Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Ninaangalia hapa list ya wale wote waliopewa tenda za kutoa huduma kwenye mradi wa Nyerere nabaki kutikisa kichwa tu. Tenda hizi zilikuwa ni za mabilioni na kwa ajili ya ku-supply kila kitu, kuanzia chakula, vifaa, huduma nk. Sana sana ulinzi ndio naona walipewa Suma JKT. Naona majina hapa ya mbunge huyu yupo mkoa jirani, halafu mke wa aliekuwa raisi, mawaziri nk!
Huenda mtu akaona kama hili sio tatizo. Ni tatizo sana, maana hawa wote wenye hizi tenda wana connection ya kuweza ku-influence uamuzi juu ya mradi. Kwa mfano, waliweza ku-influence mradi uchelewe kukamilika ili waendelee kutoa huduma za tenda zao.
Hii haitakiwi kabisa, inaitwa conflict of interest. Mtakumbuka suala la ucheleweshaji wa mradi lilipohojiwa kulitolewa majibu mepesi sana, ambapo kikawaida mkandarasi alipaswa kuwajibishwa lakini haikuwa hivyo, kwa sababu kuchelewa kwa mradi kulikuwa na manufaa kwa hawa wenye tenda, na hawakujali kuongezeka kwa gharama za mradi.
Kweli nchi hii ina wenyewe, na ndio maana ukitaka kuwaondoa kwenye hiyo himaya yao watakuwa tayari hata utekwe na kupotezewa!