Ukweli kuhusu Vita vya Majimaji

Ukweli kuhusu Vita vya Majimaji

vita ya maji maji ilipiganwa 1905-1907,
'rosary' ninavyofahamu kidogo ilianza kusaliwa 1917 baada ya bikira maria kuwatokea Lucia, Francis na Yasinta huko Fatma na kuwaamuru kusali rosary na kuieneza ibada hiyo duniani ili kuomba amani. (kama siko sahihi naomba kurekebishwa)

Sasa kama hivyo ninavyofahamu ndivyo; inakuaje kwenye picha za askari wa kitanzania waliopigana 1905/07 kuonekana wameshika rosary kama rosary ilikua bado haijaanza kusaliwa duniani??

Naomba kujuzwa hili nijue usasahihi wake.
 
Ukitaka kumfurahisha muislamu wewe mwambie kila kitu duniani ni matokeo ya uislamu.

Remote,
Hapa ni swali la Transatlantic Slave Trade.

Hayo mengine tukiyaleta hapa yatatuvurugia mnakasha.
 
Ukweli ni kwamba makabila ya kusini yalikuwa na imani zao za asili.
Mwarabu alipokuja akawaletea dini ya kiislamu kama ilivyo kwa wakristo.
Hivyo basi siyo wote walikuwa waislam hiyo siyo dini ya asilia imekuja tu kama nyingine zote zilivyokuja.
Mohamed jitahidi kuondoa hiyo element ya udini uliyonayo.
Kinjekitile aliitwa jina gani la kiislamu?
 
Kahinda,
Mimi bado sijasema lolote kuhusu Maji Maji.

Ikiwa unataka niingie In Sha Allah nifahamishe.
 
Hili ni swaki makini sababu kama ni Kweli waarabu walitengeneza uswahiba na waafrika kiasi hicho ni dhahiri kwamba maelfu kwa maelfu ya waafrika waliochukuliwa kama maswahiba a.k.a watumwa wangekuwa wengi sana huko uarabuni.

Wazungu ni makatili lakini waafrika wapo wengi mpaka wana mataifa yao huko latin America yenye dola kamili ya watu weusi Caribbean islands mataifa kama Haiti Trinidad and Tobago Jamaica etc.

Can you give us the statistics of how many wazungu were in those countries you mentioned, where are now originaly they were plenty of African slaves? And can you give the population count of Arabs in those countries where is what you claim there are many arabs but African slaves were killed?


For instance. Wazungu and Africans of Trinidad and Tobago and Arabsa and Africans of Oman, your newly politically acquired Bogeyman.
 
Jamaa kapiga porojo na hadithi halafu anaita historia. Historia ili iwe credible lazima kuwe na source. Tena vyanzo vijumuishe primary and secondary zionyeshwe kwenye footnote ili ku-authenticate reliability and validity. Hizi footnotes lazima zionyeshe wapi source inapatikana, zimetokea wapi na lini lilipatikana. Weye unabwabwaja kama chiriku halafu unaita eti ni historia.
 
Kwa niaba yake nakuomba useme kuhusu Maji Maji mzee ili na sisi tuelimike.

Chipanga,
Hayo hapo chini ni kutoka kitabu changu: "The Life and Times of
Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle
Against British Colonialism in Tanganyika," Minerva Press London, 1998.

Hivyo vita ninavyovieleza ni Vita Vya Maji Maji na hayo mawasiliano ni kati
ya baadhi ya viongozi wa vita hivyo.

Soma kwa utulivu na tafakari:
[TABLE="width: 601"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Islam has always been the ideology of resistance against colonial rule or any
other authority which tried to subjugate Muslims.

Consequently, no government in power either indigenous or foreign has ever
been kind or supportive to Islam, and likewise Muslims have always been
engaged in a continuous struggle to preserve their faith and fight for their
rights.

Christianity was resisted by Muslims right from the beginning.

In any uprising against the colonial government, Muslims took the opportunity
to attack missionaries and Christian establishments.

Muslim perceived both missionaries and the colonial government as fellow
collaborators and therefore enemies to Islam.

