Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

Binafsi kama ni muislam na unanijua na nakujua basi kutopata hiyo shkamo ni mwendo wa asalam alaykum,au habari za saizi only,hata wazee wangu wanaipata kwa tabu mnoo na soon naelekea kuikata hii salam ya shkamoo.nimepiga marufuku nyumban hii salam kwangu.
 
Ukiwa na pesa we tajirii oh hata usipo sema shikamoo wazee watakupa na kushangiliwa kwa maneno matamu na utaamkiwa tu hadi na hawa wazee hataa kama mdogo huna mvii ndiyo ujue pesa mwanaharamu😅
 
Kuna wazee yani Shikamoo kwao ndiyo umemuheshimu na usipoitoa utasikia kijana ehhh vipi hapo anaanza kuiitafuta kwa nguvu shikamoo sasa utasikia kwahiyo tunalingana siku hizi umeota mapembe vijana wa siku hizi ni wa hovyo sana nyie,ila kama pesa ipo hizo sio lawama tena zinaenda na sifa zako juu yake😅
 
79 si una miaka 45 tu? Mbona kama mvi zimekuja mapema sana?

Mimi principle yangu ninayotumia kama MTU huna uwezo was kunizaa, sikuamkii shikamoo, maana unaweza kuta watu umewazidi umri shikamaoo, (au wanafikiri umewazidi umri wakakushangaa)
45 mdau ana mvi kwa dunia ya sasa ni kitu cha kushangaza?ninawajua madogo kwenye 20s wanapaka Ile wanaita piko.

Nahisi ni aina ya vyakula tunavyotumia inaleta hii shida
 
Hao wazee wamedataka kweli

Aisee umesema kweli huwa smtm inatokea unamfanyia mtu tathimini ya haraka kujua huyu wa kuamkiwa au laa!

Hawa wakoloni wajinga sana aisee,wametupa salamu ya hovyo sana
 
Kuna wazima ukiwasalimia 'habari za saa hizi' wanaona hujawatendea haki; kwamba dharau. Walipaswa kuamkiwa 'shikamoo'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…