Ulichoonge ni makosa ilibidi ufanye research kisawasawa .
Ingekuwa Uislamu ndio imechangia hayo ungefanya tafiti je Uislamu unasemaje kuhusiana na hayo ?
Mfano mzuri angalia Uarabuni ulipotoka Uislamu je , Wanawake wao wapo kama kina Mwajuma na Ashura wa bongo ? wakati huko ndipo Uislamu umekolea kama Wanawake kuwehuka huko si ndipo ilibidi wawe zaidi ya bongo ?
Vipi Wanawake Waislamu wa Uchagani , Mbeya wapo sawa na wa Dar au Mtwara ? kwa nini usingechunguza Influence ya kimazingira , tamaduni , makabila nk kuchangia hayo kuliko kuangalia dini pekee ? ukiacha mambo ya dini makabila ya Pwani yanatamaduni zao za hovyo za mambo ya kuendeleza ngoma toka enzi ..
Mfano baadhi ya jamii za Wakiristo Wakurya nk wanakeketa na kupiga sana Wanawake je , itakuwa sawa kuhusisha Moja kwa moja na Ukiristo bila kuangalia engo nyingine mfano Mila na desturi ?