Islamic radicalism has therefore a long history in the struggle against colonial
rule and Christianity.

Christianity became a reactionary force siding with the colonial authority.

One needs only to read the letter written by the Chief Songea bin Ruuf at
the time when he was mobilising his people for war while at the same time
trying to cement alliances with other chiefs in Southern Tanganyika and
across River Ruvuma in Mozambique.

This letter written to Sheikh and Sultan Mataka bin Hamin Massaninga
reads:[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]"Sultan Songea bin Ruuf writes: To the Shaykh and Sultan Mataka bin
Hamis
Massaninga.

Greetings, etc.

I am sending you a letter through Kazembe.

We have received an order from God that the Europeans must leave the
country.

We are in the process of fighting them here. I believe that we have long
since been reconciled,[so] send me your children, so that we may make an
alliance.

I had wanted to send you some cattle as a gift, but am not able to[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]do so, as the war which God desired is continuing.

Send me a hundred riflemen, and support me in storming the Boma (Songea).[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]I am also sending you a flask of the Prophet Muhammad, which contains the
means for conquering the Europeans.

Have no doubt about it, it possessed great power.

And when we have taken the Boma (Songea), we shall go on the stations on
the Nyasa together, you and I.

Now, let us forget our old quarrels.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]This bottle, with a da’wa, has been sent by Chinyalanyala himself, the war
leader.

He also sends the container (kombe), and sends you many greetings.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]If your men will come, then Chinyalanyala himself will come and will give you
many of the holy things.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Hassan bin Isma’il greets you.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Many salutations,[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Sultan Songea bin Ruuf[1][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]A point to note here is that this letter, beautiful as it is, it is being doubted
by Becker, who maintains that the origins of the letter are dubious.[2]

This is the stand which many Christian researchers have taken when faced
with the realities of Islam in Tanganyika.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[1]C.H. Becker, ‘Material for the Understanding Islam in German East Africa’,
Tanzania Notes and Records, No. 68, February, 1968, p.58.

[2]Ibid.
 
atapata tabu na wewe kwa kuwa umekwenda hadi istanbul tena ukapiga picha na prof mohamed bakari, naye ukamsomesha hizo hadithi? ???????

Ninaona utasumbuka sana wewe kuwashawishi watu juu ya uelewa wako hata kama unaweka picha ulizopiga na kina wasira n.k, kwa sababu hakuna mtu duniani anajali unapigaga picha na nani hadi aelewe kwamba unafahamu.

Unaweza kulazimisha hoja masikioni mwa watu lakini kinachoingia akilini na moyoni, huna uwezo wa kukifahamu tu richa ya kukicontrol.

Ehhhe, leta picha zingine ulizopiga na sadamu hussein!.

CHADEMA islamophobes beware the Ides of October 2015
 
Unaongea utafikiri waarabu walikuwa malaika wazungu walikuwa makatili sana ila hawatafikia ukatili wa waarabu sababu hao waliwakatili wazee wetu wao pamoja na kizazi chao wote makatili wakutupwa makafiri kabisa.

"wajerumani walipoingia walikuta makadhi na watu woote wakiwa katika imani ya kiislam huku maisha yakienda bilaa matatizo yoyote "

albuluushiy una uhakika na usemi huo?

Swali chokonozi....

Kwa nini hakuna "Black Arabs"

Hili ni swaki makini sababu kama ni Kweli waarabu walitengeneza uswahiba na waafrika kiasi hicho ni dhahiri kwamba maelfu kwa maelfu ya waafrika waliochukuliwa kama maswahiba a.k.a watumwa wangekuwa wengi sana huko uarabuni.

Wazungu ni makatili lakini waafrika wapo wengi mpaka wana mataifa yao huko latin America yenye dola kamili ya watu weusi Caribbean islands mataifa kama Haiti Trinidad and Tobago Jamaica etc.

