Niseme japo kwa kifupi kuhusu lawama zako kwa mwalimu hayati JK Nyerere juu ya elimu ya Tanzania.
Mwalimu alipokea nchi toka kwa wakoloni ikiwa na kundi dogo sana la wasomi, na kundi jingine dogo la wanaojua kusoma na kuandika tofauti na majirani zetu.
Kazi ya kwanza ilikuwa ni kupunguza kundi la wasiojua kusoma na kuandika ambalo lilikuwa kubwa zaidi.
Akawa na kazi ya pili ya kuwasomesha vijana watakaosaidia katika idara nyeti kama madaktari na wahandisi. Kumbuka nafasi tunapopata uhuru zilikuwa zimeshikwa zaidi na wageni japo na wenyeji kidogo walikuwepo.
Haikuwa kazi rahisi kwa uchumi wa wakati huo kutoa elimu ya juu kwa watu wengi. Lakini alipambana kujenga shule za msingi,sekondari na chuo kikuu ili kuongeza idadi ya wasomi.
Alitumia wasomi wa idara mbalimbali kama walimu katika maeneo yao. Kwa mfano walimu mahali popote walipo walitakiwa kufundisha si tu wanafunzi, bali hata watu wazima katika eneo hilo japo wajue kusoma na kuandika.
Aliandika vitabu vya elimu ya watu wazima kwa mkono wake na wadau wengine, vikiwa na taaluma mbalumbali kama upishi, ufundi nk.
Kama haitoshi, ili kukuza kwa haraka elimu kwa wananchi, alianzisha mpango wa UPE (universal primary education), mpango ambao umerudiwa na Rais Magufuli. Mpango huu ndiyo ulioipa Tanzania sifa ya kuwa na wananchi wengi wanaojua Kusoma na Kuandika katika bara la Afrika mwishoni mwa miaka ya 70 hadi mwanzoni mwa miaka ya 80.
Kifupi mwalimu alipambana sana kuiinua Tanzania. Kumbuka haikuwa rahisi kutokana na mabeberu kuwakandamiza waafrika kupunguza kundi la wasomi wasijeleta upinzani wanapotaka kutunyonya.
Kama unaweza kujifunza, jifunze kwanini viwanda vya vyetu vilijengwa kisha vilikufa kwa haraka sana. Moja ya sababu ilikuwa ni kukosa vipuli na nguvu kazi (wataalam) kutokana na wazungu kugoma kuendeleza wataalamu wetu na kutuuzia vipuli.
Kama siyo juhudi zake Nyerere, tungekuwa na maisha kama ya Kenya. Sipati picha ingekuwaje.
Sent from my Infinix X688B using
JamiiForums mobile app