Ukweli hausemwi. Kilimo cha Parachichi ni kigumu sana na pesa yake ni ndogo

Kama ulimsoma Napolean Hill ktk kitabu chake How to be rich.
Yeye anasema, ukiona umeanguka kwenye biashara basi fanya mara mbili yake.
Wale wasiojua structure of the markert and how it operate watajitoa taratibu na kubaki wajasilia mali halisi.
Mimi chuoni nilijifunza kwamba kila kitu kina utitiri hivyo ni wewe kushindindana na utitiri, na tatizo sio kuzalisha bali kuzalisha bidhaa bora na kuuza.
Marketing and selling is everything in business and entrepreneurship.
Ukishindwa kuuza wewe unakosa sifa za mjasiliamsli.
AVOCADO ni industrial crop sasa iweje ioze wakati ni bidhaa ya kiviwanda?
Sisi kama vijana tunatakiwa to innovate different products tuache ujinga wa kusubiri wazungu,wahindi, warabu na wachina kufikiri kwa niaba yetu.
I have alternative for my Avocado.
Bahati mbaya sijaanza kuuza zangu kushuhudia zinavyooza kwa kukosa wateja, ila parachichi zangu hazitaoza.
Ukichunguza uzalishaji wa Avocado ni subsistence agriculture, yaani ni tushamba twa kuokoteza ispokuwa Rungwe Company.
Sasa iweje unishawishi eti Avocado zimezalishwa sana wakati vishamba ni vya kuokoteza?
Avocado agriculture bado sans sana ktk ukubw, yani bado inaachwa na machungwa,chai, nduzi, miwa nk.
Mimi natamani nione mkulima mmoja walau minimum awe na heka 10.
Tujiuliza kikijengwa kiwanda kikubwa kitapata AVOCADO mda wote?
 
Mkuu
umenena yaliyo kweli kabisaa
kuna mwekezaji alikuja RUNGWE watu walikata mpaka kahawa wakaotesha parachichi
mwaka huu, wakulima wa parachichi mbeya wanalia,,mpaka serekali ya wilaya inawaomba wanunuzi waende.....wakajitokeza wakulima wakachangishana wakapeleka parachichi Njombe na FUSO KADHAA, wamefikisha wakapokelewa,,,ukaguzi umefanyika parachichi zikawa rejected zote tena wakaingia garama tena ya kwenda kutupa

Hiki kilimo kwa NJOMBE waliopiga pesa ni wale waliowahi wakauza MBEGU na wanaosoma ramani TU

Inahitajika ELIMU, mtaji wa kutosha na MUDA otherwise bora tufuge SAMAKI TU wanasema zinalipa
 
Hiyo ipo, lakini kwenye hivi vitu aisee kuna mbegu za aina nyingi sana. Wiki iliyopita nimeanzisha mradi wa bustani bamia, karoti, nyanya, nyanya chungu, spinachi, mchicha, chaina, matango, tikiti maji, sukuma wiki, pilipili.

Wakati naenda mjini kununua mbegu huko ndiko nilishangaa kukutana na mbegu za maajabu, aisee kuna bamia tangu nizaliwe sijawahi kuziona, ni kubwa kama tango. Wakati wa kununua mbegu za nyanya yule mzee kanipa za aina tatu hivi ila moja wapo kaniambia hiyo mbegu nyanya zake hukaa hata miezi miwili bila kuharibika baadae huwa ni kama zinanyauka vile. Na kuna mbegu zingine za nyanya japo sikuweza kuinua kutokana na bei yake kuwa juu kaniambia hii mbegu ukipanda unauwezo wa kuvuna nyanya zaidi ya miezi mitano
 
Hivi kuna kilimo ambacho hakina changamoto, ukienda kulima mahindi unakutana na hali ya hewa na soko, ukienda kulima mpunga utasikia mwaka huu mvua zimekata, kilimo cha kitanzania ni cha uwendawazimu uelewe hilo
Mahindi ni kilimo cha muda mfupi na una alternative, ni tofauti na Parachichi

Ardhi ya Tanzania ni nzuri sana kwa kilimo cha mazao mengi, tatizo la Tanzania ni KUKOSA MTAJI HASA NA KUTOKUWA NA TEKNOLOJIA YA KILIMO.
 
Kila zao ni la biashara, ila si kila zao ni la chakula kama tumbaku.
 


Kukurupukia hizi mambo shida sana, pole.
 
Watanzania twapenda kurupuka na wazee wa fursa
Wazee wa fursa ni wahuni sana. Wanalimia kwenye daftari na kupeleka taarifa za uongo Instagram na Facebook.

Miaka michache iliyopita walieneza taarifa za uongo kwamba ekari moja ya matikiti mtu anaweza kupata milioni 20 kwa mtaji wa shilingi 2M-3M.

Watu wakakuripuka, wakaangukia pua.
 
Mkuu tusaidie location ya huko uliko ili na sisi tuhame huku kwenye parachuchi
 
Migomba ilifyekwa mno, misitu ikachomwa moto na kuvunwa hovyo ili wapande maparachichi.

Kwa maana waliopanda mwaka juzi saivi wanalia tu,parachichi liliwafaidisha wale watu wa mwanzo kabisa miaka ya 2011 kidogo mpaka mwaka juzi.
Bila shaka ulikusudia kuandika 2021??
 
Je ukikomaa na soko la ndani tu je hailipi kweli kama wadau wanavyosema?
Mwaka huu nina project ya heka 20 na watu wana toa tahadhari nami siwezi puuza.
Mkuu soko la ndani limetawaliwa na wahuni na linaendeshwa kihuni, hivyo utapata hasara tu. Walanguzi kipimo chao ni kiroba cha kilo 25 unalipwa efu 3 au 5. Hutaki baki nayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…