Ukristo na Uislamu ni Dini mbili zisizofanana kabisa

Okay nilitaka kukujibu kwa hoja ila umemaliza vizuri..tuendelee kuishi na imani zetu maana hata hizi dini ni tofauti na imani za mababu zetu ni vile hatujui tmetupwa kwenye uwanja wa masbindano tusiyoyajua ila imani zetu ndizozitatuokoa kutoka katika vita na mashindano ya mataifa.
Niwaachie quiz ndogo but very wide
"Kwanini dini zimetoka kwa mataifa ya wazungu na kwanini sio taifa moja mean urabuni islam and European Christ?"
 
Wewe umeweza kuthibitisha Mungu yupo?

Unabaki kusema Mungu yupo ilhali wewe mwenyewe hujathibitisha Mungu yupo?

Unataka mimi nithibitishe Mungu hayupo ilhali wewe umeshindwa kuthibitisha yupo!

Hivi wewe unafikiri sawasawa kweli?

Nakwambia hivi ukishindwa kuthibitisha kwamba Mungu yupo, Ni kwamba hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Ninyi wavaa kobazi mna matatizo ya akili.
 
Ina maanisha kila mtu aliyejisikia aliandika biblia?na haiwezi kuwa ni maneno ya mungu
Tuanzie hapo kwanza.... Kwani unamaanisha nini ukisema "Maneno ya Mungu"

Neno la mungu ni ujumbe wowote kutoka kwa Mungu kupitia kwa mtu yeyote.

Biblia iliandikwa kwa uwezo wa Roho mtakatifu kupitia manabii na wanafunzi wa yesu na wafuasi wake. Na maneno hayo hayakutungwa tu, bali yalishuhudiwa na watu... Nimekupa mfano Agano Jipya linakitabu cha Luka, Mathayo, Yohana ambao wote wameandika vitabu vyao lakini vinafanana maandiko... Ingekuwa kila mtu kajiandikia tu si maandiko hayo yanatofautiana!
 
Acha uongo
 
Wewe ndio umepotoka.... Injili ya yesu agano jipya imeandikwa na Mathayo, Luka na Yohana ambao kimsingi ni wanafunzi wa Yesu na walikuwa nae nyakati nyingi na Biblia inasema hivyo

Kijana uje na facts za maana
 
Tuonyeshe alitupiga fix wapi ?
Unbelievers are enemies of Allah and they will roast in hell. - 41:14

Kama alisema ukweli kwa nini hapa aagize tena wauawe?

Fight unbelievers who are near to you. 9:123
 
Hakuna mfuasi hata mmoja wa Yesu aliandika Biblia..
Kama unaweza nithibitishie
Mkuu narudia tena Biblia ni muunganiko wa vitabu vilivyoandikwa na watu tofauti... Yani maandiko yao yaliunganishwa na kuitwa biblia, na biblia imeandikw nyakati tofauti tofauti, kuna agano la kale lililoandikwa kabla ya Yesu na yesu alilikuta, na kuna agano jipya ambalo limeandika injili ya Yesu kristo... Biblia imeandikwa sio kwa pamoja bali kwa kukusanya maandiko kutoka kwa manabii wa kale, wanafunzi wa yesu na wafuasi wa Mungu
 
Yeremia hakuwa nabii
Unazungumzia katika Dini gani? Ndio maana na sema uislamu na ukristo ni dini zisizofanana

Katika Ukristo, Yeremia alikuwa nabii katika historia ya Israeli na katika Biblia. Yeye ni moja ya manabii mashuhuri wa Agano la Kale, aliyejulikana kwa unabii wake na ujumbe wa kiroho aliowasilisha kwa watu wa Israeli.

Yeremia alizaliwa karibu mwaka 650 KK na alitumikia kama nabii kwa karibu miaka 40, akihubiri ujumbe wa Mungu kwa watu wa Yuda, hasa wakati wa kipindi cha kushuka kwa ufalme wa Yuda kwa mikono ya Wababiloni. Alikuwa na jukumu la kuonya watu kuhusu hukumu za Mungu na kuwahimiza kurekebisha njia zao ili kuepuka msiba.

Maisha na unabii wa Yeremia yameandikwa katika kitabu cha Biblia kinachoitwa "Kitabu cha Yeremia," ambacho kinaelezea jinsi alivyohubiri na kushuhudia kipindi cha kisiasa na kiroho cha taifa la Yuda. Yeremia alikuwa nabii aliyejitolea sana kwa Mungu, akifanya kazi yake kwa uaminifu licha ya upinzani na mateso aliyopata.
 