Wapo waafrika walioenda huko uarabuni. Kwa kukimbia vita na kuzamia na wamelowea huko karne ya 19 lakini waliochukuliwa kama maswahiba hakuna kizazi chao wanaume walihasiwa na hiyo ndio iliyokuwa VISA ya kuingilia uarabuni.

waarabu weusi ni wa asili tofauti na wazungu weusi ni wale walokwenda utumwani

Tabby,
Umeingia mjadala katikati na ndiyo maana ukawa hujui mantiki wala historia ya mimi kuweka picha.

Umefanya haraka labda ungesubiri Ngongo mwenyewe anijibu ungeelewa.

Nimeanza na picha niko BBC Studio za Glasgow nafanya kipindi cha historia ya Africa.

Ikaja picha niko Berlin, Zentrum Moderner Orient namalizia kuandika kitabu.

Kisha Geneva United Nations.

Halafu London Tower Bridge.

Na Prof. Ali Mazrui Nile Hilton, Kampala.

Nyingine Harlem, New York....nk. nk.

Nyingine Capitol Hill Washington. ..

Mimi sikukulazimisha kunijibu...

Umeingia kwangu kwa kutaka mwenyewe. ..

Nilisahau picha nyingine Library of Congress, Washington. ..

Hayo ya Sadam ni hamaki zako.
Pole sana.

Sioni sababu ya mie kujibu kejeli.

Naamini ushanifahamu.
Ukipenda kunijua zaidi ingia hapa: www.mohammedsaid.com

Mkuu unamaanisha wakristo ndio wavivu wa kusoma?

Hizi dini za kuja bure kabisa...bora dini zetu ''za ujima'' ambazo hazikutuharibu uwezo wa kufikiri!

Hivi kabla ya kuja kwa wazungu wakoloni ni nani alianzisha biashara ya utumwa Afrika Mashariki? Ni nani alikuwa anawatoboa waafrika miguu na kuipenyeza minyororo?
-Ni nani alikuwa anawahasi waafrika ili wasizae na mabinti zao?

-Ni nani alianzisha usultan zanzibar?

-Lakini pia hayo mangome ya kilwa naa kwingineko unakozungumzia ni nani aliyoijenga?

-Na hiyo dini unayoitetea na kuiona ya haki uliletewa na nani? Kama wasingekuja waarabu je ungekuwa muislam? Hahaha...

Za kuambiwa/za kusoma.....changanya na zako, Sioni sababu ya kutengeneza mazingira ya udini kwa karne hii zaidi ya kufanya maendeleo zaidi.

Nemulo,
Ukitaka historia ya utumwa itabidi kwanza usome Transatlantic Trave Trade.

Unaijua?

safi kwa makala nzuri, cku nyingine utuletee jinsi waafrika walivyoteswa na waarabu kwenye biashara ya utumwa

Mzee! Respect to you. You are a great man your achievement are so good.
It is said that kama hujui ulipotoka hutajua unapoenda, wewe ni msomi, sisi weusi it is obvious na kuna proofs nyingi msomi kama ww utakuwa ulikutana nazo tulikuwapo kabla hata ya hizi dini za walowezi kuingia, we were great men of kush we had our gods and we did built pyramids, mathematics, philosophy, governments and so many more.
Kwanini wasomi kama nyie mnazdi turudisha kwa slaves masters way of worship and mind slavery. You supposed to educate the masses abt the truth, muslim christianity etc hizi si dini za watu weusi si tamaduni zetu hizi.
Let us emancipate our selves from mental slavery.

Waarabu waliuwa watumwa wote walipelekwa uarabuni.
 
27 / 2/ 1906, Vita vya Majimaji ni vita vilivyopiganwa na wazee wa kiislamu kupinga utawala wa kimabavu wa Kijerumani, lakini kwa makusudi vita hivi historia yake imechafuliwa kwa makusudi kuonesha kuwa vilikuwa vita vilivyopiganwa kwa imani za kishirikina.

