Ukristo na Uislamu ni Dini mbili zisizofanana kabisa

Utume wa Musa ni karne nyingi sana, haikuwa rahisi kugundua moja kwa moja kama ni yeye ndio aliandika au watu aliokuwa nao
Sasa kama ilikuwa ngumu, kwanini yanafanyiwa kazi maandiko yake na huku mnajua wazi ya kuwa hakuna hakika yake ?
 
Mhaya , Uko vizuri sana
 
Hakuna uthibitisho wa kutokuwepo Mungu kwa vile Hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Huu ni uthibitisho tosha kwamba hayupo.

Ukiweza thibitisha yupo.
Hivi huwa unaelewa unachokiandika ? Unajua kama hakuna maana ?

Kitu ambacho hakijawahi kuwepo wewe unakijuaje ? Hivi una akili kijana ? Kisome ulicho kiandika uone kama kina maana.

Usiniambie nithibitishe ya kuwa hayupo wakati wewe umeshindwa kuthibitisha kutokuwepo na kutuambia unajuaje kutokuwepo kwa kitu ambacho hakijawahi kuwepo. Hivi unafikiri unachokiandika ?

Ili ujue kutokuwepo kwa kitu lazima kutanguliwe na kuwepo kwake au ujue kwa hakika kabisa ya kuwa hicho kitu hakipo.

Sasa wewe vyote huna. Halafu unakuja kuandika ujinga na utoto. Tetea hoja yako sio maneno matupu.
 
Wewe ndio huna akili unasema kitu kipo halafu huwezi kuthibitisha kipo?

Ukishindwa kuthibitisha kitu kipo ni kwamba hakipo.

Usicho elewa ni nini?

Wewe unasema Mungu yupo halafu huwezi kuthibitisha kwamba yupo?

Una puyanga puyanga tu kama mtu aliyerukwa akili.
 
 
Nimecheka sana, kuthibitisha uwepo wa Mungu ni jambo rahisi sana na jepesi mno. Na muda wowote nalifanyia.

Wewe soma ulichokoandika kisha uonyeshe kama kina maana, ukiweza kuonyesha ya kuwa kina maana, Mimi naacha kujadili huu mjadala.

Unapojenga hoja hakikisha unaweza kuitetea, huwezi kusema eti ushahidi au uthibitisho wa kuwa Mungu hayupo ni sababu hajawahi kuwepo ? Sasa swali linakuja kitu ambacho hakijawahi kuwepo wewe unajuaje kama hakipo au umekidiriki vipi ? Unaruka ruka.

Ili uone kati yangu Mimi na wewe nani anapuyanga, ni wewe ujibu maswali niliyokujibu kuuliza.
 
Qur'an imeandikwa miaka 100 toka kufariki mtume 😂.

Unaweza kuthibitisha hiki
 
Ukishindwa kuthibitisha kitu kipo ni kwamba hakipo.
Kushindwa kuthibitisha kitu kipo ni kwamba hakipo. Hii akili ya wapi kijana ? Yaani Falsafa na Logic zinawafanya muwe wavivu sana kufikiri.

Kushindwa kuthibitisha uwepo wa kitu Kuna sababu kadhaa miongoni mwa sababu ni kutokuwa na elimu juu ya kitu husika.

Lakini Kuna vitu vingine uwepo wake ni lazima, na unajithibitisha wenyewe. Mfano uwepo wa simu, unathibitisha uwepo wa Msanifu wa simu hiyo.

Sasa unaposema Mungu hayupo kwa sababu hakuwahi kuwepo, ho sentensi Haina maana. Sasa unajengaje hoja kwa kitu ambacho hakina maana ? Huu ni uzwa zwa.
 
Ni sawa Kuwa watu wawili wanaweza kuwa Jina zaidi ya Moja?
Au hilo unabisha?
Ndio inawezekana kuwepo watu wawili tofauti kabisa wenye jina linalofanana... Kitu kinachofanya watu hawa wawili kusemekana kuwa ni mtu mmoja ni kufanana kwa matukio au historia yao... Ila wasipofanana tu matukio basi hao sio mtu mmoja... Mfano Yesu na Issa ni watu wawili tofauti kabisa kwa sababu historia zao hazifanani.