Ndicho kilichopelekea Ukristo kuwa na madhehebu ambayo unayoyaona leo... Watu walianza kujitenga na kutengeneza madhehebu mengine baada ya kuona ukristo unapotoka kutoka katika asili yake halisi
 
Daah MB zako zikechakaa kwa kuandika utopolo
 
Ndio maana wadudu(finyofinyo) wanaweza kujitokeza wenyewe tu kwenye Nyama bila kuhitaji muumbaji.
Hao wadudu unaowazungumzia ni funza waliotagwa na nzi.... Leo hii wewe ukioza ukiwa nje ya dunia uwezi kutoa funza kwa sababu kule hakuna nzi... Au nyama ukiifungia kwenye chombo ambacho mdudu hawezi kuingia basi nyama itaoza bila kuwa na hao wadudu... Huo sio muujiza
 
Wakati ulipokuwa mchungaji ulikuwa unamhubiri mungu yupi?
Ulitumia kitabu gani?
Mkuu Nyakati za zamani zikishapita Ndo kipindi ambacho mtu akikumbuka Hujiona Jinsi gani alivyokuwa Mjinga..

Kwa mfano Huwezk waambia Wana wa Israel wale vyakula Vilivyo Najisi ambavyo walikula wakiwa misri wavile hivyo hovyo wakiwa Kanaani wakati Mungu amewapa maagizo ya KOSHER
 
Wazungu wameshtukia kama walikuwa wanapigwa , hakuna mungu anabariki mashoga, hakuna mungu watatu na mungu hajawahi kuwa na mtoto, mungu gani anateswa na yeye anamlilia mungu? Does it make sense kweli
Ndio shida ya kutokusoma maandiko ya biblia... Huo ushoga hata kwenye Sodoma na Gomorrah kwenye biblia ulikuwepo ukapelekea mungu kushusha gharika la moto katika miji hiyo...

Kwa kifupi biblia ilishatabiri hayo matukio yote, yesu mwenyewe ananukuliwa akisema nyakati za mwisho watatokea manabii wa uongo, watu watatumia jina la MUNGU kufanya maovu... Kwa mkristo anayejua dini vizuri hawezi kushtuka, na hili unabii utimie lazima yatokee haya tunatoyashuhudia leo.

Kuhusu kuwa na watoto, hili nilishazungumzia... Sio kila baba ni mpaka akuzae... Kwani baba yako wa kambo kakuzaa, mbona unamuita baba... Uumbaji ni jambo tosha la kumuita MUNGU Baba mkuu. Bila yeye wewe si kitu.

Kuhusu kuteswa Yesu, ni jambo lililo kwisha kupangwa, yani Yesu alitabiriwa kuwa atakuja na atakufa msalabani kwa dhambi zetu ili tujue ni jinsi gani MUNGU anatupenda mpaka anamtoa Yesu msalabani ili tuweze kumuamini... Ule ni utabiri hata malaika Gabriel alimwambia Mariam mama yake yesu kuhusu habari za yesu
 
Kuna watu wako hai na wanaoza viungo vyao na kutoa wadudu.

Je hao wadudu wanaletwa pia na nzi?
 
Sijaona jibu la swali mkuu.
 
Kama haujui vitu uwe unauliza. Uslam na Ukristu ni kama Harrier na Lexus au Nissan Dualis na Nissan Qashqai.

Ngoja nikupe ufananio.

1. Amri kumi za MUNGU walizopewa wakristo ndizo hizo hizo wanazofata na kushika waislam. Kama unabisha niambie wapi sio kweli.

2. Dini zote zina siku maalumu ya ibada, yaani Jumapili na ijumaa.

3. Dini zote wanatoa sadaka siku za ibada na siku za kawaida wanahimizwa kufanya zaka na sadaka binafsi.

4. Dini zote zinatumia lugha za kigeni yaani English,latin na kiarabu

5. Dini zote zinahimiza kutenda mema na kupiga vita uovu na ubaya.

6. Dini zote zina muabudu MUNGU, na zinamlaani shetani.

7. Dini zote zina vitabu vikuu yaani Bible na Msaafu vyenye mafundisho na kanuni za kale zenye maudhui ya kisasa.

8. Dini zote zinaamrisha maisha kuanza na Ndoa.

9. Dini zote zina role model figure yaani Mitume Yesu na Mohamed.

Hapo ni kwa machache tu nimekulistia ili ujionee kuwa kuna vitu vingi hizi dini zipo common na zinamuingiliano.
 
Mathayo alikuwa ni nani kwa Yesu ? Je alimuona Yesu ?
Nimeshasema mara kadhaa mathayo ni mwanafunzi wa Yesu, sasa wewe ni mwanafunzi alafu ushindwe kumuona mwalimu wako.... Sio alimuona tu, bali alitembea nae na kula nae

Ebu uliza swali lenye mantiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…