Ikumbukwe kuwa kusini mwa Tanzania kuna mkoa unaitwa Lindi, ambapo ndani ya mkoa wa Lindi kuna wilaya inaitwa Kilwa ambapo hapo mwanzo ilikuwa ni dola kamili ya Kiislamu iliyokuwa na utawala kamili na kutumia pesa yake na kuhukumu watu kwa mujibu wa dini ya Kiislam, ambapo kanda yote ya kusini mwa Tanzania walikuwa wanafuata mfumo wa kiislam.

Wajerumani walipoingia walikuta Makadhi na watu wote wakiwa katika imani ya Kiislam huku maisha yakienda bila matatizo yoyote, Wajerumani wakaanza na kufanya mambo ambayo hayakukubalika katika jamii kwa kulazimisha ili malengo yao yafikiwe, maafisa na askari walikuwa wanatembea na rozari na kulazimisha watu kuwa Wakristo kinguvu, baadhi ya maaskari walibaka wanawake wa kiislam ndani ya maboma yao na huko mashambani, hata waislam walipotaka kujua kwanini wake zao au mabinti zao wanabakwa, walijibiwa majibu ya karaha na dharau.

Ndipo chuki ilizidi kuwa juu ya Wajerumani, wazee wa kiislam waliwahimiza vijana wao kujiandaa kwa kujikomboa kutoka katika utawala wa kikafiri, wakisema wakati wa dola ya Kiislamu mambo haya hayakuwepo na iweje leo, ndipo kiongozi wa Wamatumbi aitwae Kinjeketile Ngwale aliwaongoza wapiganaji wa Kimatumbi kupambana na Wajerumani, wakati wote huo ukatili wa Ujerumani ulikuwa unajulikana kote kusini, wakati vita vinaanza na vilianza kwa nguvu kubwa, Wajerumani waliua kila walieona huenda ni adui yao, majeshi ya Ujerumani wakaanzisha kampeni kubwa kukamata kila waliemuona katika majumba ya ibada.

Kumbuka wakati huo nyumba za ibada ilikuwa ni Misikiti na kila wakati wa sala majeshi ya Ujerumani yalivamia misikiti na kumkamata kila waliemkuta humo, ndipo chifu wa Suleymaan Mamba wa kabila la Wamwera akatangaza vita kwa watu wake kuwa kila atakapoonekana Mjerumani akatwe kichwa, nae chifu Abdallah Chami wa kabila la Wangindo nae akatangaza vita rasmi kwa Wajerumani, nae chifu Mataka Ambunje wa kabila la Wayao nae akatangaza vita rasmi na Wajerumani, haikutosha nae Chifu Songea Rauf Mbano wa kabila la Wangoni nae akatangaza vita Wajerumani, na hapo makabila matani makubwa Kanda ya Kusini wakawa wanapigana na Wajerumani, na baadhi ya makabila madogo madogo nayo yakawa yanapigana kuwasaidia ndugu zao dhidi ya Majeshi dhalimu ya Ujerumani.

Makabila hayo ni kama Wandendeule, Wamatengo, Wambunga, Wandamba n.k. Wapiganaji wa vita hivyo mnamo tarehe 5/8/1905 walivamia misheni ya Kanisa Katoliki huko Nachingwea na kufanya shambulio la kustukiza na kuua makumi ya wanajeshi wa Ujerumani na kumuua Askofu Cassian Speis ambae huyu ndio alikuwa Askofu wa kwanza Dar es salaam.

Na mnamo tarehe 14/8/1905 wapiganaji hodari walivamia boma la Mjerumani na kufanya uharibifu mkubwa hali iliyopelekea mapigano makali yalioacha majeruhi na maiti kila upande, wapiganaji wengi walikuwa wanatumia mishale, mikuki, mundu, silaha za jadi na bunduki kadhaaa walitoka baada ya kuwaua majeshi ya Ujerumani, na Mjerumani akitumia bunduki za moto na kupelekea majeshi ya wazalendo kuzidiwa nguvu na Mjerumani kushinda vita hivyo.

