Ukiwa Mtu Mzima Utagundua Kwamba Salamu Ya Shikamoo Ni Mtihani

"Mimi tangia zamani huwa nasalimia hivi"

"Habari ya uzima " hii salamu nilianza kuitumia chuoni baada ya kupata rafiki mlokole.

Kwanza inapendwa Sana hii salamu Sana na ukimsaimia MTU anakuona upo na maadili kwake
 
Hakuna kitu ambacho sipendi kama kusalimiwa shikamoo yaani sipendi.
Na mimi pia huwa sisalimii kabisa watu hiyo salamu.
Hadi nione kabisa mtu kazeeka kabisa kajichokea anaenda kuwa babu au bibi yaani kifupi kasha jikubali kuwa ni mzee ndio nasalimia.
 
Salamu ya habari ni nzuri zaidi kwa mtu usiemjua, hiyo shkamo salimia wakubwa unaowajua wenye umli sawa na mzazi wako, lakini mnaokutaka just say to hello, hi, habari, za saa hivi full stop. Me watoto angu wote kusalimia shkamo ndo walishashindwaga kitambo, labda mzazi, bibi, babu, aunty, uncle that ok
 
Hahaha hii inanikuta mimi kuna mda nawasalimia wadogo zangu kabisa siku hizi watu wanakua haraka sana hasa wanawake hahahaha kuna profesa mmoja nikimuamkia shikamoo haitikii na madam flani ivi alikua mwalimu wangu wa kozi hahah
 
Nasalimia kwa unyenyekevu sjui so far naonekana na heshima sana kumbe kawaida tuu πŸ˜‚
Haaahaa πŸ˜† ☺️ kuna siku Kuna ka brother kangu kana MWILI mdogo mdogo sikuwai kuonana nako tangia nikiwa mdogo.

Siku moja nikawa nimeenda kinyerezi nikamkuta kavaa jezi yake yupo na brother angu mmoja nikasalimia habari za leo kajamaa kakagoma kakasema nikape shikamoo tukalumbana nikakasalimia kwa shingo upande.

Baadae ndio brother mwingine AKAJA aka ni introduce kwake ni brother mkubwa na ana wadhifa kubwa tuu mpaka NIKAONA AIBU Ila Kuna watu Wana miili midogo midogo mpaka wanaweza kunyimwa kiti ugenini πŸ€“
 
Kuna kipindi niliamkia sana makinda huko kanda ya ziwa. Siku moja mama mmoja akasema kijana wangu nakuona unaamkia sana wadogo zako hata kama unataka kuoa usukumani usifanye hivyo. Nisilikia aibu sana tangu siku hiyo hadi leo salamu yangu kubwa ni habari.

Na nikikutana na mtu simuelewi naanza kwa kuchangamsha maongezi bila salam. Isitoshe wengi siku hizi hawaipendi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…