Ukitaka kujua nchi hii ina wenyewe, uliza tenda zote za mabilioni za huduma kwenye mradi wa bwawa la Nyerere nani walipewa!

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
12,699
Reaction score
22,598
Ninaangalia hapa list ya wale wote waliopewa tenda za kutoa huduma kwenye mradi wa Nyerere nabaki kutikisa kichwa tu. Tenda hizi zilikuwa ni za mabilioni na kwa ajili ya ku-supply kila kitu, kuanzia chakula, vifaa, huduma nk. Sana sana ulinzi ndio naona walipewa Suma JKT. Naona majina hapa ya mbunge huyu yupo mkoa jirani, halafu mke wa aliekuwa raisi, mawaziri nk!

Huenda mtu akaona kama hili sio tatizo. Ni tatizo sana, maana hawa wote wenye hizi tenda wana connection ya kuweza ku-influence uamuzi juu ya mradi. Kwa mfano, waliweza ku-influence mradi uchelewe kukamilika ili waendelee kutoa huduma za tenda zao.

Hii haitakiwi kabisa, inaitwa conflict of interest. Mtakumbuka suala la ucheleweshaji wa mradi lilipohojiwa kulitolewa majibu mepesi sana, ambapo kikawaida mkandarasi alipaswa kuwajibishwa lakini haikuwa hivyo, kwa sababu kuchelewa kwa mradi kulikuwa na manufaa kwa hawa wenye tenda, na hawakujali kuongezeka kwa gharama za mradi.

Kweli nchi hii ina wenyewe, na ndio maana ukitaka kuwaondoa kwenye hiyo himaya yao watakuwa tayari hata utekwe na kupotezewa!
 
Kama list unayo na hujaweka hii post yako inakuwa ni kama umbea tu.
Basi acha iwe hivyo, maana hilo ndilo tatizo la Watanzania, wana upofu wa kutoona uovu na siku zote wataita umbea. Hata vyombo vya dola kuhusika na utekaji ni umbea tu, kwani hujui?

Na pia nimesema uliza. Na wewe una haki kumwambia mbunge wako akaulize Bungeni.
 
serikali haikuwa na mamlaka za kutoa tenda hizo , za watoa huduma wa kumuhudumia mkandarasi wa mradi ,, Mtoa tenda za subcontractor alikuwa ni mjenzi ambaye ni Arab Contractor. Yeye ndie aliekuwa analipia huduma hizo na wala sio serikali.

Hivyo hao unaowataja kwenye hiyo list waliletwa kazini na Arab Contractor na wanalipwa na Arab contractor.

Kuhusu swala la muda ni uongo pia kwamba hili bwawa lingekamilika kwa miaka mitatu. Maana kuna muda wa kupisha zege likauke lishikane. Ndio hatua ingine ifate.

Nioneshe bwawa lolote la umeme kubwa la kuzalisha megawatts zaidi ya 1000 yaani GW ambalo limekamilika chini ya miaka mitano.

Canada wanajenga bwawa la Mw 1100 ila lina miaka 8 sasa bado halijaisha.

Ethiopia wamejanga bwawa lao la umeme kwa miaka zaidi ya 10 bado halijaisha.

Uganda wanajenga bwawa la umeme la MW 600 Karuma Hydroelectric Power Station limeanza kujengwa Toka mwaka 2013 mpaka leo 2024 bado halijaisha.. miaka zaidi ya 10 imepita

Tanzania tunalikimbiza sana bwawa tupewe pongezi kwa tulipofikia. Bwawa la Megawatts 2100 sio kazi ndogo
 
Basi acha iwe hivyo, maana hilo ndilo tatizo la Watanzania, wana upofu wa kutoona uovu na siku zote wataita umbea. Hata vyombo vya dola kuhusika na utekaji ni umbea tu, kwani hujui?
Bro wewe ni platinum member ila unafanya mambo ki amateur sana. Yani unaandika kuwa "unaangalia list" halafu ushindwe kuweka hiyo document hapa watu tuione?

Halafu tunaotaka ushahidi unasema eti ndio shida ya watanzania.

Anyways miafrika ndio mlivyo. Wenzetu wakipataga documents za hivyo huwa zinakuwa leaked fasta ku expose uozo ila wewe umeikalia halafu unalaumu eti ndio tatizo la watanzania.
 
Hajiamini, ametumwa na info nusu nusu
 
Weka na majina kabla mods hawajaona na kufuta Uzi tutakuwa tumesha ya save
 
Wewe amini hilo utaamini kila kitu, pamoja na maamuzi ya Polisi. Tenda zilikuwa chini ya usimamizi wa Tanesco
 
Tanesco ana mamlaka gani ya kumletea arab contractor mpishi ?

Je hao subcontractor walikuwa wanalipwa na Tanesco ?
Angalia mkataba wa serikali na Arab contractors. Arab contractors kazi yake ni kujenga mradi tu. Kwa mfano, Arab contractors hawakuingia mkataba wa huduma ya chakula kwa wafanyakazi waliokuwepo pale, karibu 12,000. Bill ya chakula ilizidi Tshs 200m kwa wiki. Arab contractors hawakuingia mkataba na SUMA JKT kutoa ulinzi. Lakini Arab contractors waliwasub-contract Sino company ya China kujenga ukuta wa bwawa, sio Tanesco. Arab contractors hawakuwa na mkataba na kampuni iliyo maintain barabara ya kwenda kwenye project kwa njia ya Kibiti

Kwa hiyo mikataba ya huduma yote ilikuwa ya Tanesco, na ndio maana ikaenda kwa wenyewe. Mfano, Arab contractors hawakutaka kabisa watu kunywa bia eneo la mradi, na ukizingatia uislamu wao. Lakini Tanesco ilikuja kuingia na kigogo mwingine kujenga baa kambi zote za mradi, na hili liliwaudhi sana Arab Contractors.
 
wewe ni muongo

Joint venture ya Arab contractor na el sewedy electric ndio imelipwa zaidi ya trilioni 7. Kwa ajili ya kazi ya bwawa rufiji

Na arab contractor ndie aliempa tenda sinohydro.. ila sio Tanesco.

Sinohydro hajalipwa hata mia na tanesco. Na wala hamjui tanesco kwenye kazi ya rufiji. maana Sinohydro ni subcontractor wa mjenzi ambaye ni arab contractor
 
Wewe mjinga nini, mie nimesema nini hapo juu? Kumbe hujui hata kusoma?

"Arab contractors hawakuingia mkataba na SUMA JKT kutoa ulinzi. Lakini Arab contractors waliwasub-contract Sino company ya China kujenga ukuta wa bwawa, sio Tanesco."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…