Ikumbukwe majeshi ya mjerumani walikuwa wanachoma majumba moto ili kuwakamata wanaume lakini waliokuwa wanaungua mpaka kufa walikuwa ni watoto na wanawake. Nje kidogo ya mji wa Songea kuna kitongoji kinaitwa Mahenge, hapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji. Jambo kubwa la mahala hapo ni kaburi kubwa la halaiki ambamo askari zaidi 67 walizikwa kwa pamoja. Na kando ya kaburi hilo la pamoja kuna kaburi la Ally Songea Mbano ambae yeye alizikwa peke yake.

Kwa mara ya kwanza nilitembelea Makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona wakubwa wa kituo hicho.

Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko. Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo, na badala yake imewekwa karatasi nyingine ambayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza muhudumu kulikoni? Akasema, “Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi. Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka.

Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Ally Songea Mbano. Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.

Ukiingia ndani ya kinyumba cha ghorofa, unaanza kuona picha za mashujaa wa Maji Maji wakiwa wamevaa mavazi ya vita mithili ya mahujaji wanavyovaa Ihraam wakati wa hija. Kinachoongezeka kwao ni vilemba kichwani. Chini ya kila picha kuna jina la aliyekuwa kwenye picha ile. Ukipanda gorofani utaona silaha za kijadi kama mikuki, pinde, ngao n.k. Kinachosisimua zaidi ni mavazi ya vita. Mavazi ya vita ya askari wa Maji Maji wengi walivaa kanzu za Kiislaam na vilemba.

Jambo jingine linalosisimua ni kile ambacho watu wa kituo hicho wameandika ”rosary” hili ni jina la Kikristo, hasa la Kikatoliki, ni zile shanga ambazo huning’inia msalaba lakini unapotazama hicho kilichoitwa “rosary” utaona si “rosary,” bali ni tasbihi hasa ya Kiislaam yenye kupangika hasa shanga zake, 33, 33,34. Maneno yaliyoandikwa kuelezea “rosary” hizo ambazo ni tasbihi ni;

“Hizi ni rosary ambazo wapiganaji wa Majimaji walikuwa wakitumia KUTAMBIKA kabla ya kwenda vitani kwa kuamini kwamba zitawakinga na risasi. ”Ukweli ni kwamba hawa askari wa Maji Maji wengi walikuwa ni Waislaam hivyo hawakuwa WAKITAMBIKA bali walikuwa wakitumia tasbihi hizo kufanya dhikri kwa Allah kabla ya kwenda vitani. Midhali sisi Waislaam hatujawa tayari kuandika historia yetu kama Waislaam wanaotuandikia watapotosha na kupindisha na kutuzulia wanavyotaka.

Hapo gorofani kuna jambo jingine la kusisimua. Kuna magudulia na makopo. Wameandika kuwa, haya ndio makopo ambayo askari wa Maji Maji walikuwa wakiyatumia KUNAWA kabla ya kwenda vitani [kushika udhu na sio kunawa] pia kwa kuamini kuwa maji hayo yatawakinga. Muhudumu alitueleza kuwa kumbukumbu nzuri na za kuaminika ziko Jimbo Kuu la Wakatoliki Peramiho. Tulikwenda jimboni lakini hatufanikiwa kwa sababu za ki-urasimu tu. Tulitakiwa tupate kibali cha Askofu Mkuu. Hatukukipata.

Kwa yale tuliyoyaona na kuyashudia yafuatayo;

Vita vya Maji Maji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao. La. Vilikuwa ni vita vya Waislaam wakipigana na Wakristo wa Kijerumani waliovamia maeneo asilia ya Waislaam kwa lengo la kuuwa Uislam na kusimamisha Kanisa kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya Maji Maji ni mazingira ya Kiislaam, kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa Kijerumani ila katika miji ya Waislaam kama Kilwa, Bagamoyo n.k.

Kwa nini wauliwe maeneo ya Waislaam tu? Walifuata nini huko? Kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya Maji Maji. Vinaoneshwa kama ni vita vya wazalendo wakipigana na wakoloni wa Kijerumani, wakati ukweli si hivyo. Ukweli ni kwamba vita vya Maji Maji vilikuwa ni vita baina ya Waislaam na Wakrito wa Kijerumani, Waafrika Wakristo wa Songea walijiunga na Wakristo wenzao wa Kijerumani dhidi ya Waafrika wenzao wa Kiislam. Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao.