Kwenye Biblia kuna watu wamekosewa mara nyingi sana Unakuta kwenye Agano jipya baba yake kaandikwa jina jingine na kwenye agano la kale baba yake jina jingine...
Taja hayo majina yaliyokosewa kwenye biblia. Au leta huo mfano

Hakuna Mtu aliyekuwa akiitwa Yesu na wala kwenye Majina ya kiyahudi hakuna jina Linaloitwa Yesu.
Yesu ni tafsiri tu ya kiswahili
Jina "Yesu" ni tafsiri ya Kiswahili ya jina la Kigiriki "Ἰησοῦς" (Iēsous), ambalo lenyewe ni tafsiri ya jina la Kiebrania "ישוע" (Yeshua) au "יְהוֹשֻׁעַ" (Yehoshua), linalomaanisha "Yahweh anaokoa" au "Yahweh ndiye wokovu."

Kama ilivyo kwa majina mengine ya kiebrania yaliyotafsiriwa kuja kiswahili kama Yohana, Musa, Petro na mengineyo. Kitu pekee kinachofanya jina hilo kudhiriisha huyo mtu ni mfanano wa historia na matukio yao
Sarai mkewe Abramu akamtwaa Hajiri Mmisri mjakazi wake, baada ya kukaa Abramu katika nchi ya Kanaani miaka kumi, akampa Abramu mumewe, awe mkewe."
Hajiri kipindi anaolewa alikuwa bado kijakazi, na hata hakupata haki zote kama mke. Hata mtoto wake hakufanywa mwana mkuu machoni pa Ibrahim badala yake Mke wake Sarah baada ya kuzaa ndio isaka akafanywa mtoto mkuu machoni pa baba.

Waislamu wao wanaelezea historia ya Ibrahim na Ismail katika muktadha tofauti. Na kufanya watu hawa wasifanane na wa kwenye biblia. Historia ya Abrahim wa biblia na Ibrahim wa Quran inaelezea watu hawa katika utofauti hivyo hawawezi kuwa mtu mmoja
 
Kwanini unaandika Uongo ?

Tuwekee tatizo Moja tu la kiuandishi ambalo lipo katika Qur'an.

Unaposema iliandikwa au kukusanywa, hapa umeonyesha wazi ya kuwa Qur'an huijui. Qur'an imeandikwa yote na kukamilika hata Mtume hajafa. Alivyo kufa Mtume ndio ikakusanywa na haikupita hata miaka 20. Hii miaka 100 umeipata wapi ?
 
kumbe biblia sio maneno ya yesu!...ahsante mkuu
 
wakati Biblia ilikuwa imekamilika au baadhi ya vitabu vyake viliandikwa miaka 30-40 baada ya Yesu kupaa. N walioandika waliishi naye;
Kitabu kiliandikwa ndani ya miaka hiyo.

Kisha utuambie hao walio andika ni kina nani na je walimuona Yesu ?
 
kumbe biblia sio maneno ya yesu!...ahsante mkuu
Wakristo Wana Historia tu na maisha ya Yesu ila hawana matini ya neno kwa neno ya Mafundisho ya Yesu.

Halafu walivyo pewa mtihani hawana muda wa kuyahakiki maandiko yao na kujua yapi sahihi na yapi sio sahihi. Wame kaa kaa tu.
 
Samahani Mkuu Unajua maana Ya Torati au Torah?
Kama unajua nadhani hautakuwa na shaka mtu akisema Musa alipewa Torati..
Katika ukristo torati ni kitabu kinachomuelezea Musa.... Musa wa biblia na musa wa Quran ni watu wawili tofauti....

Quran haielezei Amri kumi za MUNGU ambazo ni nguzo za ukristo. Mikasa inatofautiana uwezi kusema mtu huyo ni mmoja kaka
 
Sasa kutokuijua ni jambo la mtu binafsi. Wewe Biblia unaijua au Wakristo wote wanaijua Biblia ?

Sababu hii ni elimu, lazima utoe juhudu kutaka kuijua ndio unaijua ukizembea huwezi kuijua.
 
Wakristo Wana Historia tu na maisha ya Yesu ila hawana matini ya neno kwa neno ya Mafundisho ya Yesu.

Halafu walivyo pewa mtihani hawana muda wa kuyahakiki maandiko yao na kujua yapi sahihi na yapi sio sahihi. Wame kaa kaa tu.
Mud aliwapiga fix mkajaa
 
Quran haielezei Amri kumi za MUNGU ambazo ni nguzo za ukristo. Mikasa inatofautiana uwezi kusema mtu huyo ni mmoja kaka
Nani aliwaambia ya kuwa amri kumi za Mungu ni nguzo za Ukristo ?

Shida yenu Ukristo ni dini isiyo kuwa na misingi yenyewe haikamiliki mpaka itumie maandiko yasiyo wahusu. Mfano wa kumbukumbu la Taurati. Taurati haikuletwa kwa Wakristo sababu Mpaka Yesu anaondoka hapakuwa na Ukristo duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…