Thecoder
JF-Expert Member
- Aug 10, 2015
- 1,590
- 4,244
Torati ni Sheria na si Sheria zote zilitoka kwa the most high bali zingine zilikua ni mapendekezo binafsi ya Musa na kwenye hizi za mapendekezo binafsi zingine zilikua poa na zingine zilikua na utata na moja kati ya hizo zenye utata ni hiyo ya kuoa. Lakini pia ukifuatia utagundua zipo nyingi ambazo alizitengua kwa matendo kama ile ya kuponya siku ya sabato na kadhalika.K
Kwanini wasikae chungu kimoja?
Sasa hapo hatimizi, hapo anakuwa katengua, yaani ruhusa ya mke wa pili ye aseme mke mmoja sasa hapo anaikamilisha ama anaitengua sheria, angesema mfano mke wa pili awe hivi na hivi na vile, hapo sasa ndio anaikamilisha torati, anakamilisha pale ambapo hapajaelezea vizuri
Ndio maana watu mmekua mkidai katiba mara kwa mara kwasababu iliyopo haiendani na zama tulizopo, kwahiyo torati ilikua kama katiba ya waamini ila kuna mambo yalikua hayaendani na nyakati basi yakabadilishwa na sasa hivi tuko na katiba mpya ambayo ni mjumuiko wa mambo mapya na yale ya zamani ambayo bado yanafaa kuendelea kutumika.