Kuna haja ya wasomi wetu wa Kiislaam kufanya juhudi za makusudi za utafiti wa historia yetu ili kukifanya kizazi hiki cha Kiislaam kujitambua zaidi na kujenga ujasiri. Taasisi za Kiislaam na watu binafsi [matajiri] wawawezeshe kiuchumi wasomi hawa kufanya kazi hii. Mwaka 2008 nimetembelea Kilwa Kisiwani, huko nikamkuta Mzungu wa Kifaransa akiandika historia ya Kilwa Kisiwani akiitwa Thiery, ameweka kambi na majenereta ya umeme, solar power na makompyuta. Kazi nyingine kubwa alokuwa akifanya ni kukarabati yale magofu ambayo mengi ni Misikiti na majumba ya mawe ya wafalme wa kale.

Kilwa Kisiwani ni moja kati ya dola kubwa za Kiislaam katika mwambao wa Afrika Mashariki, ndio dola ya mwanzo kuwa na sarafu yake ambayo iliandikwa jina la Allah. Tuliposoma kazi ile ya Yule Thiery Mfaransa tayari alikwisha ipotosha kwa kiasi kikubwa. Sikuwa na la kumfanya. Kizazi cha vijana wa Kiislaam hakitopata historia ya kweli ya Kiislaam kama tutawaacha akina Thiery waandike na hivyo vijana wetu hawatajitambua na hawatokuwa na ujasiri katika Uislam wao.

Maisha yao ya kila siku, hawa wanajua ni nini hasa wamekifanya kwa wazee wetu, kuanzia kwa Chifu Kimweri mpaka Chifu Mkwawa, wanasema etia mejiua, ni nani anaweza kujiua mpaka kukin’goa kichwa chake jamani?!

Majeshi yaliyofanya mauaji dhidi ya wazee ni Major Johannes, Captain Mortz Merker, Luteni Spiegel, Staff Sajent Engalnd na wengineo!

Ewe Allah (S.W.T.), Wazidishie adhabu hao madhalimu wa Kijerumani, Amiiyn!

Ahsateni, Nakutakieni siku njema!

Kuna kitu kanisa katoliki linaficha.
Mkuu hongera. Ila tunaitaji more references.
 
Waarabu waliuwa watumwa wote walipelekwa uarabuni.

Naifahamu vizuri Trans Atlantic Slave trade(Triangular slave trade) ilikuwa ni ya Western Africa zaidi,na ni tofauti na East African Slave Trade iliyofanywa zaidi na waarabu.
 
Remote,
Hapa ni swali la Transatlantic Slave Trade.

Hayo mengine tukiyaleta hapa yatatuvurugia mnakasha.

Sawa,hebu Mohamed Said naomba utupe wewe historia ya vita vya majimaji tena bila kumsupport mleta mada kwa kuwa ni muislam mwenzio na pia bila kudharau dini nyingine yoyote.

Tafadhali tusaidie hilo.
 
Last edited by a moderator:
Sawa,hebu Mohamed Said naomba utupe wewe historia ya vita vya majimaji tena bila kumsupport mleta mada kwa kuwa ni muislam mwenzio na pia bila kudharau dini nyingine yoyote.

Tafadhali tusaidie hilo.

Nemulo,
Nitoe mimi "historia ya Vita Vya Maji Maji" na "bila ya kumsupport mleta
mada kwa kwa kuwa ni Muislam," na "pia bila ya kudharau dini nyingine."

Ikiwa haya ndiyo masharti yako inaelekea hunijui kwa kuwa siko hivyo.
Mimi naandika kile ninachokijua tena kwa adabu zote.

Vita vya Maji Maji nimevieleza katika moja ya post zangu za nyuma na ni
kutoka kitabu changu.

Soma post #61 .
 
Naifahamu vizuri Trans Atlantic Slave trade(Triangular slave trade) ilikuwa ni ya Western Africa zaidi,na ni tofauti na East African Slave Trade iliyofanywa zaidi na waarabu.

