Kwamba Mungu leo haongei na watu...alishia kuongea na Musa Peke yake sio...? Hebu tusome ile Kut :20:8 na kuendelea tujadiliane .....
St. Paul katika Epistles zake anasema "Kama Mussa alivyomunua nyoka wa Shaba, ndivyo hivyo mwana Wa Adam atainuliwa kwenye msalaba na kila amtizamaye kwa imani atapona..."
Ndio maana Msalaba(Crucifix) upo juu mbele ya altare
Leta hayo maandiko tuyachambue hapa..sio unaleta blah blah
Mkuu soma kwa makini post zangu,ukipanic hutanielewa,na kama unataka kuelewa weka pembeni dini yako simama katika biblia.
Nimesema Mungu hata leo anaongea na watu,kwa hiyo kama aliongea na wewe uweke sanamu hizo wewe ulitakiwa tu useme Mungu aliongea na St.Otorong'ongo akamwambia atengeneze sanamu simple like that.hapo hatujazungumuzia kama sura ya Yesu iliyopo ni ya kweli au ni ya zile movie,najua uliambiwa milipatikana kutoka kwenye kitambaa cha yule mwanamke aliyemfuta yesu.I have been where you are,baada ya kutumia kama miaka 2 natafuta kweli,nilihama chombo cha usafiri nikapanda kingine.
Nikuulize yule nyoka wa shaba aliyetengenezwa na Mussa baada ya issue ya nyoka kuwauma wana wa israel kuisha biblia imesema alipelekwa wapi?Je walimtunza wakawa wanaendela kumwinua muda wote wakati issue ya nyoka imeshaisha?
"Kama Mussa alivyomunua nyoka wa Shaba, ndivyo hivyo mwana Wa Adam atainuliwa kwenye msalaba
na kila amtizamaye kwa imani atapona..."Hili andiko usilitumie vibaya,utaona linakubaliana na nilichokisema mwanzo kwamba waliomtazama nyoka wa shaba walipona.Hapo unatakiwa umtazame Yesu na kumtazama Yesu hakumanishi kuangalia picha yake au sanamu yake,toka mwilini.Inamanisha umkimbilie yeye,umtumainiye yeye,umwamini yeye kwamba anaweza kukusaidia.Angalia hapo red highlighted,kwa hiyo andiko lilipo sema na kila amtizamaye yeye kwa imani atapona,mkaona mtengeneze sanamu ili watu waitizame kwa imani?Hapo umepotea,brother kama ni msomaji wa biblia soma ukiwa na biblia ya kiingereza na kiswahili kuna muda utagundua kitu fulani wanapotafasiri kutoka kiingereza kuja kiswahili.
labda nikuelezee kwa urahisi,kwa kutumia andiko lako hilo hilo,je kwa kuwa Yesu wako bado yuko msalabani,mimi Yesu ninayemwamini kwa sasa hayuko msalabani ameketi kuume kwa Baba au biblia yako inasemaje?Wewe umemuweka msalabani miaka nenda miaka rudi,kaka tuache ushabiki,soma biblia yako utaijua kweli.Na ukiniletea ushahidi wa watu waliomtazama huyo mliye naye kwa imani wakapona mimi nitarudi Rumi.
Samahani sana najua haya mambo mazito lakini kuna watu wanafunguliwa na macho yao yanatiwa nuru kwa jina la Yesu aliye hai,ufahamu wao wa neno la Mungu unaongezeka kwa jina la Yesu.
Huwezi kujaza maji kwenye glass ambayo tayari kuna maji yamejaa,ukitaka kuweka maji mapya lazima utoe ya zamani.Ondoa elimu yako ya zamani kubali kujifunza,unaweza usinielewe leo ukanielewa mwishoni mwa mwaka it is ok,najua adui hajalala.