Ukiwa na EV, kwa umeme wa elfu 40 unatoka Dar hadi Dodoma, na kurudi tena Dar!

Hapo kwenye viatu 😅😅 mie naendesha nikiwa PEKU kbs.. ndio nakuwa huru.. yaan nikipand tu ktk gari navua viatu naweka pembeni.
 
Si rahisi kama mnavodhani zile zinahitaji uelewa wa Power electronics
 

Utazoea tu Mkuu. Kama nilivyoeleza awali, Kwa mjini, ka Toyota Aqua kanakidhi mahitaji. Ila Sasa Kuna wakati unataka ufanye mambo, unakumbuka uwezo wa gari unakua mpole.

Kwa miundo mbinu yetu, hasa charging stations na upatikanaji wa mafundi/vifaa, Bora hybrid kuliko Full EV, ili hata mfumo ukisumbua, haupati shida sana.

Kwa uzoefu wangu, hybrid ikitokea mfumo wa umeme umesumbua, inakunywa mafuta balaa
 
Tatizo hizo gari hazina mwendo,wabongo tunapenda kupeleka moto.
Unaongelea kitu gani mzee🤣 sio kwa Tesla! Tesla zinatembea mno tena zina quick launch ya ndani ya sekunde 3!

Yani ticks tatu za mshale wa sekunde kwenye saa mtu anakuwa ameshafikia speed ya kilometer 100 kwa saa!

Yani mfano mtu akiwa mataa ya ubungo anaelekea mwenge, taa zitakaporuhusu akiikanyagia gari anafika njia panda ya chuo pale akiwa speed 140 kitu ambacho kwa gari zetu nyingi za petrol hakiwezekani.
 
Yeah baada ya kilometa atleast 400,000 unatakiwa ubadirishe battery. Itakua imepungua range.
Sasa kilometre laki 4 hadi ifike kwa safari za kazini na nyumbani ni leo? Si almost miaka 20 mbeleni huko. Tuache uwoga mwanzo ilikuwa tunaogopa magari ya mzungu ila naona yule jinamizi tulimvua. Sahizi gari mchanganyiko tu ukienda Masaki, Msasani, Oysterbay unaweza hisi upo Frankfurt ujerumani 🤣
 
Sasa kilometa 400,000 ni leo? Mimi nimenunua gari 2017 na ninaitumia kila siku kwa mizunguko yangu ya mjini. Niliinunua na km 67,000 leo iko 138,000.

Kilometa 400,000 ni miaka angalau 10 - 15 kwa matumizi ya kawaida.
Na gari za umeme zitakuwa kama appliances tu. Yani kama ambavyo tunabadili simu ama TV. Ikitoka mpya unanunua unaachana na la zamani.
 
Hakuna IST ya kwenda Dodoma kwa mafuta ya 70k
 
Niliona siku nikajua anazingua tu, alikua na Toyota BZ4x EV. View attachment 3090326
Toyota ujanja mwingi ila kwenye EV anaogopa. Wajapan wote EV wanaingia kwa mguu nusu, wengi wanashirikiana na Mchina kufanya maajabu sio wenyewe.
Mjapan sifa yake kubwa ni kuwa risk-averse kibiashara. Hapendi kujaribu kitu kipya kama hana uhakika, na akianza kitu ujue amejiridhisha. Hivyo sio innovators wakubwa kivile lakini wanatendea haki proven tech.
 
Tatizo serkali yetu ina roho mbaya. Kingine ni hatuna mafundi
Mkuu hata sisi pia
Mtu anamtuma mwanae kwenda kusoma nje kwenye vyuo vinavyotambulika
Ila hakuna anaewaza future kabisa
Wao wanawaza akirudi anaajiriwa badala ya kujiajiri
Leo angalia magari mangapi yenye majina makubwa mafundi wameshindwa kuyatengeneza na kuishia garages
Wanasema wenyewe wameyatelekeza ila sidhani una afford kununua Range au BMW eti hukuwaza service zake

Vijana wangejituma na kwenda nje kusomea utengenezaji wa kila gari
Siku hizi kuna car diagnostic unachomeka inakupa kila kosa
Hivi kuna Hybrids zimeingia kwa wingi au mafundi tatizo?

Walahi nilipeleka Benz langu garage moja huku nje
Yaani nimekuta garage kama Hospitali
Marumaru kuta nyeupe na hata mechanic kavaa koti jeupe
Ila ni kama anafanya operation
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…