Nemulo,
Umesahau kuwataja wahusika wa Transatlantic Slave Trade.
Ila umekumbuka kuwataja wa East African Slave Trade peke yao.

Barza inasubiri uwataje na hao wengine walikuwa kutoka utaifa upi?
 
Nemulo,
Umesahau kuwataja wahusika wa Transatlantic Slave Trade.
Ila umekumbuka kuwataja wa East African Slave Trade peke yao.

Barza inasubiri uwataje na hao wengine walikuwa kutoka utaifa upi?

Nijuavyo wahusika wa Trans Atlantic slave trade ni European(wazungu na ndio walioconduct),waafrika(watumwa) waliopelekwa utumwani kuwork kama vibaraka Amerika pamoja na baadhi ya waamerika(wakati huo ni red Indians)
 
Wengine walihasiwa kabisa, hizo historia mzee wala hazitafuti.
 
Kuna kitu kanisa katoliki linaficha.
Mkuu hongera. Ila tunaitaji more references.

Cerengeti,
Hebu msome Chief Songea anavyotokea katika utafiti wa Baker hapa chini:

[TABLE="class: cms_table, width: 601"]
[TR]
[TD]One needs only to read the letter written by the Chief Songea bin Ruuf at
the time when he was mobilising his people for war while at the same time
trying to cement alliances with other chiefs in Southern Tanganyika and
across River Ruvuma in Mozambique.

This letter written to Sheikh and Sultan Mataka bin Hamin Massaninga
reads:[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]"Sultan Songea bin Ruuf writes: To the Shaykh and Sultan Mataka bin
Hamis
Massaninga.

Greetings, etc.

I am sending you a letter through Kazembe.

We have received an order from God that the Europeans must leave the
country.

We are in the process of fighting them here. I believe that we have long
since been reconciled,[so] send me your children, so that we may make an
alliance.

I had wanted to send you some cattle as a gift, but am not able to[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]do so, as the war which God desired is continuing.

Send me a hundred riflemen, and support me in storming the Boma (Songea).[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]I am also sending you a flask of the Prophet Muhammad, which contains the
means for conquering the Europeans.

Have no doubt about it, it possessed great power.

And when we have taken the Boma (Songea), we shall go on the stations on
the Nyasa together, you and I.

Now, let us forget our old quarrels.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]This bottle, with a da'wa, has been sent by Chinyalanyala himself, the war
leader.

He also sends the container (kombe), and sends you many greetings.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]If your men will come, then Chinyalanyala himself will come and will give you
many of the holy things.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Hassan bin Isma'il greets you.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Many salutations,[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Sultan Songea bin Ruuf." [1]

Kutoka: Mohamed Said, "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of The Muslim Struggle Against British Colonialism in Tangnayika, Minerva Press, London 1998."[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Sultan Songea bin Ruuf huyu hapo juu ndiyo huyu anayoelezwa tena hapa chini kama Chief
Songea Mbano?:


"Anasema hali hiyo ilitokea kwa sababu Chifu Songea Mbano alikuwa ndiyo Jemedari Mkuu
wa Jeshi la Wangoni na alikuwa ni hodari sana asiyeogopa lolote kwa hiyo Wajerumani walitaka
abakie ili wamtumie kwa malengo yao.


"Yeye Chifu Songea alidai na yeye anyongwe kama walivyonyongwa ndugu zake, basi alinyongwa
na Wajerumani ambao waliondoka na kichwa chake wakiwa wamekiweka ndani ya kasha kwenda
Ujerumani ambako hakijarudi hadi leo na kiwiliwili chake kuzikwa katika kaburi la peke yake."

(Kutoka:https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/64754-historia-ya-vita-vya-majimaji.html)


Wanajamvi
Naamini mnaiona tofauti iliyopo.
Au hawa ni machifu wawili tofauti?

Nani anahusika na uchakachuaji huu wa majina haya ya Kiislam katika historia ya Vita Vya Maji Maji?
 
Back
Top Bottom