Ukipata milioni unaila siku tatu, ikibaki elfu kumi unaishi nayo week. Hii kitaalam mnaiitaje?

Ukipata milioni unaila siku tatu, ikibaki elfu kumi unaishi nayo week. Hii kitaalam mnaiitaje?

Mathayo 6 (Biblia Takatifu)
Β―Β―Β―Β―Β―Β―Β―Β―Β―Β―
¹⁹ Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;
²⁰ bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;
Β²ΒΉ kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

…
²⁴ Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
²⁡ Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
²⁢ Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?
²⁷ Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
²⁸ Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti
²⁹ nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.
³⁰ Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
Β³ΒΉ Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?
Β³Β² Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
Β³Β³ Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.
³⁴ Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Haya maneno Bwana Yesu aliwaambia wanafunzi wake (sio Makutano). mwanafunzi wa Yesu ni yule aliyezaliwa mara ya pili kwa maana ya kuokoka. Ni mtu ambaye Mungu ni Baba. mahusiano na Mungu ni BABA na MWANA. Kila mtu ni mtu wa Mungu, ila sio kila mtu ni mtoto wa Mungu.

hivyo haya maneno ya Bwana Yesu hapo sio ya kila mtu, ni kwa wale waliozaliwa na Mungu katika Roho.


JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Hivi hii huwa ni hali ya kawaida au kuna namna? Huyu jamaa yangu akishaishiwa anatia huruma sana na kujiapiza hatorudia kutumia pesa vibaya ila akipata pesa kidogo anarudi kule kule, huwa namuonea sana huruma hasa kwa future yake kama ataendelea kuwa hivyo. Hawezi kukaa na hela kabisa.

Kamari iliwahi kunitesa sana nilikuwa siwezi kukaa na hela ila nikafanikiwa kutoka huko nnaweza kuwa na laki kwenye simu na ikakaa hata mwezi mzima sijaigusa jambo ambalo lilikuwa ni mtihani mgumu sana kwangu.


Ni tabia ambayo inabidi muhusika aamue na kudhamiria kubadilika.
Wengi tunajifunza Kwa maumivu makali sana lakini sio rahisi ila inawezekana.

Pesa inahitaji discipline na Ina kanuni zake, ukizifuata hizo kanuni haikutupi. Itakuheshimu
 
Ni tabia ambayo inabidi muhusika aamue na kudhamiria kubadilika.
Wengi tunajifunza Kwa maumivu makali sana lakini sio rahisi ila inawezekana.

Pesa inahitaji discipline na Ina kanuni zake, ukizifuata hizo kanuni haikutupi. Itakuheshimu
Hakika mkuu nachokiona kwa jamaa kama ana nia ya kubadilika ila kuisimamia nia yake ndio changamoto kwake hasa akishapata hela.
 
Hakuna gari la laki 1 kula mbavu za kitimoto na bia wewee
πŸ˜‚ kuna waliowahi kusema hivyo sahivi wanajutia.

Mzee wangu aliwahi niambia miaka hiyo anaitiwa maeneo ya kununua kimara alipuuzia na kusema nani anunue pori, hela akaweka heshima bar kuna rafiki yake alinunua akatulia kaja kuuza kwa sasa anaponda raha za uzeeni. Kupanga ni kuchagua.
 
Hivi hii huwa ni hali ya kawaida au kuna namna? Huyu jamaa yangu akishaishiwa anatia huruma sana na kujiapiza hatorudia kutumia pesa vibaya ila akipata pesa kidogo anarudi kule kule, huwa namuonea sana huruma hasa kwa future yake kama ataendelea kuwa hivyo. Hawezi kukaa na hela kabisa.

Kamari iliwahi kunitesa sana nilikuwa siwezi kukaa na hela ila nikafanikiwa kutoka huko nnaweza kuwa na laki kwenye simu na ikakaa hata mwezi mzima sijaigusa jambo ambalo lilikuwa ni mtihani mgumu sana kwangu.
Asilimia mia moja ni kujiendekeza tu...hamna lolote...

sijawahi kucheza kamari yeyote ile kwa zaidi ya miaka kumi na tano mpaka sasa,...
Situmii kilevi chochote kile kwa zaidi ya miaka mitano sasa...

Nikiwa najitafuta migodini, rafiki zangu walikuwa wanashangaa nawezaje kwenda kugonga nyundo maporini huko, ilihari nina zaidi ya million kwenye account yangu..wakati huo na mimi nawashanga WANASHINDWA NN...
kifupi wengi hawana ndoto kubwa,na walionazo hawawezi kujitoa muhanga vya kutosha ili kutimiza ndoto zao,wapenda sifa za kijinga zinazodumu kwa siku moja na kisha kuyeyuka kama barafu tu,na ndio sababu kama umechunguza vizuri watu wengi wakishajenga kanyumba tu ka kulaza mbavu, hata jitihada za utafutaji au uwekezaji zinapungua, akinunua kipikipiki au kigari basi kamaliza kila kitu..kinachobaki ni kujitamba huko bar, vijiweni na kwenye mitandao ya kijaamii.....

mtu ambaye akipata pesa kidogo hakamatiki, wala hashauriki na zikiisha ndo anatia huruma na kuwa msikilizaji mzuri na kuapa kuto kurudia kwingi, kamwe usimsaidie kwa kumpa pesa, anapolia njaa mkumbushe juu ya kutapanya kwake pesa kipindi alipopata kilaki moja...
 
Tumia pesa ikuzoee Mnyampaa.

Pesa Ina kanuni na taratibu zake, haijalishi una Elimu Gani ukizifuata, haitakuangusha.

Kama hauna mipango na malengo, utafanya chochote unachomudu Kwa pesa uliyonayo Kwa wakati huo.

Mwisho wa siku, pesa hua haitoshi, ni wewe kuamua ukipata, ifanye vitu gani vya muhimu.

Kuna mtu akiwa na 1M haujui, akiwa na 10k haujui, Yuko vilevile. Lakini mwingine alipata 50k siku hiyo hamnywi maji, ni fujo za hatari. Mtu wa aina hiyo hata umpatie pesa kiasi Gani, atatapanya tu.

Kutafuta na kupata pesa ni jambo Moja, kuitunza ikaongezeka ni kitu kingine kabisa na sio Kila mtu anaweza.
Maelezo yamejitosheleza
 
Back
Top Bottom