakati dunia ya leo ina mamilionea wenye miaka chini ya 25. Fikra kama hizo ndo zimefanya nchi kuendelea kupoteza pesa kwenye miradi kama BBT kwa kudhani kuna utajiri wa vikundi badala ya kuwawezesha vijana ambao tayari wako kwenye kilimo. Umaskini ni fedheha, tuukatae. Utajiri sio dhambi wala uhalifu.
Wazee wetu wengi hawataki kabisa changamoto mpya toka kwa vijana. Mimi niliwahi kuwa mwalimu wa sekondari kwa miezi kadhaa kabla sijaenda chuo.. nakumbuka niliandaa matokeo ya wanafunzi wa kidato cha pili nikayaweka kwenye wastani na madaraja (division). Mkuu wa shule akaniambia hiyo haifai yabadilishe kwenye report form isome wastani tu. Mambo ya division hadi form four. Nikashangaa sana na ninakumbuka waalimu wazoefu walinicheka na kusema TULIKUAMBIA. Miaka kadhaa mbele NECTA wanatoa matokeo ya form II kwa division. Kama lile wazo lingechukuliwa tungekuwa mbali sana ila kwa sababu ndo kwanza nilikuwa mdogo wa umri miaka 20 kasoro nikapuuzwa.