TATIZO LA MAJINA YA KIISLAM KATIKA KUMBUKUMBU YA VITA VYA MAJI MAJI (1905 – 1907) MAHENGE SONGEA
Katika kumbukumbu ya Vita Vya Maji Maji Songea sehemu inayotia simanzzi kubwa ni pale penye kaburi kubwa la halaiki walipozikwa wazalendo 67 walionyanyua silaha dhidi ya dhulma za Wajerumani. Hawa walihukumiwa kunyongwa.
Kando ya kaburi hili la halaiki kuna kaburi moja lililo peke yake.
Hili ni kaburi la Abdulrauf Songea Mbano aliyenyongwa peke yake na kuzikwa kwenye kaburi la peke yake.
Hapo Mahenge ilikuwapo orodha ya majina ya wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam.
Lakini karatasi hii yenye majina ya Kiislam yamewekwa mbele ya majina haya majina mengine ambayo si ya Kiislam.
Linaanza jina lake la Kiiislam kisha lingine mfano Abdulrahman (Dominic) Mputa Gama.
Ingekuwa kama siku kuchomekwa jina lingine jina lingesomeka kama hivi, ‘’Abdulrahman Mputa Gama.’’
Kazi hii ilifanywa na padre kutoka Peramiho aliyeletwa Mahenge kuwabatiza Waislam kwa ahadi kwa kuwa wakikubali kubatizwa hawatanyongwa.
Orodha hii yenye majina ya Kiislam hivi sasa imeondolewa na badala yake kuna orodha mpya yenye majina mengine ambayo yanasomeka kwa mfano wa hapo juu, ‘’Dominic Mputa Gama,’’ badala ya ‘’Abdulrahman (Dominic) Mputa Gama.’’
Labda tujiulize nani anafanya haya nani anamtuma nini nia ya kufanya hivi?
Lipi lisilotakiwa lijulikane katika historia ya Vita Vya Maji Maji?
https://www.theeastafrican.co.ke/te...-7SNVfAliRvaeGuYtrn0n4dPKU1IGudszkPmpZuJpbqe0